Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, December 21, 2023

FAINALI LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP SONGWE FURAHA NYINGINE YA X-MASS

 


FINAL LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP SONGWE. kupigwa tarehe 24/12/2023 katika viwanja vya Tunduma day Sekondari iliyopo tunduma Kati ya MKWAJUNI FC kutoka Wilaya ya SONGWE na LAMBYA FC kutoka wilaya ya ILEJE kuanzia majira ya saa kumi jioni shamlashamla za fainal zitaanza mapema sana mwambie rafiki ni bonge Moja la fainal.LIGI YA MKOA STELLA FIYAO CUP 2023/2024 IMEDHAMINIWA NA MBUNGE VITI MAALUMU MKOA SONGWE MH.STELLA FIYAO

Thursday, October 26, 2023

KenGold wataka kujiimarisha zaidi kileleni Championship



 

NA MWANDISHI WETU


VINARA wa NBC Championship League KenGold FC wamewasili salama mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wao wa mzunguko wa nane dhidi ya Biashara United uliopangwa kuchezwa katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Jumamosi ya Oktoba 28,2023.

Vinara hao wamesema matarajio yao ni kuendeleza ushindi kwenye michezo yake ili kujiweka mahali salama zaidi hivyo wamejipanga kupata matokeo ya ushindi katika mchezo huo wa kesho.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada ya kuwasili Kagera mshambuliaji wa kikosi hicho, Emanuel Mpuka alisema licha ya kusafiri umbali mrefu wachezaji wote wapo na afya njema na morali kubwa kuelekea kwenye mchezo huo.

Aamesema matarajio ya matokeo bora yanatokana na maandalizi waliyoyafanya hata kabla ya kuanza kwa safari huku akisema mabadiliko ya hali ya hewa hayatarajiwi kuwa kikwazo kwao.

"Tunaamini kwenye maandalizi tuliyojiandaa, tumekuja kupambana kusaka alama tatu,hali ya hewa ya huku inautofauti mkubwa sana na Mbeya...kuna muda joto,kuna muda baridi na wakati mwingine mvua inanyesha kabisa. Lakini hiyo haituondoei kwenye nia yetu" Amesema Mpuka

Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefunga magoli 3 na Assist 2 kwenye kikosi cha KenGold FC ambacho kinaongoza msimamo wa NBC Championship League kikiwa na alama 16.

CHUNYA YAENDELEA KUWABURUZA WAPINZANI SHIMISEMITA DODOMA

 

Timu ya wanawake ya kuvuta Kamba ya Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ikiongozwa na Kiongozi mwanamama mwenye misuli Bi Devotha Mwasaga ikiendeleza ubabe wa Halmashauri ya wilaya ya Chunya Jijini Dodoma

NA MWANDISHI WETU, DODOMA


Halmashauri ya wilaya ya Chunya Bingwa mtetezi wa mchezo wa kuvuta Kamba  SHIMISEMITA msimu uliopita msimu huu bado inaendelea kuwabuluza wapinzani wake katika michezo ya watumishi inayoendela jijini Dodoma baada ya Timu ya wanawake kuvuta Kamba kuingia nusu fainali wakati Timu ya wanaume kuvuta kamba iko Robo Fainali

                          Chunya DC Vs Moshi DC (ME) mshindi CHUNYA DC

                         Chunya DC Vs Tunduma TC (KE) mshindi CHUNYA DC

Kwa matokeo hayo  Chunya Dc wanaume wametinga hatua ya robo fainali (Mtoano) ambapo watakutana uso kwa uso timu ya watumishi kutoka Arusha jiji  huku timu ya Chunya DC wanawake wao wametinga hatua ya nusu fainali ambapo watavaa na timu Kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (DAR CC) ambayo ni kesho asubuhi.


Kuelekea Mchezo wa Nusu Fainali kepten wa timu ya wanawakeChunya DC Kuvuta kamba Bi Devotha Mwasaga amesema kilichobaki kutoka kwa wanachunya ni dua, Sara na Maombi ili kufanikisha azma ya kuleta ushindi Chunya na hatimaye kuiheshimisha wilaya ya Chunya kwani upande wa Maandalizi hakuna changamoto yoyote timu iko salama.


“Tunachokihitaji kutoka kwa wananchunya ni maombi kila mmoja kwa Imani yake ili timu iweze kufanikiwa kutwaa ubingwa kwani upande wa maandalizi kila kitu kiko vizuri, wachezaji wana ari na morali wa kuhakikisha ubingwa unakuja Chunya hivyo tuiheshimishe Chunya yetu”.


