Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 29, 2013

INASADIKIWA HII NI RIPOTI YA CHANZO CHA KIFO CHA MSANII MANGWAIR

Helen Joseph Hospital - Auckland Park, Johannesburg, South Africa. The Medical report from Helen Joseph hospital, Dr. Shirley Radcliffe confirming that; Albert Mangwair died from: “Alcohol toxicity” after drinking too much, Over-exhaustion and drugs overdose. The inquest heard that Albert 28, collapsed in his friend's home had been more than five-times the legal S.A drink-drive limit with 416mg of alcohol per 100 millilitres of blood in his system. Dr. Radcliffe described the reasons for ICU admission included hypoxemia and one of his friend found “two empty vodka bottles in the car” and he had been suffering from the eating disorder (Bulimia) for several months before his death and endless partying session with little or no resting. Sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he overdosed Heroin, Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in his blood, and his death was caused by massive heart attack and respiratory failure followed by sudden heart stop...and end up dead within seconds.KWA HISANI YA MITANDAO MBALIMBALI

TUJIKUMBUSHE HAYA

SIMANZI......................MSANII ALBERT MANGWAIR AFARIKI DUNIA

MSANII maarufu wa nyimbo za 'hip hop' na Bongo Fleva, Albert Mangwea maarufu kama Mangwair aka Ngwair ametangazwa kuwa amefariki dunia leo akiwa nchini Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen ya jijini Johanesburg. Kwa mujibu wa taarifa za redio mbalimbali jioni hii nchini, inadhaniwa huenda Ngwair amefariki dunia kutokana na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, taarifa kutoka kwa mmoja wa mtu wa karibu wa Ngwair nchini humo, Hussein Original aliyepo mji wa Pretoria, alisema alikutwa amefariki wakati msanii mwenzake ‘M To The P’ alikutwa amepoteza fahamu majira ya asubuhi walipokwenda kuwagongea mlango gheto kwao. Daktari tayari alishathibitisha taarifa hizo na tayari ametoa taarifa kwa watu wa karibu wa msanii huyo. Akiongea na redio ya Clouds FM, mwenyeji mwingine wa Afrika Kusini aliyejitambulisha kwa jina la Jonathan amesema usiku wa kuamkia leoMangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka: “Sijui hata huko alitumia nini,” amesema Johnson. Amesema naye asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka Ngwair hospitali kwa kuwa alikuwa bado hajaamka. Naye mwanamuziki Bushoke anayeishi jijini Pretoria amesema alikuwa akutane na Ngwair leo jijini Johannesburg lakini alishangaa kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washikaji ambao ni wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki: “Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke. Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe. Kwa mujibu wa blogu ya GSengo, wanamuziki MWANA FA na KALA PINA wamesimamisha maonesho "shows" kufuatia msiba wa Mangwair. Kimuziki, Ngwair aliibukia kwenye Dodoma ambako alikuwa katika kundi moja na Noorah na Mez B. Baadaye akapata dili Bongo Records chini ya mmiliki wa studio hizo, Petter Matthysse ‘P Funk’ aliyemuinua zaidi kimuziki na kumfanya awe miongoni mwa wanamuziki nyota nchini. Wimbo wake wa kwanza kutamba ni Gheto Langu mwaka 2003 ambao ulimpatia umaarufu kabla ya kutoa albamu yake ya kwanza a.k.a Mimi mwaka 2003 ambayo ilimpatia mafanikio makubwa na kubadili maisha yake. Hata hivyo, mafanikio hayo yalimlevya na kujitumbukiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, hivyo kujikuta akishindwa kufanya kazi ya muziki kwa usanifu na kuanza taratibu kufilisika hadi kuuza mali zake zote, ikiwemo gari aina ya Jeep. Ngwair kutoka kwenye kupanga nyumba nzima maeneo ya Sinza, Dar es Salaam akajikuta anarejea kuishi katika ‘magheto’ ya washkaji zake sehemu mbalimbali Dar es Salaam. Mwaka 2010, Athumani Tippo, mmiliki wa maduka ya Zizzou Fashions alijaribu kumuinua tena msanii huyo baada ya kumchukua kwenye lebo yake na kumuwezesha kutoa albamu ya pili, Nge. Hata hivyo, Nge haikufanya vizuri sana na kuzidi kumchanganya msanii huyo hivyo kutopea kwenye dimbwi la utumiaji wa dawa za kulevya na ‘kuharibika zaidi’. Mafanikio yake zaidi ni kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka 2003, msanii Wayne Wonder aliyekuja kutumbuiza kwenye Fiesta aliondoka na CD ya wimbo Mikasi ya Ngwair baada ya kuvutiwa na kibao hicho alichowashirikisha Mchizi Mox na Ferooz. Pumzika kwa amani. Mbele yako, nyuma yetu Ngwair. RIP. KWA HISAN YA MITANDAIO MBALIMBALI.

