Mtendaji Mkuu wa Lafarge Tanzania Ilse Boshof akiwa
ameshika mfuko wa saruji aina ya TemboFundi akiwa pamoja na Mkurugenzi wa
masoko na mawasiliano
Mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa Lafarge,
Allan Chonjo akizungumza jambo wakati wa hafla ya kuzindua aina mpya ya saruji
ya Tembo Fundi
Meneja Mawasiliano wa Lafarge, Straton Bahati
akizungumza namna watakavyoweza kuwafikia wateja na kutoa elimu kuhusu matumizi
ya Saruji mpya ya TemboFundi.
Kampuni ya Saruji ya Lafarge
Tanzania imezindua saruji ya kwanza maalumu kwa matumizi ya uashi.
Saruji hiyo inayojulikana kama
Tembo Fundi itawapa wajenzi chaguo bora kwa ajili ya kazi za uashi ikiwa ni
pamoja na kupiga plasta ukuta, kusakafia, kujengea tofali na kupangilia
marumaru.
Saruji hiyo iliyotengenezwa maalum
kwa kazi ya uashi wa kuta za nje na ndani inatajwa kuwa na ubora katika kufanya
kazi, nguvu kwenye ugundishaji,inashika vizuri na ina umaliziaji bora wenye
kuleta matokeo yaliyo bora zaidi kwenye kujenga tofali, uzio, marumaru na
sakafu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo, Ilse Boshoff, alisema wakati wa uzinduzi kuwa Tembo Fundi imeundwa
mahususi kwa ajili ya kazi za uashi na kuwapa wajenzi utendaji bora wa kazi na
thamani ya fedha.
“Ikiwa imetengenezwa kutokana na uzoefu na
utaalamu wa Lafarge kimataifa katika kuzalisha saruji, Tembo Fundi ni rahisi
kutumia katika kupiga plasta, tofauti na saruji ya matumizi ya jumla ambayo
itamchukua muashi muda mrefu katika kusawazisha ukuta.”alisema Boshoff
Boshoff alisema faida nyingine
muhimu katika matumizi ya Tembo Fundi ni unafuu katika gharama kutokana na
mfuko mmoja wa Tembo Fundi kutumika eneo pana zaidi ukilinganisha na mfuko wa saruji
ya matumizi ya jumla.
Kutokana ya kwamba inafanya kazi
vizuri na uimara wake kudumu kwa muda mrefu Tembo Fundi itawasaidia wajenzi
kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment