WAREMBO 11 wanatarajia kupanda
Jukwaani ijumaa hii(Mei 20) kuwania taji la Miss Mbeya 2016 kwenye mashindano
yatakayofanyika katika Hotel ya Paradise,Soweto jijini Mbeya.
Warembo wanaowania taji hilo ni
Emmiliana Abdalla,Anitha Patric,Aziza Lysamuya,Praxeda Geofray,Juliana
Gilbert,Nancy Matta,Agnes Boliva,Julitha Mponela,Afrodisia Chapa,Eunicer
Robert,Priscar Mengi na Juliana Lyampawe.
Mratibu wa mashindano hayo Tom
Chilala amesema maandalizi yote yamekamilika na kilichobakia ni warembo kupanda
jukwaani mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala atakayekuwa mgeni rasmi.
Chilala amesema kuwa majaji wa
shindano hilo akiwemo mwenyekiti wa shindano la Miss Kanda ya nyanda za juu
kusini Dosi Magambo ndiyo watakaosimamia vigezo vyote vya kuchagua mshindi.
“Shindano linatarajiwa kuvuta hisia
za mashabiki wengi kutokana na muonekano wa warembo wa mwaka huu na pia
umaarufu alionao kwa sasa msanii Hamornize atakayepamba onesho hili”
“Awali washiriki walikuwa kumi na
tano lakini baada ya kuwachuja wakiwa kambini wamebakia kumi na moja ambao
ndiyo watapanda jukwaani kuwania taji”anasema Chilala.
Mratibu huyo amesema mshindi wa
kwanza katika mashindano hayo atazawadiwa fedha taslimu shilingi laki saba,wa
pili laki nne,wa tatu laki tatu na wan ne laki mbili huku waliosalia wakipewa
kifuta jasho cha shilingi 80,000 kila mmoja.
No comments:
Post a Comment