Maneno yaliyowekwa katika ukurasa wa FB wa Yanga yanaeleza hiviiiii......
”Nimeomba
kuuzwa na tayari barua ipo mezani kwenye ofisi ya Yanga na nimewatajia
mahali ninapopenda kuuzwa, nimeomba kuuzwa ili wasiingie hasara
kwasababu walininunua kwa pesa nyingi. Sababu kubwa ya maamuzi Yangu
haya ni nafasi finyu ya kucheza niliyonayo katika kikosi cha Yanga
kutokana ubora walionao wenzangu wanaocheza nafasi niichezayo na
wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki nafasi hiyo”, amesema
Nonga.
Nonga ameongeza kuwa uamuzi huo ni wakwake mwenyewe na
wala hajashurutishwa, ”Maamuzi haya ni yangu binafsi sijashurutishwa na
mtu, nafanya hivi ili nijaribu kukinusuru kipaji changu”, aliongeza Paul
Nonga.
Je kuna ukweli ndani yakeeee!!!! Na tusubiriii majibu hapa hapa Lyamba Lya Mfipaaaa!
Tuesday, May 31, 2016
Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM yaanza Mjini Dodoma
Luhwavi akitazama hali ya maua kwenye bustani za jengo la ukumbi huo. |
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akihoji kuhusu hali ya bustani zinazozunguka jengo hilo. |
Luhwavi akielekeza namna ya kuboreshwa bustani zinazozunguka jengo la ukumbi huo. |
Luhwavi akiingia ndai ya ukumbi wa jengo hilo kuona hali halisi. |
Bendera ya Taifa na bendera ya CCM zikipepea kwenye jengo hilo la Mikutano la CCM, kama ilivyo kawaida. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO |
Mkutano wa Mapitio ya Mpango wa Taifa kwa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Wafanyika ARUSHA
Profesa Ayoub Magimba akisalimiana na Mshauri wa Kitaalamu wa Shirika la RTI International kutoka Washington DC. |
Profesa Magimba akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa mkutano huo... |
SABABU 10 WAZEE MBEYA KUMUUNGA MKONO JPM
Na Joachim Nyambo.
“Kaulimbiu ya Hapa Kazi Tu inatukumbusha kaulimbiu
za huko nyuma kama vile Uhuru na kazi,Uhuru ni kazi na Heshima ya mtu
kazi” Ni kauli ya Mwenyekiti wa wazee
wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mbeya,Isakwisa Mwambulukutu wakati wazee
hao walipotoa tamko la kupongeza utendaji kazi wa rais John Magufuli.
Tamko hilo liliungwa mkono na wazee wengine
wanachama wa umoja huo wakiwemo Edward Ndonde,Daniel Fussi,Kikeke A
Kikeke,Rogate Masuba,John Mushi,Bujo Mwakatumbula,Joji Nyirenda,Boniface
Kasyunguti,Philimon Mwansasu na mmoja wa waasisi wa TANU mkoani Mbeya,Helena
Mwaipasi.
“Sisi wazee tunaounda umoja wa Wazee wa CCM
tunaoishi jijini Mbeya kwa niaba ya wazee wenzetu tunapenda kutoa tamko rasmi
la kumpongeza rais John Magufuli kwa utekelezaji wake mzuri wa Ilani yetu ya
CCM ya uchaguzi ya mwaka 2015 na utendaji wake mzuri wa kazi katika awamu hii
ya tano ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”alisema Mzee Mwambulukutu.
“Tunapotoa tamko la kumpongeza Dk.Magufuli
isieleweke kuwa tunaziona awamu nyingine zilizotangulia hazikufanya
mazuri,lahasha.Kama alivyosema aliyekuwa rais wa awamu ya pili Alhaji Ali
Hassan Mwinyi kuwa Kila zama na Kitabu chake,viongozi wa awamu zilizotangulia
kila mmoja alifanya mambo kwa kadiri ya karama aliyojaliwa na Mwenyezi Mungu
kulingana na hali halisi ya wakati wake huo.Hara Dk Magufuli ni moja ya matunda
ya awamu hizo zilizotangulia”anasema.