Kwa upande wa timu wanaume kuvuta kamba kepteni wa Timu hiyo Ridhiwani Mshigati amesema bado timu iko Imara na iki tayari kwa michezo yote iliyo mbele yetu huku lengo ni lile lile kuchukua tena ubingwa katika mashindano hayo hasa kwa upande wa Mchezo wa Kuvuta Kamba.


“Kwenye mchezo wa kuvuta kamba tumeendelea na kutetea ubingwa wetu na ndo maana tumeshinda 2 bila kwa maana ya kwamba tuliocheza nao tumefunga awamu zote mbili, na kamba ina mbinu za kupata ushindi, sisi tumehatika kupata mtaalamu anatuongoza vizuri na kwasasa tuko kambini tunaendelea kupeana mbinu na kutunza nidhamu. kurudi mikono mitupu kwa Mwajiri ni aibu kubwa ambayo sisi hatutaki itokee kwetu kulingana na huduma tulizopewa na mwajili wetu.


Na tunashukuru Halmashauri jirani za Rungwe na Tunduma wanatusapo, ingawa Tunduma Tc walifungwa na timu ya wanawake kuvuta kamba tuliwaomba radhi na kuwambia kwa hili hatuna ujirani tukawatoa, Tunaomba  watu wa Chunya waendelee kutuombea ili kutetee ubingwa wetu na lengo ni siku ya kufungwa kwa Mashindano haya Halmashauri yetu ya Chunya Itajwe na Mgeni rasmi na Bendera yetu iweze kupepea mbela ya Halmashauri zaiidi ya Mia moja zilizoshiriki Mashindano hayo” amesema Mshigati.


Utofauti wa hatua yaani Timu ya wanaume kuwa hatua ya Robo Fainali (Mtoano) huku timu ya wanawake kuwa hatua ya Nusu Fainali umetokana na Idadi ya timu zilizoshiriki mchezo huo kwani Timu za wanawake zilikuwa chache kulinganisha na timu za wanaume hivyo kupelekea  kupelekea baadhi ya hatua za mashindano kuwa na mzunguko mfupi kulingana na timu za wanaume.


Halmashauri ya wilaya ya Chunya Ndiye Bingwa Mtetezi wa Mchezo wa Kuvuta Kamba Taifa kwa msimu wa mwaka 2022 na sasa timu zote ziko hatua nzuri kutetea ubingwa mwaka huu 2023, Maombi, bahati pamoja na kujituma vitaendelea kuhitajika ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri

Friday, August 11, 2023

USHIRIKI WA MASHUJAA FC LIGI KUU TANZANIA KUONGEZA CHACHU YA MAENDELEO KIGOMA


 Na Mwandishi Wetu, Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema ushiriki wa Timu ya Mashujaa FC katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara utaongeza chachu ya Maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Kigoma.

Andengenye ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua Maendeleo ya Ukarabati wa Uwanja wa CCM Lake Tanganyika Stadium utakaotumiwa na Timu ya Mashujaa kwa ajili ya michezo ya nyumbani katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara Msimu wa 2023/2024.

Ameeleza kuwa, kutokana na ushiriki wa timu hiyo, Mkoa utapokea wageni kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kushuhudia michezo ya ligi kuu ambapo kuanzia wafanyabiashara wakubwa  hadi wajasiriamali wadogo watapata fursa ya kunufaika kiuchumi kutokana na kuwahudumia wageni hao.

"Pamoja na kupata burudani, michezo inatoa fursa  mbalimbali za kujiimarisha kiuchumi kupitia biashara, nitoe wito kwa wafanyabiashara na wakazi kwa ujumla tuchangamkie fursa za kiuchumi zitakazojitokeza ambazo zitatokana na wageni watakaokuja kwa ajili ya kushuhudia michezo mbalimbali ya ligi kuu" amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Upande wake Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mha. Francisco Magoti amesema ukarabati huo unahusu maeneo ya majukwaa, vyumba vya kubadilishia nguo kwa wachezaji, ukumbi wa mikutano, vyoo pamoja na eneo la kuchezea mpira.

