Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 22, 2013

HATARIIIIIIIIIIIIIIIIII

UONGOZI wa mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga jijini Mbeya umelazimika kuiondoka katika umoja wa ubalozi familia moja kutokana na wazazi wa familia hiyo kumfanyia mmoja wa watoto wao ukatili usio vumilika. Ukatili wanaoufanya baba wa familia Joseph Simon na mama wa kufikia Sekera Witson kwa mtoto Joshua Joseph(3) ni pamoja na kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka miwili pasipo kuruhusiwa kutoka nje huku akiwa hapewi chakula kama wanavyopewa wenzake walio watoto wa halisi wa Sekera. Inaelezwa kuwa manyanyaso kwa mtoto huyo yalianza tangu akiwa mchanga alipoachwa na mama yake mzazi aliyekimbia kipigo kutoka kwa mumewe na ndipo akawa chini ya uangalizi wa mama huyo wa katili. Eneo linalotajwa kuwa ni ndilo amekuwa akilala pamoja kucheza yanatia simanzi kuonesha dhahiri kuwa ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kudhoofu kwa afya ya mtoto Joshua na kumfanya asitembee mpaka leo. Baadhi ya wanahabari na maafisa maendeleo ya jamii kata za Igawilo na Iyunga walijionea maisha halisi ya mtoto huyo juzi walipotembelea familia hiyo baada ya kupewa taarifa na baadhi ya majirani. Balozi wa mtaa wa Ikuti Aloni Mboya alisema mtoto huyo alianza kufanyiwa ukatili huo karibia miaka mitatu sasa hali ambayo imepelekea mtoto huyo kukumbwa na maradhi mbalimbali ikiwemo utapiamlo. Mboya alisema mnamo Machi 2011 alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo na ndipo uongozi wa mtaa ukalazimika kumwita baba wa mtoto na alipohojiwa juu ya malezi ya mwanaye akakiri kosa na ndipo akaagiwazwa kumtunza vema mtoto huyo kwa kumpa chakula na huduma nyingine muhimu. Hata hivyo alisema pamoja na kalipio hilo hakuna mabadiliko yaliyojitokeza hali iliyolazima uongozi wa mtaa kuwaita tena wazazi wote na kuwapa miezi sita wawe wamehama mtaani hapo kwakuwa kitu walichokuwa wakikifanya ni aibu ikwa wakazi wa mtaa huo.

No comments:

Post a Comment