Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, May 12, 2013

WADAU MBEYA CITY WALALAMIKIA UHAMISHO WA MKURUGENZI WA JIJI

WADAU wa soka mkoani Mbeya wameonesha hali ya wasiwasi wa timu yao kipenzi ya Mbeya City kuendelea vyema na maandalizi ya ligi kuu bara msimu ujao kufuatia kuhamishwa kwa mkurugenzi wa halmashauri ya jiji Juma Idd. Kwa nyakati na maeneo tofauti wadau hao wameelezea wasiwasi wao wakisema huenda mkurugenzi mpya asiwe na hamasa ya michezo hivyo anaweza kuvunja mikakati iliyokuwa imeandaliwa kuiwezesha timu hiyo kuanza vyema michuano ya lihi kuu baada ya kupanda msimu huu. Miongoni waliozungumzia hayo ni pamoja na katibu wa chama cha Makocha(Tafca) mkoa wa Mbeya Thomas Kasombwe aliyesema wadau wa soka watahuzunishwa iwapo mkurugenzi mpya hatokipa kipaumbele timu hiyo inayomilikiwa na halmashauri ya jiji. Kasombwe alisema “Ni uhamisho ambao kimsingi sisi kama wadau umetuhuzunisha.Mkurugenzi aliyekuwepo alikuwa na hamasa kubwa sana ya michezo hata tukafanikiwa kununua timu na kuipandisha hadi ligi kuu.Sasa ameondoka na hatujui ajaye ana mapenzi na michezo ama la” alisema. Kutokana na hali hiyo Kasombwe alisema ipo haja ya uongozi wa timu hiyo kuanzisha mfumo wa uuzaji hisa kwa wanachama ili uongozi wa juu wa halmashauri unapobadilishwa isiweze kutetereka. Naye mmoja wa makocha mkoani hapa Amos Chuma alisema uzoefu unaonyesha timu nyingi zimekuwa zikishindwa kuendeleza uimara wake kutokana na mabadiliko ya uongozi hususani pale kiongozi mpya anayeletwa anapokosa ari ya michezo.

No comments:

Post a Comment