" Mafundi wapo kazini na tutahakikisha  maboresho muhimu yanakamilika kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania Bara ili kuruhusu michezo ifanyike kama ilivyopangwa huku uwanja ukiwa katika ubora unaotakiwa" amefafanua Magoti.

Upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Kigoma, Edward Manase amesema  wameridhishwa na maendeleo ya kazi mbalimbali zinazofanyika za marekebisho ya uwanja huo huku akiwahimiza watendaji kutanguliza uzalendo na kuzingatia ubora.

Hisia zote:
6

MAMBO YOTE NI KESHO,TUKUTANE UYOLE

 


 


Wednesday, June 28, 2023

 https://www.facebook.com/100001526491541/videos/163778579924492/

Wednesday, June 14, 2023

SINGIDA BIG STARS YAPIGWA MNADA

Na Lyamba Lya Mfipa
Uongozi wa klabu ya Singida Big Stars umefikia makubaliano ya kuiuza timu hiyo kwa wamiliki wa Fountain Gate.

Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars John Kadutu amesema hayo mkoani Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema wameridhia kuiuza timu hiyo kwa fountain Gate, lakini kwa sharti la timu hiyo kubakia mkoani Singida.
Kwa upande wake Mmiliki mpya wa Timu hiyo Japhet Makau amesema, fursa hiyo imekuja katika wakati muafaka ndio maana wamemua kuichangamkia.
Kwa sasa jina la Singida Big Stars limebadilishwa na kuitwa Singida Fountain Gate Football Club.

MICHUANO TULIA TRUST BODABODA CUP 2023 YAZINDULIWA RASMI.

 
Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na wachezaji wa timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

Na Joachim Nyambo, Mbeya.

 

MEYA wa jiji la Mbeya Dormohamed Issa amezindua rasmi michuano ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 yatakayoshirikisha timu nane kutoka kanda za madereva bodaboda zilizogawanywa kwenye makundi mawili ya A na B.

 

Michuano hiyo imerejea tena baada ya kusitishwa kwa misimu miwili mfululizo ambapo kwa mara ya kwanza yalifanyika 2019 lakini kwa miaka iliyofuata haikufanyika kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mlipuko wa Covid-19

 

Kwa upande wa kundi A timu zinazoshiriki michuano hiyo ni za madereva bodaboda kutoka kanda za Iyunga, Stendi Kuu, Soweto na Kabwe wakati kundi B zipo timu za kanda za Mafiati, Sae, Uyole na Kadege.

 

Akizindua michuano hiyo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge, Meya wa jiji la Mbeya Meya Issa ameipongeza Taasisi ya Tulia Trust inayoyaandaa akisema yana mchango mkubwa katika kuibua na kukuza vipaji vya vijana.

 

Amewasihi madereva bodaboda kutumia michuano hiyo situ kwa kuibua vipaji vyao bali pia kuimarisha afya zao hivyo kuwataka kuwa na nidhamu ya hali ya juu wakati wote yatakapokuwa yanaendelea.

 

“Mpira unaanza kucheza chini lakini haujui huko mbele utafika wapi…naamini kabisa kuna wachezaji miongoni mwenu mkionyesha nidhamu mkazingatia yale mnayofundishwa na walimu kuyafuata ipo siku mtafika mbali.”  

 

“Mpira ni nidhamu..na ukitaka kufanikisha katika jambo lolote weka nidhamu mbele..ukiamua kuwa padre weka nidhamu mbele, ukitaka kuwa shekh weka nidhamu mbele na hata ukitaka kuwa kiongozi wajali watu wako.” Amesisitiza Issa.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Chama cha soka Mbeya mjini(Mufa), Ramadhan Nyambala amesema kutokana na ari ya mpira wa miguu katika mkoa wa Mbeya ni muhimu wadau wengi kuzidi kujitokeza kuandaa mashindano mbalimbali.

 

Amesema kuandaliwa kwa mashindano kama ya Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 ni sehemu ya mikakati muhimu na inayotarajiwa kwenye kuibua na kukuza vipaji vya vijana.

 

Afisa Habari na Mawasiliano wa Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema baada ya michuano hiyo kufanyika kwa mara ya kwanza 2019 iaka miwili mfululizo ilisimama kutokana na changamoto mbalimbali zilizoibuka ikiwemo cha mlipuko wa ugojwa wa corona.

 

Mwakanolo amesema michuano hiyo itakayokuwa ikifanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge na Magereza Mbeya yanatarajia kufikia tamati mwezi ujao huku akisema zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu zitatangazwa hivi karibuni.

