Kaimu katibu tawala mkoa wa Mbeya Bw.Costantine Mushi
akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku tatu ya Mafunzo ya watoa huduma wa
mradi wa KFW inayofanyika katika kituo cha mikutano cha Mkapa kilichopo jijini
Mbeya.
Watoa huduma wa mradi wa KFW kutoka wilalaya za Ileje,Momba,Mbozi,Chunya na Mbeya jiji wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmiMeneja wa miradi inayofadhiliwa na wafadhili wa NHIF Daud Bunyinyiga akisoma risala ambapo moja kati aliyozungumza na pamoja na mafanikio makubwa ya mradi wa KFW ambapo uandikishaji wa wajawazito umevuka malengo kwa asilimia216.
Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa MbeyaPriscar Butuyuyu akizungumza jambo kwenye ufunguzi wa semina hiyo ya mafunzo.
AfisaMawasiliano wa NHIF Luhende Andrew Singu akitoa ufafanuzi zaidi juu ya namna mafunzo yatakavyoendeshwa
Mmoja wa washiri wa semina kutoka wilayani Momba Alisi Msukwa akiwawakilisha washiriki wenzake kutoa neno la shukrani ambapo aliahidi maagizo yaliyotolewa na kaimu katibu tawala watakwenda kuyafanyia kazi kwa ustawi wa jamii wanayoihudumia
Mgeni rasmi akiagana na baadhi ya maafisa wa NHIF ngazi ya taifa na Mkoa kabla ya kuondoka baada ya kufungua semina hiyo.
HABARI KAMILI
HABARI KAMILI
MFUKO wa taifa wa Bima ya Afya(NHIF) umefanikiwa
kuvuka malengo ya kuandikisha akina mama wajawazito kupitia mradi wa afya ya
mama na mtoto wa KFW kwa asilimia 216.
Lengo la awali la NHIF ilikuwa kuandikisha
wajawazito 80,000 katika kipindi cha miaka mitatu ya mradi lakini hadi sasa
wajawazito walioandikishwa ni 152,287.
Meneja wa miradi inayofadhiliwa na wafadhili Daud
Bunyinyiga amebainisha hayo leo(Oktoba 6) kwenye ufunguzi wa semina ya mafunzo
ya siku tatu ya watoa huduma za mradi wa afya ya mama na mtoto(KFW)
inayofanyika jijini Mbeya.
Bunyinyiga amesema mafaniko hayo yamepatikana
kutokana na ushirikiano mzuri baina ya wafadhili yaani benki ya Maendeleo ya
watu wa Ujerumani,NHIF pamoja na watoa huduma kupitia KFW.
Akifungua mafunzo hayo,Kaimu katibu tawala mkoa wa
Mbeya Costantine Mushi amewataka wasimamizi wa miradi ya KFW na mfuko wa afya
ya jamii(CHF) kuwa wawazi katika utendaji kazi iwao ikiwa ni sambamba na kuweka
bayana taarifa za mapato na matumizi ya fedha wanazokusanya.
Mushi amesema kwa kuweka wazi taarifa itaongeza
hamasa kwa jamii kuzidi kujiunga na huduma hizo na kunufaika kwa kupata tiba
stahili hivyo kuwezesha kuwa na jamii yenye afya njema.
No comments:
Post a Comment