Tuesday, May 28, 2013

COCA COLA WAPANIA KUCHEZA LIGI KUU

Meneja wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza cha mkoani Mbeya Gary Pay akiwa amembeba mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ikiwa ni moja ya michezo iliyofanyika kwenye hafra ya kusherehekea kombe la mashindano ya kombe la Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola nchini lililofahamika kama MD Cup 2013 ambapo timu ya Coca Cola kwanza waliibuka mabingwa na kukabidhiwa kombe hilo. KIWANDA cha vinywaji baridi cha Coca Cola Kwanza cha mkoani Mbeya kimeelezea nia yake ya kuwa na timu itakayoshiriki mashindano makubwa nchini ikiwemo ligi kuu ya Tanzania bara. Meneja wa kiwanda Gary Pay alieleza nia hiyo kwa wafanyakazi wake waliohudhuria hafra ya kusherehekea kombe la mashindano ya kombe la Mkurugenzi mkuu wa Coca Cola nchini lililofahamika kama MD Cup 2013 ambapo timu ya Coca Cola kwanza waliibuka mabingwa na kukabidhiwa kombe hilo. Pay alisema kampuni ya Coca Cola kupitia kiwanda hicho iko katika mkakati wa kuhakikisha wanaismarisha timu hiyo na kuiwexzesha kushiriki mashindano makubwa. Alisema ili kutekeleza nia hiyo tayari kampuni imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Charles Makwaza atakayekuwa akiinoa kwa muda huyo na tayari wameanza mchakato wa kuisajili na kuiwezesha kushiriki michuano kwa ngazi mbalimbali ili kuanza kupanda daraja. “Sisi tunalinganisha uwepo wa timu sawa na utendajui katika kiwanda chetu.Tukiitazama safu ya ushambuliaji ni sawa na safu yetu ya mauzo,kwa upande wa safu ya ulinzi ni sawa na kitengo cha uzalishaji kiwandani.Kwa ujumla timu yote ni sawa na watumishi wote pale kiwandani.Hii ni sehemu ya mafanikio yetu kibiashara” “Tumedhamiria,tumeamua na tunaamini tutafanikiwa siku moja kuwa na timu itakayokuwa na upinzani mkubwa kwa timu nyingine nchini kwenye mashindano makubwa hususani ligi kuu” alisema. Naye kocha Makwaza alisema aliipongeza kampuni hiyo kwa kutambua uwezo wake na kumpa mkataba wa kuifundisha timu hiyo huku akiahidi kuhakikisha kikosi chake kinakuwa tishio kwa timu nyingine ili kutimiza malengo ya kuanzishwa kwa timu. Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo Bahati Jonas alisema ushirikiano wa karibu baina ya wachezaji na uongozi wa kampuni ni miongoni mwa mambo yatakayoiwezesha kufikia malengo yanayotarajiwa