Meya wa Jiji la Mbeya, Dormohamed Issa akisalimiana na waamuzi wa mchezo kati ya timu za Madereva Bodaboda za Uyole na Stendi kuu kwenye uzinduzi wa Tulia Trust Bodaboda Cup 2023 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge.

Sunday, June 11, 2023

Tulia Trust Bodaboda Cup hatua ya makundi

Tunakutana jumatatu hii Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge Jijini Mbeya tukizindua msimu wa Pili ligi ya TULIA TRUST BODABODA CUP 2023.

Wednesday, May 31, 2023

MAHUNDI AWAPA SAPOTI MWANJELWA VETERANI

 
Naibu waziri wa maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapa sapoti ya vifaa mbalimbali wachezaji soka wa zamani wa Mwanjelwa Veterani kuelekea Bonanza la  maveterani  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambalo limepangwa kufanyika Juni tatu na nne mwaka huu.


Kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika jijini Mbeya kwenye uwanja wa Magereza na uwanja wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(Must).

 

Mwenyekiti wa Mwanjelwa Veterani Ndambi Mwaipopo amesema wao kama wenyeji wa mashindano hayo wanamshukuru Naibu waziri wa maji Mahundi kwa kuendelea kuwaunga mkono wachezaji waliocheza soka zamani maarufu kama maveterani ambao wamekuwa wakikutana mara kwa mara.

 

“Tunamshukuru sana Mhandisi Mahundi amekuwa bega kwa bega kusapoti michezo,mabonanza haya yanatukutanisha wachezaji wakongwe,tunabadilishana uzoefu wa mambo mbalimbali"amesema Mwaipopo

 

Mwanjelwa Veterans ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo ambapo msimu uliopita walifanikiwa kuchukua ubingwa wa Bonanza hilo ambalo lilifanyika Songea na Ilula.

 

CREDIT TO SHABAN NASSORO

PRISONS YAPIGA MARUFUKU WACHEZAJI NDONDO CUP

Klabu ya Soka ya Tanzania Prisons imepiga marufuku wachezaji wake kucheza michezo ya ligi za mchangani maarufu kama Ndondo Cup katika kipindi hiki cha kuelekea kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya NBC 2022/23.

 

Ofisa habari wa Prisons, Jackson Mwafulango amesisitiza kuwa ni marufuku wakati ligi ikiwa bado haijamalizika mchezaji wao kuchezea ndondo Cup na kusisitiza kuwa mchezaji yeyote atakaebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

 

CREDIT TO SHABAN NASSORO


Tuesday, May 30, 2023

ZILIZOFUZU NUSU FAINALI AESHI SUPER CUP 2023

 


KUTOKA SUMBAWANGA- AESHI SUPER CUP 2023

 


MWENENDO WA AESH SUPER CUP- SUMBAWANGA.

 


KENGOLD KUVUNJA KIKOSI CHOTE, BENCHI LA UFUNDI


Mkurugenzi wa kikosi cha KenGold FC Keneth Mwakyusa Mwambungu amepanga kufanya maboresho makubwa katika timu hiyo kuelekea msimu ujao wa ligi ya Championship...!!

Mwambungu amesema baada ya kumalizika ligi wamefanya tathimini na kubaini mapungufu mbalimbali hivyo wanaanza kuyafanyia kazi mapema....!!
""Unajua ligi daraja la kwanza ni ngumu sana,,tumecheza huu msimu wa tatu sasa,,navunja kikosi chote pamoja na benchi la ufundi,tunaanza upya" Amesema Keneth
Nae Katibu mkuu wa KenGold Benson Mkocha ameongeza kuwa baada ya kushindwa kufikia malengo ya kupanda ligi wameona waanze upya ambapo hivi karibuni wataanza kutangaza utaratibu wa namna gani watafanya usajili...

MBEYA KUZIDI KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA.

 Mwenyekiti wa Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya(MREFA) Sadiki Jumbe amesema mkoa wa Mbeya umejaaliwa vipaji hivyo watahakikisha soka linachezwa kila sehemu...!!

