Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 31, 2016

ETI NONGA ANUIA KUIKIMBIA YANGA!AKIRI KIWANGO CHAKE KUWA CHINI!!!

Maneno yaliyowekwa katika ukurasa wa FB wa Yanga yanaeleza hiviiiii......

”Nimeomba kuuzwa na tayari barua ipo mezani kwenye ofisi ya Yanga na nimewatajia mahali ninapopenda kuuzwa, nimeomba kuuzwa ili wasiingie hasara kwasababu walininunua kwa pesa nyingi. Sababu kubwa ya maamuzi Yangu haya ni nafasi finyu ya kucheza niliyonayo katika kikosi cha Yanga kutokana ubora walionao wenzangu wanaocheza nafasi niichezayo na wanatimiza majukumu yao ipasavyo na kuitendea haki nafasi hiyo”, amesema Nonga.

Nonga ameongeza kuwa uamuzi huo ni wakwake mwenyewe na wala hajashurutishwa, ”Maamuzi haya ni yangu binafsi sijashurutishwa na mtu, nafanya hivi ili nijaribu kukinusuru kipaji changu”, aliongeza Paul Nonga.


Je kuna ukweli ndani yakeeee!!!! Na tusubiriii majibu hapa hapa Lyamba Lya Mfipaaaa!

No comments:

Post a Comment