Monday, May 27, 2013

HII NDIYO YANGA

WANAWAKE KULIPIWA CHF

WANAWAKE waliojiunga na umoja wa vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA), katika mji wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, wameahidiwa kulipiwa bima ya afya ya jamii (CHF) wao pamoja na familia zao. Ahadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na katibu wa umoja huo Gordon Kalulunga baada ya vijana wa mji huo kufanya usafi na uhifadhi wa mazingira katika eneo la Manyanya na njia panda sokoni. Kalulunga alisema, ili kuwapa motisha wanawake wote waliojiunga na umoja huo na kufanya usafi kwa kujitolea kuonesha uzalendo na uwajibikaji kwa taifa lao, kufikia Julai 15 mwaka huu atawalipia bima za afya. ‘’Hii ni zawadi kwa wanawake wote waliopo kwenye umoja huu, na msichana yeyote atakayeungana nasi nitamlipia pia bima ya afya ya jamii ambapo kila mmoja anatakiwa kuwa na picha moja ya kwake,mume,watoto au wategemezi’’ alisema Kalulunga huku akishukuliwa. Kalulunga ambaye ni mwandishi wa habari aliyebobea katika masuala ya afya ya uzazi, alisema kwa kutambua umuhimu wa wanawake kuwa na mahitaji ya matibabu ndiyo maana ameamua kufanya hivyo na ili kiwe kivutio pia kwa wanawake wengine na jamii nzima kwa ujumla kujumuika katika kutunza na kuhifadhi mazingira Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo wa vijana wazalendo Mbalizi, Bahati Mwaipopo, alisema ni jukumu la jamii kufanya usafi na kuhifadhi mazingira bila shuruti kwa manufaa y afya za viumbe hai wakiwemo binadamu.

Saturday, May 25, 2013

UMISSETA MBEYA YAMALIZIKA

MASHINDANO ya umiseta kwa shulea za sekondari(Umisseta) mkoa wa Mbeya yamemalizika na kupatikana wanafunzi 135 ambao watachujwa na kubakia 125 watakaounda timu ya mkoa kushiriki hatua ya kanda. Akitangaza matokeo ya mashindano hayo,afisa michezo mkoani hapa George Mbijima alisema katika mchezo wa mpira wa mkono(Handba ll) mshindi kwa wasichana ilikuwa halmashauri ya wilaya ya Mbozi na wavulana halmashauri ya jiji la Mbeya. Voleyball wasichana ilishinda halmashauri ya wilaya ya Mbeya na wavulana ikaibuka halmashauri mpya ya Busokelo huku mchezo wa Netiball wilaya ya Kyela wakiibuka mabingwa. Mchezo wa kikapu Rungwe alichukua kombe la ubingwa kwawasichana na wavulana jiji la Mbeya likaibuka kinara huku riadha Rungwe wakionesha kuwa mabingwa wa kukimbiza upepo. Mchezo wa fainali wa mpira wa miguu wavulana ulimalizika kwa vijana wa jiji kuwanyuka goli 2-1 wenzao wa Mbozi huku halmashauri ya wilaya ya Rungwe ikijilaumu yenyewe kwa kuchezesha mamluki hali iliyosababisha kunyang’anywa pointi sita ilizokuwa imepata kwenye michezo miwili ya awali. Hata hivyo wasichana wa halmashauri hiyo wakapunguza majonzi kwa kuibuka mabingwa kwenye mchezo wa soka pamoja na mpira wa meza ambao kwa wavulana mabingwa ni halmashauri ya jiji. Akifunga mashindano hayo afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda aliwataka waratibu kuhakikisha wanatafuta vikombe vyenye hadhi kwa washindi wa mwakani tofauti na vile vilivyotolewa mwaka huu. Kaponda alisema vikombe vya sasa havina hadhi ya mashindano ya sekondari kwani vinazidiwa hata na vile vya mashindano ya shule za msingi(Umitashumita) alivyosema ni vizuri na vina heshima ya mabingwa. Afisa elimu huyo aliagiza pia wakuu wa shule kutowaruhusu wanafunzi walio kidato cha nne la sita kushiriki mashindano hayo kwakuwa muda huo wanapaswa kujiandaa na mitihani sawa na ilivyo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa mashindano ya shule za msingi

