Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, May 27, 2013

WANAWAKE KULIPIWA CHF

WANAWAKE waliojiunga na umoja wa vijana wazalendo Mbalizi(UVIWAMBA), katika mji wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, wameahidiwa kulipiwa bima ya afya ya jamii (CHF) wao pamoja na familia zao. Ahadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na katibu wa umoja huo Gordon Kalulunga baada ya vijana wa mji huo kufanya usafi na uhifadhi wa mazingira katika eneo la Manyanya na njia panda sokoni. Kalulunga alisema, ili kuwapa motisha wanawake wote waliojiunga na umoja huo na kufanya usafi kwa kujitolea kuonesha uzalendo na uwajibikaji kwa taifa lao, kufikia Julai 15 mwaka huu atawalipia bima za afya. ‘’Hii ni zawadi kwa wanawake wote waliopo kwenye umoja huu, na msichana yeyote atakayeungana nasi nitamlipia pia bima ya afya ya jamii ambapo kila mmoja anatakiwa kuwa na picha moja ya kwake,mume,watoto au wategemezi’’ alisema Kalulunga huku akishukuliwa. Kalulunga ambaye ni mwandishi wa habari aliyebobea katika masuala ya afya ya uzazi, alisema kwa kutambua umuhimu wa wanawake kuwa na mahitaji ya matibabu ndiyo maana ameamua kufanya hivyo na ili kiwe kivutio pia kwa wanawake wengine na jamii nzima kwa ujumla kujumuika katika kutunza na kuhifadhi mazingira Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo wa vijana wazalendo Mbalizi, Bahati Mwaipopo, alisema ni jukumu la jamii kufanya usafi na kuhifadhi mazingira bila shuruti kwa manufaa y afya za viumbe hai wakiwemo binadamu.

No comments:

Post a Comment