Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, May 31, 2016

Mkutano wa Mapitio ya Mpango wa Taifa kwa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Wafanyika ARUSHA

Mgeni rasmi wa Mkutano huo Profesa Ayoub Magimba ( kushoto ) akisalimiana na Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu ( NIMR ) Dkt Mwele Malecela ( kulia ), aliyesimama katikati ni Mratibu wa Mpango huo Dkt Upendo Mwingira.
Profesa Ayoub Magimba akisalimiana na Mshauri wa Kitaalamu wa Shirika la RTI  International kutoka Washington DC.
Profesa Ayoub Magimba akifungua Mkutano wa tano wa Mapitio ya Mpango wa taifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ambao unapitia na kupanga mikakati ya utekelezaji wa kutoa Elimu, kinga na kutibu magonjwa hayo ambayo ni Usubi,vikope,kichocho, minyoo ya tumboni pamoja na matende na Mabusha.
Waratibu wa Mpango huo kutoka halmashauri mbalimbali, wakijiandaa kuwasilisha mada zinazoelezea walivyofanikiwa kutekeleza mipango hiyo kwa mwaka 2015 / 2016, wa Kwanza kulia ni Dkt Mabai Leonard ( Mwanza ), katikati Dkt Faraja Lyamuya ( Dodoma ) na Dkt Ida Ngowi.
Profesa Magimba akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa mkutano huo...

No comments:

Post a Comment