Jumbe ameyasema hayo wakati wa Hafla ya utambulisho wa mashindano ya MO Quality Mbeya Ndondo Cup ambapo amesema kupitia mashindano hayo wanaamini wataibua vipaji ambavyo vitakuwa msaada kwa soka la Tanzania...!
""Mkoa wa Mbeya ni wa pili kisoka ukiondoa Dar es Salaam,tuna timu tatu za ligi kuu,tunatamani kuona hizi ndondo zinachochea maendeleo katika soka," amesema Jumbe
Mashindano ya MO Quality Mbeya Ndondo Cup 2023 yamepangwa kuanza kutimua vumbi June 10,2023 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge ambapo timu 16 zitashiriki michuano hiyo...!!




Saturday, May 20, 2023

HAKUNA MCHEZAJI ANAEDAI MSHAHARA MBEYA CITY


Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Dour Issa Mohamed ambae pia ni mlezi wa klabu ya Mbeya City amesema hakuna mchezaji yoyote anayedai mshahara kama inavyoripotiwa na baadhi ya wadau wa soka...!!

Ameyasema hayo wakati Taasisi ya Tulia Trust ikizindua zoezi la ugawaji wa jezi za mashabiki wa Mbeya City kutoka Kata zote 36 ndani ya jiji la Mbeya kwa lengo la kuhamasisha michezo....!!
""Maneno yamekuwa mengi ,,niwahakikishie wachezaji wamelipwa mpaka mwezi wa nne 2023 hakuna mchezaji anaedai mshahara,hata bonasi zao zote wamelipwa,,wale vijana wanafanya kazi wanafamilia zinawategemea kwaio lazima tuwawekee mazingira mazuri,tunathamini sana jasho lao"" amesema Dour Mohamed..
Hata hivyo ameongeza kuwa wadau na mashabiki wanapaswa kushikimana ili kuhakikisha kikosi chao kinamaliza vizuri michezo yao miwili iliyosalia ya kumaliza msimu wa mwaka 2022/2023 dhidi ya Yanga pamoja na KMC.

Friday, May 5, 2023

TFF YATUPILIA MBALI MAOMBI YA FEISAL JUU YA YANGA.

 


TANZANIA YACHAGULIWA KWA KISHINDO KUWA MAKAO MAKUU YA BARAZA LA MICHEZO AFRIKA KANDA YA NNE


 Na Mwandishi Wetu, Arusha.

 

Nchi Wanachama wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV zimeichagua  Tanzania kuwa  Makao Makuu ya Sekretarieti ya Baraza hilo linaloundwa na nchi 14.

 

Ushindi huo umepatikana kupitia mkutano wa Baraza hilo uliofanyika jana Mei 4, 2023 jijini Arusha chini ya uongozi wa na Mwenyekiti  Mhe. Peter Ogwang ambaye ni Waziri anayeshughulikia masuala ya Michezo nchini Uganda.

 

Tanzania imepitiswa na Wajumbe kutoka Nchi 14 zinazoshiriki Mkutano  huo ambazo ni Comoro, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Uganda na  wenyeji Tanzania.

 

Akizungumza mara baada ya Tanzania kuchaguliwa, Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewashukuru Wajumbe hao akiwahakikishia kuwa Tanzania itakua tayari kusimamia, kuendeleza na kuhakikisha mipango na matarajio ya Baraza hilo yanafikiwa kwa mafanikio makubwa.

 

Mkutano unaofuata wa Baraza hilo utafanyika Zanzibar Aprili, 2024.


WCB KUPAMBA KILELE CHA TULIA TRUST MARATHON 2023


Wasanii kutoka kundi la WCB wakiongozwa na Nasib Abdul maarufu kama Dimond Plutnamz kesho wanaungana na wasanii wengine katika kuyapamaba mashindano ya mbio ya Tulia Marathon 2023 ambayo yaliyoanza jana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano cha Tulia Trust ,Joshua Mwakanolo wasanii wengine watakaoongozana na Dimond kutoka WCB ni Raymond Mwakyusa(Rayvan), Zuhura Othman Soud(Zuchu) na Mbwana Yusuph Kilungi(Mbosso)

Tuesday, April 18, 2023

SPIKA DKT. TULIA AICHANGIA MBEYA CITY MILIONI MBILI, WABUNGE NAO WAMUUNGA MKONO




Na Mwandishi wetu, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa kiasi cha Shingi Milioni mbili kwa timu ya Mbeya City ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Fedha hiyo imetolewa Aprili 18, 2023 wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Spika kwa wachezaji wa Mbeya City Jijini Dodoma wakiwa safarini kuelekea Bukoba kwenye Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa tarehe 23/04/2023
Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Mhe. Spika wa Bunge, Mbunge wa Jimbo la Lupa Chunya kwa kushirikiana na wabunge wa Mbeya nao wametoa kiasi cha Shilingi milioni moja kama sehemu ya motisha kwa wachezaji
Kiasi kilichotolewa na Spika pamoja na wabunge wa Mbeya kinafikisha jumla ya Shilingi milioni tatu.
Pamoja na mambo mengine, Wabunge hao wameahidi kununua ushindi kwa timu ya Mbeya City kwa kila mechi zilizosalia kwenye ligi Kuu ya Tanzania inayoendelea.

