Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Friday, March 7, 2014

BASI LA SAIBABA LAUA ABIRIA MMOJA NA KUJERUHI NANE

BASI la Kampuni ya Saibaba limesababisha kifo cha abiria mmoja baada ya kupata ajali likitokea Dar es salaam kwenda wilayani Kyela mkoani hapa. Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana(machi 7) majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Mwambegele kata ya Kyimo wilayani Rungwe barabara ya Mbeya/Tukuyu. Msangi alisema basi hilo lililokuwa na namba za usajiri T 973 AVM aina ya Scania likiendeshwa na dereva ambaye hakufahamika jina mara moja likiwa linatokea Dar es salaam lilipinduka na kusababisha kifo cha mmoja wa abiria wake ambaye pia hakufahamika jina wala makazi yake baada ya basihilo kumlalia. Alisema abiria wengine nane wakiwemo wanawake sita na wanaume wawili walijeruhiwa na wote walilazwa katika hospitali ya Makandana iliyopo Tukuyu wilayani Rungwe. Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliomshinda dereva kumudu gari yake na kubainisha kuwa mara baada ya ajali kutokea dereva na kondakta wake walikimbia na wanatafutwa na polisi. Wakati huo huo mtembea kwa miguu kijana wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 12 na 14 asiyefahamika jina wala makazi yake amegongwa na kufa papo hapo na hari isiyofahamika namba wala dereva wake. Kamanda Msangi alisema mtu huyo aligongwa juzi(Machi 6) saa tatu asubuhi maeneo ya kijiji cha Mlima Mpepo kata ya Igoma wilayani Mbeya katika barabara ya Isyonje/Makete na mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.

No comments:

Post a Comment