Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, May 11, 2013

MUST MABINGWA BONANZA LA WANAVYUO MBEYA

TIMU ya mpira wa miguu ya chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) iliibuka bingwa wa mchezo huo kwenye bonanza la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu lililofanyika mwishoni mwa wiki yakidhaminiwa na Mfuko wa Penseni kwa watumishi wa umma(PSPF). Must ilinyakua ubingwa huo na kuzawadiwa kombe baada ya kuinyuka goli 2-0 timu ya soka ya chuo cha kilimo Uyole cha jijini hapa kwenye mchezo wa fainali. Timu nyingine zilizoshiriki bonanza hilo ni kutoka vyuo vya Mzumbe tawi la Mbeya,Chuo cha madaktari cha hospitali ya rufaa Mbeya,Chuo cha Mafunzo na ufundi stadi(VETA),Chuo cha ualimu cha Lutherani Mbeya na Taasisi ya hesabu(TIA). Kwa upande wa michezo mingine,TIA waliibuka bingwa wa mpira wa pete kwa kuinyuka goli 45 kwa 20 Ualimu Lutherani katika mchezo wa fainali. Mchezo wa Kikapu bingwa aliibuka Must aliyeinyuka TIA vikapu 59 kwa 45 huku mchezo wa wavu TIA ikiibuka bingwa kwa kuichakaza Mzumbe seti 3-1. Afisa mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mbeya Said Kipindura alisema mfuko huo unatambua umuhimu wa michezo hususani inayowakutanisha vijana kama wanafunzi waliopo katika vyuo vya elimu ya juu kama vilivyoshiriki. Kipindura alitoa ahadi ya PSPF kuendelea kudhamini mashindano mbalimbali yanayolenga pia kuibua na kukuza vipaji akisema ni njia pia wa kuzifanya huduma zake kufahamika kwa jamii. “Sisi PSPF umuhimu wa michezo.Tumeona leo wanafunzi wa vyuo hivi mmeweza kukutana na kufurahi kwa pamoja.Hii inasaidia pia jamii yetu kuendeleza uzalenzo wa kusisitiza amani na mshikamano tulioachiwa na waasisi wa taifa letu” alisema. Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya chuo cha TIA lilikamilishwa kwa burudani ya muziki na mashindani ya mitindo katika viwanja vya baa ya New Mbeya City Pub ya Mwanjelwa.

No comments:

Post a Comment