Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, May 15, 2013

WANAFUNZI WACHOMA MOTO BWENI

WANAFUNZI 15 wa shule ya sekondari ya wazazi ya Lupata iliyopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi kwa kuchoma moto bweni moja la wanafunzi wa kiume. Wanafunzi hao wamechoma bweni hilo jana(mei 14) majira ya saa 2:00 usiku huku chanzo kikitajwa kuwa na baadhi ya wanafunzi kutoridhishwa na uongozi wa shule kuwasimamisha masomo wenzao watatu kwa makosa ya utovu wa nidhamu. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwan Athuman amewataja wanafunzi waliosimamishwa masomo kuwa ni Joseph Robert(18) mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo na mkazi wa Kitunda Dar es salaam. Wengine ni Mwita Chacha(17) wa kidato cha tatu na mkazi wa Kitunda pia na Daniel David(18) wea kidato cha tatu na mkazi wa Ipinda wilayani Kyela. Kamanda Athuman amesema kabla ya tukio wanafunzi hao watatu waliwahamasisha wanafunzi wengine kuwaunga mkono kwa kufanya vurugu kupinga adhabu waliyopewa. Hata hivyo wanafunzi 50 waliokuwa kwenye bweni moja walionekana kutounga mkono wenzao kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na ndipo baadhi ya wanafunzi walikasirika na kuamua kulichoma moto bweni hilo.

No comments:

Post a Comment