Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, February 26, 2013

Je unakumbuka Kibanga ampiga mkoloni,Siku ya gulio Katerelo,Chilunda apambana na chui,Ndoto za kimweri,Pamela na kipini,Watoto wageuka mawe,Sizitaki mbichi hizi,Brown ashika tama,Lindu amuokoa kapilima,Pepe huna masikio,Sisimizi shujaa,Tembo na chura,Chopeko na mnofu,Tola mla gizani,Tumbo niache nimwachie manenge uji

TAFAKARI MWENENDO WAKO KATIKA KIPINDI HIKI CHA KWARESMA KWA WAKRISTO KUELEKEA UFUFUO WA BWANA YESU

WIZI KWA ATM WAIBUKIA MBEYA

WATU wane wanashikiliwa na polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya kukutwa wakiiba fedha benki kupitia kadi za mashine za ATM. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa mkuu wa wilaya Chrispin Meela amesema wanaoshikiliwa ni pamoja na mhitimu wa kidato cha nne mwaka jana katika moja ya shule za sekondari za wilayani Bunda mkoani Mara Joseph Peter(20) anaeishi kwa sasa Msasani Tukuyu wilayani Rungwe. Amewataja wengine kuwa ni mfanyabiashara Juma Kabelo(28) mkazi wa Tukuyu,Jumanne Magele(29) mkazi katika mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi na Miraji Ketahe(34) mkazi wa Msasani wilayani Rungwe. Mkuu huyo wa wilaya amesema mnamo majira ya saa 2:00 usiku Februari 25 alipigiwa simu na raia mwema na kuambiwa juu ya uwepo wa watu waliokuwa wakitoa fedha mfululizo katika ATM ya benki ya NMB tawi la Tukuyu na ndipo akamuagiza mkuu wa polisi wilayani hapa kutuma makachero eneo hilo. Baada ya makachero hao kufika waliwakuta watuhumiwa wakiendelea kutoa fedha na baada ya kuwakamata wakakuta tayari wamekwishatoa shilingi milioni 20.5 huku wakiwa pia na kadi bandia 150 za ATM zilizoonekana kuwa za wateja tofauti. TAFADHALI ONA AIBU KUCOPY STORY HII.

UWEKEZAJI WA USAGAJI KOKOTO UYOLE JIJINI MBEYA

Monday, February 25, 2013

MTANDAO WA UJAMBAZI MBEYA,IRINGA,MOROGORO,DAR HUU HAPA

POLISI mkoani Mbeya kwa kushirikiana na polisi mkoani Iringa wamegundua mtandao wa majambazi Sugu ambao umekuwa ukihusika na matukio ya mauaji na unyang’aji wa kutumia silaha. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athumani amesem leo(Feb 25) kuwa watu 13 wakiwemo askari wawili wanashikiliwa huku wengine 16 wakiendelea kufanyiwa uchunguzi na jeshi hilo. Kamanda Athumani aliwataja askari waliokamatwa kuhusika na mtandao huo kuwa ni MT 85393 Samwel Balumwina(31) wa kikosi cha 844 KJ cha Jeshi la kujenga Taifa(JKT) Mbeya na polisi G 9101 PC Samwel Kigunye(27) wa kikosi cha kutuliza ghasia(FFU) Mbeya. Alisema askari hao wamekuwa wakihusika na mtandao wa ujambazi kwa kuazimisha sare za polisi na jeshi la wananchi(JWTZ) kwa wenzao wanaokwenda katika matukio ya uvamizi na kusisitiza kuwa watashitakiwa kijeshi. Wengine wanaoshikiliwa ni wanafamilia watatu wote wakazi wa makambako Japhet Ng’ang’ana(24) aliyekuwa mtunza silaha,Claud Ng’ang’ana(36) na mfanyabiashara Hilary Ng’ang’ana(30). Aliwataja wengine kuwa ni Mkazi wa Dar es salaam Rajab Mwinyi(Wakongowe)(25),mkazi wa Sabasaba jijini Mbeya Gregory Mtega(Chambo au Stanley)(25),mkazi wa Tunduma wilayani Momba Francis Sanga(Masalala)(30) aliyekuwa akinunua mali za wizi na mkazi wa Mwanjelwa Gati Mbilinyi ambaye alikuwa akitumia sare za JWTZ katika matukio ya uharifu. Kamanda huyo alisema watuhumiwa hao wote wanaonekana kuhusika na tukio la mauaji ya watu wawili waliotekwa wakati wakitokea dar es salaam kwenda Mbeya kisha kuuawa kwa kupigwa risasi na miili yao kutupwa porini na baadaye kupatikana ikiwa imeoza na kubakia mifupa mitupu maeneo ya Mafinga. Aliwataja watu hao ambao waliuawa Februari 2 mwaka huu na mali waliyokuwa wakisafirisha kuporwa kuwa ni Festo Kyando(45) aliyekuwa dereva na mmiliki wa gari namba T 586AGX Mitsubish Fuso lililokuwa na mzigo wa bidhaa mbalimbali ikiwemo vifaa vya ujenzi pamoja na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Jamali aliyekuwa utingo. Kamanda Athuman aliwataja wanaoshikiliwa kutokana na mauaji ya askari polisi G.68 PC Jafari Karume Mohamed(30) wa kituo kidogo cha polisi cha Mkwajuni wilayani Chunya katika majibizano ya risasi katika ya majambazi watano na polisi ambapo pia jambazi Shaban Msule(33) mkazi wa Makambako aliuawa. Watuhumiwa hao ni Manase Kibona(Masai)(37) mkazi wa Tunduma na Dar es salaam aliyehusika pia na uporaji katika makazi ya watawa wa kike wa kikatoliki(Masista) huko Wanging’ombe,Mashaka George(27) dereva wa bodaboda aliyekamatwa akiwa amewapakia baadhi ya majambazi katika kijiji cha Kanga wilayani Chunya,Mkazi wa Chimala wilayani Mbarali John Mahenge(39) na Narasco Mabiki(32) mkazi wa Chimala. Alisema pamoja na watuhumiwa hao 13 pia zimekamatwa silaha mbalimbali ikiwamo Bunduki Short Gun moja,bastola tatu,gobore moja,risasi 155 za aina mbalimbali za bunduki,magari manne mali ya watuhumiwa wa mtandao huo na sare nne za JWTZ. Alisema mtandao huo umekuwa ukifanya matukio ya unyang'anyi wa mali na mauaji katika mikoa ya Mbeya,Iringa na Morogogo katika maeneo ambayo yamekuwa yakitajwa kushamiri kwa utekaji magari.

