Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, March 3, 2014

MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA AIBU TUPU

WADAU mbalimbali wameonekana kukerwa na mashindano ya Safari Lager Nyama choma ambyo kwa mkoani Mbeya yalifikia kilele pale katika viwanja vya Luanda Nzovwe eneo la CCM.Malalamiko ya wadau yanahusu mapungufu luikuki yaliyobainika wakati wa fainali hizo.Kwanza watoto ndio waliojitokeza kwa wingi wakati mashindano hayo yenye lengo la kuhamasisha kilevi yaani bia ya safari hayawahusu na ni hatari kwao kushiriki katika maeneo hao.Jambo la pili ni eneo husika kutokuwa na vyoo hivyo watu waliokula nyama choma na kulewa pombe zilizokuwa zikiuzwa hapo walijisaidia katika kuta za nyumba za wakazi waishio jirani haja kubwa na ndogo.Majengo ya shule ya msingi iliyopo jirani na eneo hilo yalikumbwa zaidi na tatizo hilo kiasi kwamba yalikuwa hayatamaniki hata kuyasogelea hususani ilipofika mida ya jioni.Ukweli ni kuwa ilifika wakati mtu anapopita maeneo hayo alitamani hata nyama choma aliyokula aitapike "Inasikitisha sana kampuni kubwa na inayojinadi kila siku kuandaa masjindano kama haya kwenye mazingira machafu yasiyozingatia afya ya mlaji wa hizo nyama choma zao.Hapa hatukuja kufurahi kiukweli unakunywa pombe na kula ukajisaidie wapi hapa" alisikika ntu mmoja akiponda maandalizi ya mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment