SHULE ya sekondari ya garijembe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya imeteuliwa na halmashauri hiyo kuwa shule ya wasichana.
Lengo la kuteuliwa kwa shule hiyo
kuwa shule ya wasichana ni kuwaepushia adha ya kupatwa magonjwa na mimba
zisizotarajiwa wanafunzi wa kike wanaoishi katika nyumba za kupanga wakati
wakisoma katika shule mbalimbali za sekondari zilizopo wilayani hapa.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Sigala
amesema baada ya kuliona hilo uongozi wa halmaashauri na wilaya umepitisha
maamuzi ya kuiteua shule ya Garijembe kuwa mahali salama kwa wanafunzi wa kike
badala ya kujipangia mitaani.
Amewataka madiwani kuhakikisha suala
hilo wanalipa kipaumbele na kuhakikisha miundombinu inayohitajika inajengwa
ikiwa ni pamoja na mabweni ili wanafunzi wa kike waanze kunufaika na mkakati
huo.
Amesema uwepo wa shule hiyo
itakayowaweka katika mazingira salama wanafunzi wa kike utakuwa ni ukumbusho
mzuri pia wa utawala wa madiwani waaliopo hivi sasa kwakuwa watakuwa wameleta
mchango mkubwa katika kuinua elimu wilayani kwao.
Amewataka madiwani pia kuhamasisha
wananchi kuchangia shughuli za uboreshaji na ujenzi wa miundombinu mipya
shuleni hapo ili shughuli hizo zikamilike kwas wakati.
No comments:
Post a Comment