Mwenyekiti huyu anasema ni Ukweli usiopingika kuwa
maendeleo ya mtu au Taifa kwa ujumla hayawezi kupatikana kama watu hawataki
kufanya kazi.Ni jambo la kumpongeza rais kwa kuhimiza hilo na anapaswa
alisimamie kwa nguvu zote ili nchi iweze kujikwamua kutokana na lindi la
umasikini.
Wazee hawa wanasema sababu ya pili ya kumpongeza
rais ni Kuimarisha nidhamu na uwajibikaji wa watumishi wa umma.Watumishi wengi
wa umma walifikia mahali ambapo walifanya kazi kwa kadiri ya matakwa yao bila
kujali taratibu na kanuni za kazi.
“Walisahau ile kauli mbiu aliyotoa rais Ally Hassan
Mwinyi isemayo,Usipowajibuka,Ole Wako,Utakumbana na Fagio la Chuma.Sisi wazee
tunaamini Magufuli ni fagio la Chuma,kwani matokeo tumeanza kuyaona kwenye
sehemu ambazo huduma hutolewa kama vile hospitali,ofisi za serikali na sehemu
nyinginezo.”
Sababu ya Tatu ni Kupambana na rushwa,ukwepaji kodi
na ubadhirifu wa mali za Umma.Anasema Kwa kwa Kutumbua Majipu,Dk.Magufuli
anawakumbusha enzi za Hayati Edward Moringe Sokoine alipopambana na Wahujumu
Uchumi.
“Sisi wazee tunamwombea rais Magufuli Mungu
amlinde,ili atumbue majipu yote,vipele,chunusi na kukwangua kabisa ukurutu ili
Tanzania yetu ibaki safi na yenye afya njema kiuchumi na kiustawi wa jamii”
Kuboresha huduma za jamii ili kuleta hali nafuu ya
maisha ya watanzania ni sababu ya nne wanayoitaja wazee hawa kuwasukuma kutoa
pongezi zao.Hii ni pamoja na kuboresha huduma hospitalini,kutoa elimu bure toka
chekechea hadi kidato cha nne na kuhakikisha mikopo inapatikana kirahisi kwa
vijana wa elimu ya juu.
“Kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya
barabara,reli,umeme,maji na mingine mingi hapa anatukumbusha usemi wa It can be
done play your part.Hivyo tunatoa wito kwa watanzania wenzetu kutimiza wajibu
wao pale walipo ili huduma za kijamii ziweze kuwa bora na kutufanya wote tuwe
na maisha nafuu”.
Kufufua na kuhimiza ujenzi wa viwanda ili kuongeza
ajira,kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na Kilimo,uvuvi na Ufugaji na kuinua
uchumi wa Taifa pia limewakosha wazee hawa.Wanasema wameanza kuona matunda
kwani mkoni Mbeya tayari kiwanda cha Zana Za Kilimo(ZZK) kimeanza kufanya kazi
na baadhi ya vijana wamepata ajira.
“Hapa tukizingatia ile kaulimbiu ya Kupanga ni
Kuchagua hakuna kitakachoshindikana.Hivyo tunaomba juhudi ziendelee ili kufufua
viwanda vingine kama vile HISoap,kiwanda cha nguo na kiwanda cha kusindika
nyama”
Jambo jingine ni Kuboresha na maslahi ya wafanyakazi
kwa kuanza na kupunguza kodi itokanayo na mishahara yao kutoka asilimia 11 hadi
asilimia tisa.Wanasema wanaamini kutokana na Kutumbua Majipu,kudhibiti wafanyakazi
hewa na madeni hewa hali ya kiuchumi itakuwa bora na hivyo kuwezesha kuongezeka
kwa mishahara ya wafanyakazi na huduma bora kwa umma zitapatikana.
