Mkurugenzi wa Maendeleo wa kanisa la Anglikana dayosisi ya kanda ya Nyanda za juu kusini Padre Jonathan Mwashilindi(kushoto) akitoa maelezo ya namna miradi inayofadhiriwa na Wamarekani
Wabunge wakikagua bidhaa za mikono zilizotengenezwa na wanavikundi
HABARI KAMILI
WAJUMBE tisa wa kamati ya bunge la Congres la
Marekani wamefanya ziara ya siku moja kutembelea miradi inayoendeshwa na kanisa
la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za juu kusini inayofadhiriwa na serikali ya
Marekani kupitia shirika la Watereed.
Miradi inayoendeshwa na kanisa hilo kwa ufadhili wa
wamarekani ni ule wa Kupinga ukatili wa kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya
watoto(VAC),Ushauri na upimaji virusi vya ukimwi kwa hiari,Vikundi vya uzalishajimali
na mradi wa Elimu ya kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Wakiwa jijini Mbeya wabunge hao wamekagua shughuli
mbalimbali zinazofanywa kupitia miradi hiyo kupitia hafla fupi ya maonesho
iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mbata kabla ya kurejea jijini
Dar es salaam.
Katika hafla hiyo fupi,wabunge hao ambao
wameongozana na maafisa wachache kutoka ofisi ya Wizara ya Afya walitaka kujua
idadi ya watu ambao wamekuwa wakihudumiwa kupitia miradi inayofadhiriwa na
wamarekani na pia namna vikundi vinavyonufaika na miradi hiyo.
Akizungumzia,ujio wa wabunge hao Askofu wa kanisa la
Anglikana Dayosisi ya nyanda za juu kusini John Mwela aliiwashukuru watu wa
Marekani kwa upndo wao wa kuendelea kufadhiri miradi yenye lengo la kuistawisha
jamii ya watanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo wa kanisa la
Anglikana dayosisi ya kanda ya Nyanda za juu kusini Padre Jonathan Mwashilindi amesema
kanisa limejipanga kuwahudumia watu walio katika hali hatarishi zaidi kwa kuwafikia
na kuwapa elimu.
Amesema pia kanisa limejipanga kuimarisha klabu za watu
waliopima ambazo uanachama wake haujalishi kuwa mtu aliyekutwa na maambukizi ya
VVU au hana ili kuziwezesha kuwa na miradi ya kujiongezea kipato.
Amesema kwa kuziimarisha klabu hizo kutatoa fursa
kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuwa na njia za kuimarisha kipato chao
na kuondokana na utegemezi.
No comments:
Post a Comment