Friday, May 24, 2013

BURUDANI MURUA

MASIKHARA HAYOOOOOOOOOOO

Njia za kujua kama simu.ni ya mchina ni hizi hapa: 1. Betri inajaa baada ya dakika tatu, 2. Ina TV, tochi, mswaki, kiberiti cha sigara, 3. Ndege ikipita, simu inaandika 1 MISSED CALL 4. Ukiwa karibu na jiko, inaandika CHARGER CONNECTED na 5. Ukipita karibu na mchina, inaonyesha NEW DEVICE FOUND....!

Thursday, May 23, 2013

UMISSETA MBEYA YAFUNGULIWA KWA MAJONZI MAKUBWA

Baadhi ya wanafunzi washiriki wa mashindano ya wanafunzi wa shule za sekondari(UMISETA) mkoani Mbeya yanayoendelea katika viwanja vya Sekondari ya Iyunga pamoja na Viongozi wakifuatilia hotuba ya afisa elimu mkoani hapo Mwalimu Juma Kaponda kabla ya kufungua mashindano hayo leo. MASHINDANO ya wanafunzi wa shule za sekondari(UMISETA) mkoani Mbeya yamefunguliwa kwa simanzi kubwa baada ya mmoja wa waratibu wa mashindano hayo kupoteza maisha katika ajali. Aliyepoteza maisha usiku wa kuamkia leo ikiwa ni siku moja baada ya kuanza kwa mashindano hayo ni mwalimu Abdalah Chalo(41) wa shule ya sekondari Iyunga ya jijini hapa aliyegongwa na lori wakati akiendesha pikipiki alipokuwa akirudi nyumbani kwake muda mfupi baada ya kukamilisha zoezi la kugawa chakula kwa washiriki wa michezo. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman mwalimu Chalo aliyekuwa akiendesha pikipiki yenye namba T 815 BKQ aina ya King Fan alikutwa na mauti baada ya kugongwa na lori lenye namba T 441 BYW aina ya Scania likiwa na tela lenye namba T 496 BWD. Kamanda Athuman amesema tukio hilo lilitokea Mei 22 majira ya saa 3:00 ya usiku katika eneo la Iyunga darajani jirani na nyumbani kwa marehemu na kumtaja dereva wa lori kuwa ni Heri Faustin(35) mkazi wa eneo la Mama John jijini Mbeya. Akifungua mashindano ya Umiseta alhamisi hii katika viwanja vya shule ya sekondari Iyunga,afisa elimu mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amemtaja marehemu kuwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika ufundishaji wa somo la hisabati shuleni hapo na pia usimamizi wa shughuli za michezo. Naye afisa michezo mkoani hapa George Mbijima amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwalimu Chalo kwakuwa kilitokea ikiwa ni muda mfupi umepita tangu walipokuwa katika kikao cha pamoja kabla hajawaacha na kwenda kushughulikia shughuli ya ugawaji chakula kwa washiriki wa mashindano na kisha kuanza safari kurudi nyumbani kwake. Mashindano ya Umiseta kwa mkoa wa Mbeya mwaka huu yanashirikisha jumla ya wanafunzi 1 kutoka halmashauri 1066 za mkoani hapa lengo likiwa ni kupata wanafunzi 125 watakaounda timu ya mkoa kwaajili ya kushiriki mashindano hayo katika ngazi ya kanda.

