Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 31, 2014

JE HAYA NI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA AU BORA MAISHA?

TAFAKARIII.....TOA MAONI

JE VIONGOZI WA KIJIJI HIKI WALIKOSA JINA JINGINE MPKA SHULE YAO IITWE JINA HILI?

TAFAKARI....TOA MAONI YAKO

BABA AHUKUMIWA MIAKA 65 KWA KUMPA MIMBA MTOTO WAKE WA KUMZAA.

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana(Machi 31) imemhukumu kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 65 jela mkazi wa mtaa wa Uhamila katika mji mdogo wa Rujewa kutokana na makosa matatu tofauti yaliyotokana na kumpa ujauzito mwanaye wa kumzaa. Mshitakiwa aliyehukumiwa kifungo hicho ni Benjamin Muyinga(48) ambapo mashitaka aliyokuwa akikabiliwa nayo mahakamani hapo ni Kufanya mapenzi na mtoto wake,kubaka mtoto wake na la tatu ni kumpa mamba mwanafunzi. Awali ilielezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mazoya Luchagula,mbele ya hakimu mfawidhi Kinabo Minja kuwa mnamo Oktoba 18 mwaka 2013 mwanafunzi(jina linahifadhiwa) aliyekuwa na umri wa miaka 14 alikuwa mjamzito. Luchagula alisema walimu wa shule hiyo ndiyo walitilia shaka suala la mwanafunzi huyo aliyekuwa darasa la tano katika shule ya msingi Ibara iliyopo Rujewa kuwa alikuwa na ujauzito na ndipo alipelekwa hospitali na kwenda kukutwa akiwa na mamba ya miezi minne. Alisema baada ya kuhojiwa mwanafunzi huyo alisema kuwa ujauuzito ulikuwa wa baba yake mzazi waliyekuwa wakiishi naye wawili nyumbani kwao kufuatia baba huyo kutengana na aliyekuwa mkewe ambaye hivi sasa anaishi jijini Mbeya. Alisema mwanafunzi huyo alibainisha namna alivyokuwa akiishi na baba yake baada ya wazazi wake kutengana na ndipo baba yake akamgeuza mwanaye huo kuwa mkewe ambapo alikuwa akilala naye na kufanya naye mapenzi hadi ilipobainika kuwa na ujauzito huo. Kutokana na kitendo kilichofanywa na mzazi huyo kutokubalika katika jamii ya watanzania,mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili kumpa fundisho yeye na wazazi wengine wenye tamaa zenye kusababisha ukatili dhidi ya watoto wao. Kufuatia kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo,hakimu mfawidhi Minja alimhukumu mzazi huyo katili kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 65 jela kwa makosa hayo matatu kitakachotekelezwa kwa wakati mmoja ili iwe fundisho kwa wazazi wenye tabia hizo. Hakimu huyo alimhukumu mshitakiwa kutumikia jela miaka 30 kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake,miaka 30 mingine kwa kubaka mtoto wake na miaka mitano jela kwa kumpa mamba mwanafunzi.

WACHARANGA MBUZI MAPANGA NA KUBOMOA NYUMBA YA MWENYEKITI WA KIJIJI

WATU WASIOFAHAMIKA WAMEFANYA UHARIBIFU WA MALI PAMOJA NA KUUA MIFUGO [MBUZI] WAPATAO 15 KWA KUWAKATA KWA MAPANGA MALI YA MWENYEKITI WA KIJIJI CHA USOKE WILAYA YA MOMBA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA STANSLAUS SIMWICHE (50). KATIKA TUKIO HILO WATU HAO WALIFANYA PIA UHARIBIFU KWA KUBOMOA NYUMBA YAKE. TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.03.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KIJIJI CHA USOKE, TARAFA YA KAMSAMBA, WILAYA YA MOMBA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA MWENYEKITI HUYO KUTUHUMIWA KUMROGA MAREHEMU FRANK ABEID ALIYEFARIKI MNAMO TAREHE 27.03.2014 HUKO TUSULU. THAMANI HALISI YA MALI ILIYOHARIBIKA NI SHILINGI 5,654,000/=. JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALE WOTE WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII NA BADALA YAKE WATATUE MIGOGORO YAO KWA NJIA YA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO. Signed by: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Monday, March 24, 2014

ANGLIKANA YAKABIDHI BAISKELI KWA WAELIMISHAJIRIKA WA UWAKI

Afisa Mradi wa UWAKI wa kanisa la Anglikana Bw.Patrick Cosima(aliyevaa skafu)akimkabidhi afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Jairo Shira baiskeli kwaajili ya kuwakabidhi waelimishajirika wa mradi huo kutoka kata za Ilembo na Masoko BAISKELI 22 zenye thamani ya jumla ya shilingi 3,740,000 zimekabidhiwa kwa waelimishaji rika wa mradi wa Kupinga ukatili wakijinsia(UWAKI) na ukatili dhidiya watoto katika kata za Ilembo na Masoko wilayani Mbeya. Baiskeli hizo zimekabidhiwa mwishoni mwa wiki na kanisa la Anglikana linaoendesha mradi huo katika kata hizo kwa hisani ya watu wa marekani kupitia shirika la Watereed. Akikabidhi baiskeli hizo,Afisa mtendaji wa kata ya Ilembo Jairo Shira amewataka waelimishaji rika kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wao. Shira ameendelea kusisitiza kuwa suala la kupinga ukatili wa kijinsia ni jukumu la kila mwana jamii kutokana na athari mbaya za ukatili huo ambazo ni pamoja na kushuka kwa uchumia wa familia husika. Kwa upande wake afisa mradi wa UWAKI wa kanisa la Anglikana Patrick Cosima amesema ni imani ya kanisa kuwa kwa kuwawezesha waelimishaji rika kuwa na usafiri wa baiskeli wataweza kuifikia jamii kwa haraka zaidi na kueneza elimu ya kupinga ukatili. Cosima amesisitiza kuwa kutolewa kwa baiskeli hizo ni mwanzo wa kuhakikisha jamii yote ya wakazi wa kata za Ilembo na Masoko inabadilika na kuwa mfano wa kuigwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani kwa kuacha vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto.

Tuesday, March 18, 2014

Monday, March 17, 2014