Mwanzonje akipokea kadi ya CCM kutoka kwa Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga.
Hapa akielezea kinachompeleka CCM akitokea ChademaMstahiki Meya akizungumza jambo baada ya kumpokea
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mbeya
mjini kimepata pigo kubwa baada ya mmoja wa makada wake nguli kukihama chama
hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Kada Machachari aliyekihama Chadema ni Joseph
Mwanzonje aliyekuwa Mwekahazina wa chama hicho katika kata ya Iziwa iliyopo
jijini Mbeya na alikuwa pia mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ilungu uliopo katika
kata ya Iziwa.
Akizungumza kabla ya kukabidhi kadi ya Chadema na
kukabidhiwa ya CCM,Mwanzonje alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona chama
chake hakina mwenendo mzuri.
“Nimefikiri kwa kina nikaona Chadema kila
wanachokifanya wanafanya kwa kukurupuka.Hakuna mwelekeo wenye kuonesha dira ya
maendeleo ya kichama”
“Maamuzi haya sijakurupuka.Nimefikiri na
nikajiridhisha kuwa nahitaji kujiunga na chama chenye mtazamo mzuri.Sijaondoka
kwa kificho kwa baadhi ya wanachadema nimewaambia juu ya uamuzi wangu.Naamini
pia kati yao wengi watakuja CCM.” Alisema
Akimkaribisha ndani ya CCM mjumbe wa halmashauri kuu
ya CCM mkoa,na mlezi wa Chama hicho tawi la kata ya Iziwa,Mstahiki Meya wa jiji
la Mbeya Athanas Kapunga amepongeza uamuzi huo na kumtaka kuwa muadirifu ndani
ya chama hicho.
Kapunga alisema kujiunga na CCM ni hatua ya kwanza
lakini jambo la pili na lililomuhimu ni kutoa mawazo ya kimaendeleo kupitia
vikao mbalimbali vilivyowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama.
Alisema yale yote aliyokuwa akiyaona hayatekelezwi
na serikali ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi anapata kuitumia fursa
aliyoipata kuwashauri viongozi ili yatekelezwe kwa manufaa ya taifa.
Akiwa ndani ya Chadema Mwanzonje alikuwa tishio
kubwa kwa CCM kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa akionesha nyakati za kampeni za
chaguzi mbalimbali hivyo kujiunga na chama hicho ni faraja kubwa kwa wanaccm
katika kukijenga Chama chao.
No comments:
Post a Comment