Wednesday, May 22, 2013

HATARIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Wakazi jijini Mbeya wakiendelea na mizunguko katika eneo la uhindini jirani na ofisi za mamlaka ya mapato(TRA) na benki za NMB tawi la Loleza na benki ya Stanbic.Eneo hili limekuwa hatari kwa wapita njia kutokana na sehemu wanazopaswa kuzitumia kutumika kwa uegeshaji holela wa magari pamoja na upangaji holela wa bidhaa za wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga

HATARIIIIIIIIIIIIIIIIII

UONGOZI wa mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga jijini Mbeya umelazimika kuiondoka katika umoja wa ubalozi familia moja kutokana na wazazi wa familia hiyo kumfanyia mmoja wa watoto wao ukatili usio vumilika. Ukatili wanaoufanya baba wa familia Joseph Simon na mama wa kufikia Sekera Witson kwa mtoto Joshua Joseph(3) ni pamoja na kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka miwili pasipo kuruhusiwa kutoka nje huku akiwa hapewi chakula kama wanavyopewa wenzake walio watoto wa halisi wa Sekera. Inaelezwa kuwa manyanyaso kwa mtoto huyo yalianza tangu akiwa mchanga alipoachwa na mama yake mzazi aliyekimbia kipigo kutoka kwa mumewe na ndipo akawa chini ya uangalizi wa mama huyo wa katili. Eneo linalotajwa kuwa ni ndilo amekuwa akilala pamoja kucheza yanatia simanzi kuonesha dhahiri kuwa ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kudhoofu kwa afya ya mtoto Joshua na kumfanya asitembee mpaka leo. Baadhi ya wanahabari na maafisa maendeleo ya jamii kata za Igawilo na Iyunga walijionea maisha halisi ya mtoto huyo juzi walipotembelea familia hiyo baada ya kupewa taarifa na baadhi ya majirani. Balozi wa mtaa wa Ikuti Aloni Mboya alisema mtoto huyo alianza kufanyiwa ukatili huo karibia miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi mbalimbali ikiwemo utapiamlo. Mboya alisema mnamo Machi 2011 alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo na ndipo uongozi wa mtaa ukalazimika kumwita baba wa mtoto na alipohojiwa juu ya malezi ya mwanaye akakiri kosa na ndipo akaagiwazwa kumtunza vema mtoto huyo kwa kumpa chakula na huduma nyingine muhimu. Hata hivyo alisema pamoja na kalipio hilo hakuna mabadiliko yaliyojitokeza hali iliyolazima uongozi wa mtaa kuwaita tena wazazi wote na kuwapa miezi sita wawe wamehama mtaani hapo kwakuwa kitu walichokuwa wakikifanya ni aibu ikwa wakazi wa mtaa huo.

Wednesday, May 15, 2013

WANAFUNZI WACHOMA MOTO BWENI

WANAFUNZI 15 wa shule ya sekondari ya wazazi ya Lupata iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Wanafunzi hao wamechoma bweni hilo jana(mei 14) majira ya saa 2:00 usiku huku chanzo kikitajwa kuwa na baadhi ya wanafunzi kutoridhishwa na uongozi wa shule kuwasimamisha masomo wenzao watatu kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman amewataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kuwa ni Joseph Robert(18) mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo na mkazi wa Kitunda Dar es salaam. Wengine ni Mwita Chacha(17) wa kidato cha tatu na mkazi wa Kitunda pia na Daniel David(18) wea kidato cha tatu na mkazi wa Ipinda wilayani Kyela. Kamanda Athuman amesema kabla ya tukio wanafunzi hao watatu waliwahamasisha wanafunzi wengine kuwaunga mkono kwa kufanya vurugu kupinga adhabu waliyopewa. Hata hivyo wanafunzi 50 waliokuwa kwenye bweni moja walionekana kutounga mkono wenzao kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na ndipo baadhi ya wanafunzi walikasirika na kuamua kulichoma moto bweni hilo.

WALIOKUFA KWENYE AJARI YA GARI JANA MBEYA HAWA HAPA

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman waliokuwa kwenye ajali ya gari jana eneo la Mwansekwa ni Filimon Mgumbe(30) mkulima na mkazi wa Itigi na Baraka Mwasota(24) mkazi wa Mwansekwa. Amesema mtu wa tatu ambaye ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25-30 hakufahamika jina wala makazi yake na kuwataka wananchi kufika katika hospitali ya rufaa kuutambua mwili wake. Amewataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na wawili ambao walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kuondoka ambao maji yao hayakutambuliwa lakini wawili bado wamelazwa katika hospitali ya rufaa. Wanaoendelea kupata matibabu ni pamoja na raia wa China Don Fung Cheng(38) na mwanaume mmoja ambaye hajatambulika jina wala makazi yake kwakuwa hawezi kuzumngumza.

Tuesday, May 14, 2013

WATU WANNE WANAOFIWA KUFA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA MUDA MFUPI ULIOPITA NJE KIDOGO YA JIJI LA MBEYA BAADA YA LORI LA KAMPUNI YA WACHINA LILILOKUWA LIMEBEBA KIFUSI NA JUU YAKE VIBARUA KUPINDUKA..........Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi.
JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMMED CHANDE ATHUMAN HIVI SASA ANAZUNGUMZA NA WATUMISHI WA IDARA YA MAHAKAMA KATIKA UKUMBI WA MAHAKAMA KUU ILIYOPO JIJINI MBEYA.SEHEMU YA MAZUNGUMZO HAYO NI PAMOJA NA CHANGAMOTO ZA IDARA HIYO.

Sunday, May 12, 2013

WADAU MBEYA CITY WALALAMIKIA UHAMISHO WA MKURUGENZI WA JIJI

WADAU wa soka mkoani Mbeya wameonesha hali ya wasiwasi wa timu yao kipenzi ya Mbeya City kuendelea vyema na maandalizi ya ligi kuu bara msimu ujao kufuatia kuhamishwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji Juma Idd. Kwa nyakati na maeneo tofauti wadau hao wameelezea wasiwasi wao wakisema huenda mkurugenzi mpya asiwe na hamasa ya michezo hivyo anaweza kuvunja mikakati iliyokuwa imeandaliwa kuiwezesha timu hiyo kuanza vyema michuano ya lihi kuu baada ya kupanda msimu huu. Miongoni waliozungumzia hayo ni pamoja na katibu wa chama cha Makocha(Tafca) mkoa wa Mbeya Thomas Kasombwe aliyesema wadau wa soka watahuzunishwa iwapo mkurugenzi mpya hatokipa kipaumbele timu hiyo inayomilikiwa na halmashauri ya jiji. Kasombwe alisema “Ni uhamisho ambao kimsingi sisi kama wadau umetuhuzunisha.Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa na hamasa kubwa sana ya michezo hata tukafanikiwa kununua timu na kuipandisha hadi ligi kuu.Sasa ameondoka na hatujui ajaye ana mapenzi na michezo ama la” alisema. Kutokana na hali hiyo Kasombwe alisema ipo haja ya uongozi wa timu hiyo kuanzisha mfumo wa uuzaji hisa kwa wanachama ili uongozi wa juu wa halmashauri unapobadilishwa isiweze kutetereka. Naye mmoja wa makocha mkoani hapa Amos Chuma alisema uzoefu unaonyesha timu nyingi zimekuwa zikishindwa kuendeleza uimara wake kutokana na mabadiliko ya uongozi hususani pale kiongozi mpya anayeletwa anapokosa ari ya michezo.

