Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, March 13, 2014

MWANAMKE MWINGINE AJIFUNGUA MTOTO KWENYE CHOO CHA GUEST AKIISALITI NDOA MKOANI MBEYA

Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu mwanamke mmoja kujifungua mtoto alipokuwa akiisaliti ndoa yake huko mkoani Morogoro,Katika hali isiyo ya kawaida,mkazi wa kitongoji cha Sogea katika mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba Pendo Lyala (18) amejifungua mtoto katika choo cha nyumba ya kulala wageni. Tukio hilo lilitokea Machi 10 mwaka huu saa 4:00 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Shwali iliyopo nyuma ya shule ya msingi Mwaka, mkabala na barabara kuu iendayo Sumbawanga mkoani Rukwa. Imebainishwa kuwa binti huyo ambaye ujauzito wake haukujulikana ni wa miezi mingapi alikuwa katika nyumba hiyo ya kulala wageni kwaajili ya kupumzika na mpenzi wake. Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni aliyekuwa zamu Tresia Albeto,alisema msichana huyo aliingia usiku huo na mpenzi wake aliyejiandikisha kitabuni kwa jina la Fred Gamba mkazi wa Njombe ambaye alikuwa amechukua chumba namba 5. Tresia alisema mara baada ya kuonyeshwa chumba hicho,Gamba, alitoka nje na kuingia katika chumba hicho mara tatu katika nyakati tofautiakiwa anamuacha mpenzi wake ndani na kuna wakati aliingia akiwa na mfuko wa plastiki(Rambo) uliokuwa na chipsi na soda. Mhudumu huyo alisema baada ya Gamba kutoka mara ya mwisho na kwenda nje huku nyuma alisikia sauti ya kike ikiomba msaada,jambo lililomsukuma kwenda kushuhudia kilichokuwa kikiendelea. Alisema baada ya kuingia katika chumba namba tano alikuta mwanamke huyo akiendelea kupiga kelelea ya kuomba msaada akiwa katika choo cha chumba hicho. Alisema alikwenda moja kwa moja chooni kulikokuwa kukitokea sauti na kumkuta msichana huyo amelala chini na mtoto aliyekuwa amejifungua muda mfupi,alikuwa pembeni ya shimo la choo akilia. Alibainisha kuwa kufuatia mayowe yaliyopigwa na mwanamke huyo,baadhi ya wageni waliokuwa katika nyumba hiyo pia waliamka na kujaribu kutoa huduma ya kwanza ,lakini walikwama kwa sababu ya ukosefu wa vifaa salama. Alisema hali hiyo iliwachanganya kwa kutokujua la kufanya hadi alipo jitokeza msamaria mwema ambaye ni miongoni mwa mpangaji aliyekuwa na mke wake waliopanga katika nyumba hiyo walimchukua na kumpeleka katika kituo cha Afya Tunduma. Akizungumzia tukio hilo,ofisa Ustawi wa jamii katika mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma Godfray Simbeye alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kudai kuwa msichana huyo anaendelea kupata matibabu hospitalini hapo na hali ya mtoto inaendelea vizuri. Simbeye alisema msichana huyo alikuwa na mpenzi wake Gamba ambaye walikutana naye usiku huo kwa mapatano ya muda na kwamba alipokuwa chumbani alihisi haja kubwa ndipo alipokuwa chooni na wakati huohuo kujisikia uchungu. Akizungumza katika wodi ya wazazi Pendo alisema alishangaa kuona mtoto kwani hakujua kama muda wa kujifungua ulikuwa umefika na akabainisha kuwa Gamba walikutana kwa usiku huo na kufanya makubaliano ya kukutana kimapenzi kwa muda mfupi. Pendo aliyesema kuwa ni mhudumu katika baa aliyoitaja kwa jina la Udizungwa iliyopo eneo la ofisi za CCM kata ya Tunduma ambako ndiko alikutana na Gamba na kufanya makubaliano na kumtaja baba wa mtoto huyo aliyejifungua kuwa ni Victor aliyesema ni mkazi wa Kyela.

No comments:

Post a Comment