Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 31, 2014

BABA AHUKUMIWA MIAKA 65 KWA KUMPA MIMBA MTOTO WAKE WA KUMZAA.

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya jana(Machi 31) imemhukumu kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 65 jela mkazi wa mtaa wa Uhamila katika mji mdogo wa Rujewa kutokana na makosa matatu tofauti yaliyotokana na kumpa ujauzito mwanaye wa kumzaa. Mshitakiwa aliyehukumiwa kifungo hicho ni Benjamin Muyinga(48) ambapo mashitaka aliyokuwa akikabiliwa nayo mahakamani hapo ni Kufanya mapenzi na mtoto wake,kubaka mtoto wake na la tatu ni kumpa mamba mwanafunzi. Awali ilielezwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Mazoya Luchagula,mbele ya hakimu mfawidhi Kinabo Minja kuwa mnamo Oktoba 18 mwaka 2013 mwanafunzi(jina linahifadhiwa) aliyekuwa na umri wa miaka 14 alikuwa mjamzito. Luchagula alisema walimu wa shule hiyo ndiyo walitilia shaka suala la mwanafunzi huyo aliyekuwa darasa la tano katika shule ya msingi Ibara iliyopo Rujewa kuwa alikuwa na ujauzito na ndipo alipelekwa hospitali na kwenda kukutwa akiwa na mamba ya miezi minne. Alisema baada ya kuhojiwa mwanafunzi huyo alisema kuwa ujauuzito ulikuwa wa baba yake mzazi waliyekuwa wakiishi naye wawili nyumbani kwao kufuatia baba huyo kutengana na aliyekuwa mkewe ambaye hivi sasa anaishi jijini Mbeya. Alisema mwanafunzi huyo alibainisha namna alivyokuwa akiishi na baba yake baada ya wazazi wake kutengana na ndipo baba yake akamgeuza mwanaye huo kuwa mkewe ambapo alikuwa akilala naye na kufanya naye mapenzi hadi ilipobainika kuwa na ujauzito huo. Kutokana na kitendo kilichofanywa na mzazi huyo kutokubalika katika jamii ya watanzania,mwendesha mashitaka aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili kumpa fundisho yeye na wazazi wengine wenye tamaa zenye kusababisha ukatili dhidi ya watoto wao. Kufuatia kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo,hakimu mfawidhi Minja alimhukumu mzazi huyo katili kutumikia kifungo cha jumla ya miaka 65 jela kwa makosa hayo matatu kitakachotekelezwa kwa wakati mmoja ili iwe fundisho kwa wazazi wenye tabia hizo. Hakimu huyo alimhukumu mshitakiwa kutumikia jela miaka 30 kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake,miaka 30 mingine kwa kubaka mtoto wake na miaka mitano jela kwa kumpa mamba mwanafunzi.

No comments:

Post a Comment