Saturday, May 11, 2013

MUST MABINGWA BONANZA LA WANAVYUO MBEYA

TIMU ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) iliibuka bingwa wa mchezo huo kwenye bonanza la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lililofanyika mwishoni mwa wiki yakidhaminiwa na Mfuko wa Penseni kwa watumishi wa umma(PSPF). Must ilinyakua ubingwa huo na kuzawadiwa kombe baada ya kuinyuka goli 2-0 timu ya soka ya chuo cha kilimo Uyole cha jijini hapa kwenye mchezo wa fainali. Timu nyingine zilizoshiriki bonanza hilo ni kutoka vyuo vya Mzumbe tawi la Mbeya,Chuo cha madaktari cha hospitali ya rufaa Mbeya,Chuo cha Mafunzo na ufundi stadi(VETA),Chuo cha ualimu cha Lutherani Mbeya na Taasisi ya hesabu(TIA). Kwa upande wa michezo mingine,TIA waliibuka bingwa wa mpira wa pete kwa kuinyuka goli 45 kwa 20 Ualimu Lutherani katika mchezo wa fainali. Mchezo wa Kikapu bingwa aliibuka Must aliyeinyuka TIA vikapu 59 kwa 45 huku mchezo wa wavu TIA ikiibuka bingwa kwa kuichakaza Mzumbe seti 3-1. Afisa mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mbeya Said Kipindura alisema mfuko huo unatambua umuhimu wa michezo hususani inayowakutanisha vijana kama wanafunzi waliopo katika vyuo vya elimu ya juu kama vilivyoshiriki. Kipindura alitoa ahadi ya PSPF kuendelea kudhamini mashindano mbalimbali yanayolenga pia kuibua na kukuza vipaji akisema ni njia pia wa kuzifanya huduma zake kufahamika kwa jamii. “Sisi PSPF umuhimu wa michezo.Tumeona leo wanafunzi wa vyuo hivi mmeweza kukutana na kufurahi kwa pamoja.Hii inasaidia pia jamii yetu kuendeleza uzalenzo wa kusisitiza amani na mshikamano tulioachiwa na waasisi wa taifa letu” alisema. Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha TIA lilikamilishwa kwa burudani ya muziki na mashindani ya mitindo katika viwanja vya baa ya New Mbeya City Pub ya Mwanjelwa.

WANAHABARI WANAPOGEUKA WATOA BURUDANI

NI KATIKA BONANZA LILILOANDALIWA NA KAMPUNI YA BIA YA TBL TAWI LA MBEYA LILILOFANYIKA KWENYE UWANJA WA CHUO CHA UHASIBU(TIA) AMBAPO WANAHABARI WALIKUWA MIONGONI MWA WASHIRIKI

CHUNYA WAPONGEZWA KUNUNUA MAABARA ZINAZOTEMBEA

IDARA ya elimu katika halmashauri ya wilaya ya Chunya imepongezwa kwa kuanza kutekeleza mradi wa ununuzi wa maabara za kuhamishika kwaajili ya shule za sekondari wilayani hapa. Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya madiwani kwenye kikao cha kawaida cha robo ya tatu ya mwaka cha balaza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Chunya. Madiwani hao wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa maabara hizo zitakazowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo badala ya nadharia. Mmoja wa madiwani hao Fraterin Shirima alisema hatua ya kununua maabara hizo ni mwanzo mzuri unaoleta imani ya wanafunzi wa shule husika kuanza kufanya vizuri kwenye mitihani yao hususani ya masomo ya sayansi. Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya Elimu,Afya na Maji halmashauri hiyo imenunua maabara nne zinazotembea kwa gharama ya jumla ya shilingi milioni 24. Taarifa hiyo iliyotolewa kwenye kikao hicho imefafanua kuwa shule zilizokabidhiwa maabara hizo ni sekondari za Kiwanja,Lupa,Kapelele na Mwagala.