“Jambo ji ngine ni kuhimiza ujenzi wa Taifa
linalojitegemea.Ile kauli ya rais Magufuli ya Bora kushindia mihogo,kuliko
mkate wa Siagi wa masimango unatukumbusha kauli ya Baba wa Taifa Hayati Julius
Nyerere ya Heri kuwa masikini na Huru,Kuliko kuwa Tajiri na Mtumwa”
“Sisi wazee tunamwomba rais wetu akaze uzi wala
asijali vitisho vya wafadhili wanafiki na maneno ya Wanasiasa Uchwara.Tunaamini
pia kwa kubana matumizi ya serikali kwa kupunguza safari za nje ya nchi,posho
za vikao visivyo na tija kwa taifa letu na kupunguza sherehe zinazomaliza fedha
nyingi nchi yetu itaweza kujikwamua kiuchumi na hatimaye kuweza kujitegemea”
Wazee hawa wanasema unyenyekevu aliouonyesha
Dk.Magufuli wakati wa kuzindua Daraja la Kigamboni ni wa kipekee.Pamoja na
kwamba usimamizi wa ujenzi wa daraja hilo ulikuwa chini yake tangu alipokuwa
Waziri wa Ujenzi,alikataa daraja hilo kuitwa jina lake na badala yake aliamua
liitwe Daraja la Nyerere,kwa kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuimarisha umoja wa
Kitaifa na kupigania Uhuru wa Bara la Africa.
Mzee Mwambulukutu anasema Kudhibiti uagizwaji holela
wa sukari toka nje ya nchi ili kuhakikisha watanzania wanapata sukari iliyo
salama na kwa bei nafuu na pia kukuza viwanda vya sukari vya hapa
nchini,inastahili pongezi.Pamoja na purukushani za hapa na pale zinazofanywa na
wafanyabiashara wasio na Uzalendo wanaamini juhudi za Rais zitashinda kwakuwa
Palipo na Mwanga,giza hujitenga.
“Jambo la mwisho ni kudhibiti hali ya ulinzi na
usalama visiwani Zanzibar na hivyo kufanikisha uchaguzi wa marudio bila
fujo.Akiwa Amirijeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,aliweza
kuhakikisha ulinzi na usalamakatika visiwa vya Zanzibar unakuwepo na hivyo kuwezesha
uchaguzi wa marudio kufanyika hapo Machi 20 mwaka hu bila vurugu zozote.”
“Sisi wazee tunampongeza kwa hilo na tunapongeza
ushindi wa kishindo wa CCM katika uchaguzi huo,uliofanyika kwa amani na
utulivu”alisema Mzee Mwambulukutu.
Wazee wengine akiwemo Kikeke A Kikeke,wanasema
juhudi na ushirikiano wa pamoja baina ya watanzania wote pasipokujali nafasi
waliyonayo ndiyo utakaowezesha mikakati mbalimbali ya Dk.Magufuli
kufanikiwa.iwapo kutakuwepo na makundi ya watu wanayojitenga na kukwamisha itakuwa
vigumu kwake kuwezesha watanzania kupiga hatua kimaendeleo.
Kwa upande wa katibu wa umoja huo Philimon
Mwansasu,alisema watanzania wanapaswa kutambua kuwa maisha bora hayawezi
kupatikana kama taifa litabakia mikononi mwa matajiri wachache wenye kupenda
kulimbikiza mali kwaajili yao na familia zao na kuwaacha masikini wakiwa
watumwa ndani ya taifa lao.
