Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, October 2, 2014

CHADEMA MBEYA WAMPIGA MKWARA RPC MSANGI



            VIONGOZI WA CHADEMA MBEYA MJINI

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kimetoa siku tatu kwa kamanda wajeshi la polisi mkoani humo kukanusha iwapo hakutoa kauli ya vitisho kwa wafuasi wa chama hicho wakati alipozungumzia kukataza maandamano yaliyokuwa yafanyike hivi karibuni

Sentensi zenye maneno “Hawa jamaa nitawafanyia kitu kibaya ambacho hawatokuja kusahau.Niko radhi hata nifukuzwe kazi” ndizo zinazolalamikiwa na viongozi wa Chadema wanaodai kamanda Msangi alizitamka alipozungumza na wanahabari.

Katika kikao chao na wanahabari,viongozi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho John Mwambigija na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi wametoa siku tatu kwa kamanda Msangi kukanusha kauli hiyo kabla hawajachukua hatua waliyoiita ni ya hatari zaidi.

Akizungumzia kauli inayolalamikiwa,kamanda msangi amekana kutamka maneno yaliyochapishwa katika baadhi ya vyombo vya habari na kubainisha kuwa kwa mtu yeyote anayeijua sheria hawezi kutoa kauli hiyo.

Aidha Kamanda huyo amesisitiza kuwa alichosema yeye ni kuwa yeyote atakayeandamana jeshi hilo litamchukulia hatua kali huku pia akisema yawezekana wapo watu ambao wanataka kulichonganisha jeshi la polisi na wanachadema kwa kuongeza chumvi katika kauli alizotoa.

No comments:

Post a Comment