Tuesday, May 7, 2013

BONANZA NA SHOW YA BURUDANI YA VYUO VIKUU MBEYA ILIVYOKOLEA

TIMU ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) iliibuka bingwa wa mchezo huo kwenye bonanza la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lililofanyika mwishoni mwa wiki yakidhaminiwa na Mfuko wa Penseni kwa watumishi wa umma(PSPF). Must ilinyakua ubingwa huo na kuzawadiwa kombe baada ya kuinyuka goli 2-0 timu ya soka ya chuo cha kilimo Uyole cha jijini hapa kwenye mchezo wa fainali. Timu nyingine zilizoshiriki bonanza hilo ni kutoka vyuo vya Mzumbe tawi la Mbeya,Chuo cha madaktari cha hospitali ya rufaa Mbeya,Chuo cha Mafunzo na ufundi stadi(VETA),Chuo cha ualimu cha Lutherani Mbeya na Taasisi ya hesabu(TIA). Kwa upande wa michezo mingine,TIA waliibuka bingwa wa mpira wa pete kwa kuinyuka goli 45 kwa 20 Ualimu Lutherani katika mchezo wa fainali. Mchezo wa Kikapu bingwa aliibuka Must aliyeinyuka TIA vikapu 59 kwa 45 huku mchezo wa wavu TIA ikiibuka bingwa kwa kuichakaza Mzumbe seti 3-1. Afisa mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mbeya Said Kipindura alisema mfuko huo unatambua umuhimu wa michezo hususani inayowakutanisha vijana kama wanafunzi waliopo katika vyuo vya elimu ya juu kama vilivyoshiriki. Kipindura alitoa ahadi ya PSPF kuendelea kudhamini mashindano mbalimbali yanayolenga pia kuibua na kukuza vipaji akisema ni njia pia wa kuzifanya huduma zake kufahamika kwa jamii. “Sisi PSPF umuhimu wa michezo.Tumeona leo wanafunzi wa vyuo hivi mmeweza kukutana na kufurahi kwa pamoja.Hii inasaidia pia jamii yetu kuendeleza uzalenzo wa kusisitiza amani na mshikamano tulioachiwa na waasisi wa taifa letu” alisema. Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha TIA lilikamilishwa kwa burudani ya muziki na mashindani ya mitindo katika viwanja vya baa ya New Mbeya City Pub ya Mwanjelwa.

Saturday, May 4, 2013

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA(MBPC) KIMEWATIMUA UANACHAMA WANACHAMA WAKE WAWILI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA CHAMA HICHO WALIPOKUWA MADARAKANI.UAMUZI WA KUWAFUTA UANACHAMA WANACHAMA HAO UNATOKANA NA MAAMUZI YALIYOPIGWA KWA KURA ZA WANACHAMA JUU YA NINI KIFANYIKE DHIDI YAO

Friday, May 3, 2013

JAMBAZI WATANO WAUAWA

MAJAMBAZI watano wameuawa kwa kupigwa risasi katika majibizano ya risasi kati yao na polisi mkoani Mbeya. Kuuawa kwa majambazi hao wasiofahamika majina wala makazi yao kunatokana na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi na kuanza kuzifanyi kazi tangu asubuhi ya leo Mei 3). Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi hilo lilikuwa na wakati mgumu kufuatilia taariza za waharifu hao kwakuwa haikujulikana walikuwa wapi. Kamanda Athuman amesema hatimaye mnamo majira ya saa sita mchana askari waliokuwa katika eneo la Garijembe barabara ya Mbeya/Tukuyu walisimamisha gari yenye namba T 911 BUG aina ya Toyota Spacio kwa lengo la kuikagua na ndipo ghafla walishuka watu watano wawili kati yao wakiwa na bunduki na kuanza kufyatua hovyo risasi. Amesema hali hiyo ilisababisha askari waliokuwa eneo hilo kuanza kujibu mashambulizi na ndipo walipofanikiwa kuwajeruhi majambazi hao na walipowafikisha hospitali ya rufaa wakawa wamefariki dunia. Ametaja vitu vilivyokamatwa kuwa ni pamoja na gari waliyokuwa nayo jambazi,bunduki mbili moja ya kivita aina ya Sub Machine Gun(SMG) iliyokuwa na risasi 16 zilizokuwa zimesalia na nyingine aina ya Mark III ikiwa na risasi mbili zilizosalia. Ndani ya gari hiyo pia ilikutwa kama moja ngumu ambayo haikufahamika ilikuwa kwaajili ya shughuli ipi. Amewataka wananchi mkoani hapa kufika katika hospitali ya rufaa kuweza kutambua miili ya jambazo hao waliokufa kutokana na kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya miili yao kwa risasi.