“Tunachopaswa kufanya watanzania wote ni kushirikia
katika mipango ya rais kuhakikisha tunafichua maovu yote yanayofanywa na
watendaji wabovu.Kuchukuliwa kwao hatua ndiyo mwanzo wa walalahoi kupata unafuu
wa ugumu wa maisha.Tukisema tushirikiane na wahalifu kwa madai kuwa tunawaonea
huruma tutakuwa tunazidi kujikwamisha wenyewe”anasema Mwansasu.
Mwisho.
Saturday, May 28, 2016
KUMEKUCHA KIPYE CUP 2016,TIMU 14 KUTEULIWA KUSHIRIKI
MAANDALIZI ya Mashindano ya kuibua
vipaji katika soka Wilayani Mbarali mkoani Mbeya ya Kipye Cup 2016 yamezidi kushika kasi ambapo kesho(Mei 29)
timu 14 zinatarajiwa kupitishwa ili kushirili mashindano hayo.
Kwa mujibu wa mratibu wa Kipye
Cup,Frank Kipye,mashindano hayo ambayo ni msimu wa tatu sasa tangu kuasisiwa
kwake yatashirikisha timu 14 ambapo tati ya hizo 10 zitakuwa zikitokea katika
kata ya Mapogoro wilayani Mbarali na nne ni kutoka nje ya kata hiyo ili kuleta
ushindani.
Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa,Kipye
amesema kamati ya ligi hiyo kesho itakuwa na kazi ya kupitisha timu 14 kati ya
zile zilizochukua fomu kuomba usajiri wa kushiriki mashindano hayo.
Amesema mara baada ya timu shiriki
kuteuliwa,kazi itakayokuwa imesalia ni kutangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa
michuano huku akisisitiza kuwa zawadi kwa msimu huu ni mshindi wa kwanza Ngombe
mwenye thamani isiyopungua shilingi milioni 1.5,mshindi wa pili lakini tano,wa
tatu laki tatu.
“Lengo la mashindano hayo ni kuibua
vipaji vya soka sambamba na kutoa hamasa kwa jamii kupenda michezo kutokana na
faida zake nyingi ikiwemo vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya,ulevi na
pia ngono zembe.”
Kipye amesema msimu huu mashindano
yanatarajiwa kuwa na mvuto zaidi kutokana na kamati ya maandalizi kuamua
kuongeza idadi ya timu kutoka nje ya kata ya Mapogoro.
“Ligi itaendeshwa katika uwanja
uliopo Mabadaga kata ya Mapogoro.Tumeona tuongeze timu kutoka nje ya kata ili
kuleta mvuto zaidi.Mwaka jana tulishirikisha timu mbili tu kutoka nje ya
kata.”anasema Kipye.
Kwa msimu wa mwaka jana bingwa wa
ligi hiyo ilikuwa timu ya Kapunga FC ambao mwaka huu wanatarajiwa kuwa mabingwa
watetezi.
Thursday, May 26, 2016
NIACHE NISOME YAZINDULIWA RASMI
MKUU
WA MKOA WA MOROGORO DR KEBWE STEVEN KEBWE AMEZINDUA KAMPENI YA NIACHE NISOME
ILIYOHASISIWA NA MKUU WA WILAYA YA ULANGA YENYE LENGO LA KUTOKOMEZA TATIZO LA
MIMBA KWA WANAFUNZI.
AKIZINDUA
KAMPENI HIYO ILIYO NA KAULIMBIU YA MAGAUNI MANNE, YENYE TAFSIRI YA SARE YA
SHULE, JOHO LA MAAFALI, GAUNI LA HARUSI
NA GAUNI LA MAMA MJAMZITO AU MATENITI, MKUU WA MKOA AMEPONGEZA HATUA HIYO NA
KUSISITIZA KUWA ITAINUA KIWANGO CHA UFAULU KWA WANAFUNZI WA KIKE WILAYANI HUMO.
