Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, October 5, 2014

CBE YAZINDUA JUMUIYA YA WANAFUNZI WALIOSOMA KATIKA CHUO HICHO




Mkuu wa mkoa wa Mbeya  mstaafu John Mwakipesile(Katikati) akiwa na viongozi wa wanajumuiya ya CBE kanda ya nyanda za juu kusini baada ya kuzinduliwa kwa jumuiya hiyo.

 Mwakipesile akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua rasmi jumuiya ya wana CBE knada ya nyanda za juu kusini.

Mkuu wa vyuo vya CBE Prof.Emannuel Mjema akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo.



Msimamizi wa Taaluma kutoka CBE tawi la Mbeya Ezekiel Kayombo akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.

                            HABARI KAMILI
MKUU wa mkoa wa Mbeya Mstaafu John Mwakipesile amezindua umoja wa wahitimu wa Chuo cha biashara(CBE) waishio katika mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini.

Mwakipesile amezindua umoja huo jana katika hafla fupi iliyowakutanisha wanajamii waliosoma CBE katika kipindi cha kuanzia mwaka 1965 hadi 2014 iliyofanyika Mbeya Hotel jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho.

Akizindua umoja huo,mwakipesile ambaye ni mmoja kati ya watu waliowahi kusoma katika chuo cha CBE na baadaye kuwa mwalimu wa chuo hicho aliitaka jamii kutambua mncango mkubwa wa kitaaluma unaotolewa na chuo hicho.

Amesema chuo hicho kimekuwa na mchango mkubwa ndani na nje ya Tanzania kwa kuwezesha kupatikana kwa wanataalamu ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika suala zima la kuleta maendeleo.

Amewataja baadhi ya wana jamii waliosoma CBE na baadaye kuwa mfano mzuri wa kuigwa kuwa ni pamoja na Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Omar Kingi na  Katibu Mtendaji jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika(SADC) Dkt Stagomena Tax.

Wengine ni aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) Harry Katillya,kamanda wa polisi mkoani Tabora Suzan Kaganda, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la serikali la hifadhi ya jamii(NSSF) Dkt Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiasha,wakulima na wenye viwanda(TCCIA) kanda ya nyanda za juu kusini Gracian Kanzugala.

Awali mkuu wa vyuo vya(CBE) Profesa Emmanuel Mjema alisema wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha CBE wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwani wanaweza kukitangaza vyema chuo hicho kutokana na kuwa na ufahamu nacho zaidi.

Habari na Benny Benjamini wa Lyamba Lya Mfipa

No comments:

Post a Comment