Wednesday, March 22, 2023

Daraja la Bilioni moja lapeleka ligi daraja la nne Mwansanga na Tembela

 Na Mwandishi wetu,Mbeya.

 

UJENZI wa daraja la Mwansanga uliogharimu zaidi ya Shilingi bilioni 1.3 umeanza kuleta neena kwa wakazi wa Kata za Mwansanga na Tembela baada ya Chama cha soka Mbeya mjini(Mufa) kuamua kituo cha hatua ya awali ya Ligi daraja la nne kufanyikia kwenye kata hizo.

 

Madiwani wa Kata ya Tembela,Frank Mwasyoke na wa Kata ya Mwansanga, Jelly Wokola walisema kujengwa daraja na barabara kumeanza kufungua milango kwenye maeneo yao na sasa wana imani wananchi wao wataanza kuneemeka na fursa kama ilivyokuwa kwa wakazi wa maeneo mengine.

 

“Naamini chama cha mpira kimependekeza uwanja huu ni baada ya juhudi za serikali kujenga daraja kubwa na la kisasa maana awali maeneo haya yalikuwa hayafikiki lakini sasa hivi kufika hapa Tembela na Mwansanga limekuwa jambo jepesi sana.”

 

“Tunamshukuru rais Samia kwa kutujengea daraja na pia mbunge wetu Dk Tulia kwa kuwa karibu nasi kunanikisha hili la ujenzi wa daraja. Na kwa chama cha mpira kuleta haya mashindano ni kuunga mkono juhudi za serikali.” Alisema Mwasyoke.

 

Diwani huyo alizitaja faida zitakazopatikana kwa kata hizo kupelekewa mashindano ya ligi daraja la nne kuwa ni pamoja na vijana kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao na pia yatafungua njia za kiuchumi kwa wakazi kufanya biashara kwakuwa yanavuta watu wengi.

 

Kwa upande wake Wokola aliwasihi wadau wa mchezo wa soka mkoani hapa wakiwemo viongozi wa timu za Tanzania Prisons,Mbeya City na Ihefu FC kufika kwenye michezo ya mashindano hayo ili kuvumbua vipaji vipya vya vijana wanaoweza kuwasjiri.

 

“Tumefurahi kwamba uwanja huu lazima utatoa vijana wenye vipaji. Tunao vijana wengi  kwenye maeneo yetu..wanakuwa wachezaji wazuri lakini hawaonekani..sasa kupitia mashindano haya na sisi tunaweza kupata vijana wanaokwenda kuchezea Mbeya City.”

 

Mwenyekiti wa Mufa,John Gondwe alisema ni kwa miaka mingi Kata hizo mbili zilikuwa hazipati fursa ya kushiriki mashindano ya ligi ya wilaya kutokana na changamoto ya usafiri hususani kutokuwepo kwa daraja.

 

“Baada ya serikali kwa kushirikiana na mbunge kuweka daraja tukaona huku sasa kumefunguka.. na tukaona na wenyewe tuwaletee hii fursa ya michezo.Walikosa burudani ya michezo kwa muda mrefu.Tunaona mwitikio ni mkubwa kama unavyoona kuna watu wanafanya pia biashara hapa uwanjani.” Alisema Gondwe.

 

“Ni wakati kwa wadau wengine wa michezo waje kutuunga mkono ili tuwezeshe maeneo haya yachangamke kama ilivyo kwa maeneo mengine ya jiji letu.” Aliongeza.

 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo timu zinazoshiriki ligi hiyo ni pamoja na Mbogo Mwansanga,Ilemi FC,Ilembo FC,Leopard FC zilizopo Kundi A, huku Kundi B zikiwa ni Mpaju FC,Sido FC,Ilemi FC na Icon FC.