DR
KEBWE MARA BAADA YA KUZINDUA KAMPENI HIYO AMEPIGA MARUFUKU USHIRIKI WA
WANAFUNZI KATIKA SHUGHULI ZA MUZIKI UNAOPIGWA NYAKATI ZA USIKU MAARUFU KWA JINA
LA VIGODORO NA KUMTAKA MKUU WA WILAYA KUWAFUATILIA WANAOHUSIKA KUWAPA MIMBA
WANAFUNZI NA KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.
AIDHA
KATIKA KUUNGA MKONO KAMPENI HIYO YA NIACHE NISOME MAGAUNI MANNE MKUU WA MKOA
DR. KEBWE AMEKABIDHI VITI NA MEZA THEMANINI NA TANO ZILIZOTOLEWA NA KAMPUNI YA
UCHIMBANI MADINI YA KIBARAN KWA AJILI YA SHULE YA SEKONDARI YA NAWENGE.
MKUU
WA MKOA AMEIPONGEZA KAMPUNI HIYO KWA KUANZA KUONESHA NIA YA KUSAIDIA JAMII
KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA MAENDELEO, HUKU AKISISITIZA HALMASHAURI KUSIMAMIA
MIKATABA NA KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI ILI KUONGEA MAPATO YA NDANI YA WILAYA.
MWANDISHI: GEOFREY LIKANGAGA
Saturday, May 21, 2016
ZIARA YA WANACHAMA WA TAJATI,SUPRISE BEACH MJINI MAKAMBAKO
Wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) wakipiga picha ya pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya Star Entergrated inayomiliki Suprise Beach Bw.Patrick Kyando (aliyeshika kitabu)kabla ya kuanza kutembelea vivutio mbalimbali ndani ya eneo lake.
Baadhi ya wanachama wa TAJATI wakiwa wamepanda mkokoteni unaokokotwa na Punda kuelekea Suprise Beach.
Mwenyekiti wa TAJATI,Bw.Ulimboka Mwakilili akiwa amepanda Farasi njiani kuelekea Suprise Beach.
Hapa ni langoni pa Suprise Beach.Ukifika hapa lazima utavutiwa kupiga picha kwaajili ya ukumbusho kama ilivyotokea kwa wanatajati hawa.
Mwenyeji akitoa maelezo katika eneo ambalo hutumika kwa shughuli mbalimbali ikiwemo sherehe za Harusi.
Kwa mbaali kulia ni mfano wa Mlima Kilimanjaro na kushoto ni mfano wa boti.Hapa unaweza kujifunza kupanda mlima na pia kupanda boti.
Wanatajati wakiwa wamepozi katika eneo lililopewa jina la Mwanza.Kimsingi linavutia na unaweza kujihisi kweli umefika jijini Mwanza kutokana na mandari yanayofanana.
Mwanahabari kutoka TV 1 Laudence Simkonda akipiga kasia alipoamua kucheza na Mtumbwi kabla ya kupata ajali kama inavyoonekana hapo chini.
Wanatajati wakivuka kutoka eneo la Kigamboni kwenda kisiwani Zanzibar(Haya ni majina tu yaliyowekwa hapa)
Mwanahabari Felix Mwakyembe(aliyekaa) alikuwa mmoja kati ya wanatajati ambao hawakutaka kuondoka ndani ya eneo hili la kuvutia na la starehe za kipekee.
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Daniel Nyambo(Jodany)akionesha umahiri wa kusafiri ndani ya maji kwa kutumia Mtumbwi.
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Daniel Nyambo(Jodany)akicheza na nyani mdogo aina ya ngedere aliyepewa jina la King.
Mwanahabari Laudence Simkonda akiwa ametumbukia kwenye maji baada ya mtumbwi wake kupinduka.Hata hivyo kutokana na uzoefu wake aliweza kujiokoa mwenyewe pasipo hata kuhitaji msaada wa mtu mwingine.
Mhariri mkuu wa Lyamba Lya Mfipa Bw.Joachim Daniel Nyambo(Jodany) akiendelea na kazi ya kupiga picha za matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)