Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, May 11, 2013

CHUNYA WAPONGEZWA KUNUNUA MAABARA ZINAZOTEMBEA

IDARA ya elimu katika halmashauri ya wilaya ya Chunya imepongezwa kwa kuanza kutekeleza mradi wa ununuzi wa maabara za kuhamishika kwaajili ya shule za sekondari wilayani hapa. Pongezi hizo zimetolewa na baadhi ya madiwani kwenye kikao cha kawaida cha robo ya tatu ya mwaka cha balaza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Chunya. Madiwani hao wamesema kuna umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa maabara hizo zitakazowawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo badala ya nadharia. Mmoja wa madiwani hao Fraterin Shirima alisema hatua ya kununua maabara hizo ni mwanzo mzuri unaoleta imani ya wanafunzi wa shule husika kuanza kufanya vizuri kwenye mitihani yao hususani ya masomo ya sayansi. Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya Elimu,Afya na Maji halmashauri hiyo imenunua maabara nne zinazotembea kwa gharama ya jumla ya shilingi milioni 24. Taarifa hiyo iliyotolewa kwenye kikao hicho imefafanua kuwa shule zilizokabidhiwa maabara hizo ni sekondari za Kiwanja,Lupa,Kapelele na Mwagala.

No comments:

Post a Comment