Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, March 12, 2014

JAMBAZI WAVAMIA NYUMBA YA KULALA WAGENI

WATU wanne wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokuwa na bunduki wamevamia nyumba ya kulala wageni kijiji cha Mtowisa wiliyani Sumbawanga ,mkoa wa Rukwa na kuwapora wafanyabiashara wa ng'ombe fedha taslimu zaidi ya Sh milioni 13. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana kijijini hapo katika nyumba ya kulala wageni ya Kaozya mali ya Leonard Kaozya, mkazi wa Sumbawanga mjini wakiwa katika harakati za kununua ng'ombe kabla ya kuvamiwa majira ya saa tano usiku na majambazi hao. Taarifa iliyopatikana kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na polisi mkoani Rukwa, inaeleza kuwa usiku huo mara baada ya wafanyabiashara wa kabila Kisukuma kufika kwenye nyumba hiyo baadaye kuliibuka kundi hilo la majambazi waliofika na kuanza kumwulizia mhudumu wa nyumba hiyo ya wageni lakini mhudumu huyo alifanikiwa kutoroka na kwenda kujificha katika chumba kimoja cha nje. "Walipofika walitukuta baadhi ya watu tumekaa nje na walisema kuwa tupo chini ya ulinzi, walianza kuniulizia mimi lakini waliponikosa wakapaza sauti na kusema kuwa wanahitaji wafanyabiashara hao wa ng'ombe na walipowapata walieleza kuwa wao hawataka kuwaua ila walihitaji fedha walizokuwa nazo". Alisema Andrea Cherehani ambaye ni mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni. Andrea alisema kuwa baada ya kuona kuwa wafanyabiashara hao hawajitokezi walianza kurusha risasi zinazo kadiriwa kufika 17 kwenye paa za nyumba hiyo kabla ya kuingia kwenye vyumba vya nyumba hiyo kwa lengo la kuwasaka wanunuzi hao wa ng'ombe na kuanza kuwapiga kisha kuwapora fedha zao na kutoweka. HABARI KWA HISANI YA BLOGU YA PEMBEZONI KABISA Wafanyabiashara hao walioporwa fedha hizo kama walivyojiorodhesha kwenye kitabu cha wageni katika ni pamoja na Shija Rabandiye ambaye anadaiwa kuporwa zaidi ya Sh milioni 10 Masai Bumado na Bakaga Edward. "Kulikuwa na mfanyabiashara mwingine alikuwa maetoka nje na alipoingia akenda uani ili akachote maji ya kunywa bombani lakini aliposikia sauti ya wajambazi hao naye alikimbia kwa kupitia mlano wa uani huku akiacha wenzake wakisurubiwa na mmoja wao akipigwa na nondo katika paji la uso baada ya awali kukata kutii amri ya majambazi hao". alisema Andrea Mganga wa zamu wa kituo cha afya cha Mtowisa Linus Romani alikiri kuwapokea majeruhi wa tukio hilo ambapo amedai kuwa walialazwa hapo usiku huo kabla ya kuruhusiwa siku iliyofuata na kudai kuwa hali zao zinaendelea vema. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiowa kutokea katika maeneo jirani ya mpakani mwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa na Momba mkoani Mbeya ambao wana mahusiano ya kikabila na wafanyabiashara hao wa ng'ombe, hivyo ilikuwa rahisi kufuatilia nyendo zao. Kamanda wa Jeshi la polis mkoani Rukwa Jacob Mwaruanda licha kuthibitisha tukio hilo alisema kuwa tayari kikosi cha uchunguzi kimekwenda eneo tukio tangia juzi mchana na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.

No comments:

Post a Comment