MATUKIO KATIKA PICHA

Thursday, February 21, 2013

MBEYA MARUFUKU KUUZA KANDA,CD,DVD ZINAZOCHOCHEA MGOGORO WA KIDINI

Na Joachim Nyambo,Mbeya. SERIKALI mkoani Mbeya imeonya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakaehusika kwa aina yoyote kueneza kaulizi zenye uchochezi wa migogoro ya kidini. Hayo yamebainishwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya Dk.Norman Sigalla katika kikao chake na waandishi wa habari yakiwa ni matokea ya majadiliano ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi leo(Feb 21). Sigalla amesema kuanzia sasa serikali mkoani hapa haitaruhusu mahubiri yanayolenga uchochezi katika makanisa wala misikiti na kuonya viongozi wa dini na wanasiasa wanaoitumia migogoro kama njia ya kupata umaarufu. Amesema amri hiyo inakwenda sambamba na kuzuia kudurufu ama kusambaza mikanda na CD zenye jumbe zinazochochea migogoro ya kidini na kusema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakamata wamiliki wa maduka yaliyo na bidhaa hizo. Amewataka watu wote walio na bidhaa hizo kuzisalimisha mikononi mwa vyombo vya sheria na kwa raia wema kutoa taarifa juu ya uwepo wa bidhaa hizo katika maeneo yao.

Monday, February 18, 2013

SHAMRASHAMRA BAADA YA MBEYA CITY KUTINGA LIGI KUU TANZANIA BARA

BREAKING NEWWWWZ

YULE MAMA ALIYEMLISHA KINYESI MTOTO NA KUMCHOMA NA MOTO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA MUDA HUU! MBEYA YETU IMESHUHUDIA MUDA HUU HUKUMU YA YULE MAMA AMBAYE ALIKUWA NA KESI YA KUMLISHA KINYESI MTOTO NA KUMCHOMA NA MOTO MKONONI NA KUSABABISHA AKATWE MKONO HUO, AMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.

Wednesday, February 13, 2013

MACHINGA AKAMATWA NA KIGANJA CHA BINADAMU

POLISI mkoani Mbeya wanamshikilia mfanyabiashara mkazi wa eneo la Ilolo jijini hapa Baraka Kibona(30) kwa kukutwa na kiganja cha mkono wa binadamu nyumbani kwake. Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa nyumbani kwake Februari 12 saa 5:00 asubuhi na kutaja kiganja kilichokamatwa kuwa ni cha mkono wa kulia wa binadamu. Masaki amesema kiganja hicho ambacho hakijafahamika ni cha nani kimekutwa chumbani kwa mtuhumiwa kikiwa kimeviringishwa kamba na kisha kuhifadhiwa katika boksi. Kwa mujibu wa kaimu kamanda huyo mtuhumiwa amekiri kumiliki kiganja hicho alichosema alipewa na mganga wa jadi ili kimsaidie kujikinga ama kujilinda katika biashara zake za umachinga zisichukuliwe kwa njia za kishirikina ikiwa ni sambamba na fedha zake. Msaki amesema jeshi hilo linaendelea na taratibu za kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani na kujibu tuhuma zinazo mkabili na kuitaka jamii mkoani hapa hususani inayojishughulisha na masuala ya biashara kuachana na imani za kishirikina.

Monday, February 11, 2013

MREFA YATANGAZA WAJUMBE WA KAMATI ZAKE

CHAMA cha soka mkoani Mbeya(MREFA) kimeteua wajumbe wa kamati mbalimbali ikiwemo kamati ya Habari,Uenezi na Mawasiliano inayohusisha pia waandishi wa habari akiwamo mkurugenzi mtendaji wa Blogu ya Lyamba Lya Mfipa.
Mwenyekiti wa MREFA Elias Mwanjala alitaja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni Lwitiko Mwamundela atakayekuwa mwenyekiti,Blandy Nelson ambaye ni katibu na wajumbe ni Joachim Nyambo,Charles Mwakipesile na Saleh Kupaza, Kwa upande wa kamati ya Uchumi Fedha na Mipango mwenyekiti ameteuliwa Omary Mahinya,Emanuel Kavenga ni katibu na wajumbe ni Teddy Karua,Fidelis Mwampoma,Agustino Sanga,Ayasi Njalambaha na Ambakisye Minga. Kamati ya Ufundi,Vijana na Maendeleo ya wanawake mwenyekiti ni Willium Mwamlima,katibu ni Elizabeth Kalinga na wajumbe ni Juma Mwambusi,Alex Lusekelo na Lucas Kasmiri wakati kamati ya waamuzi mwenyekiti ni Sadiki Jumbe,katibu ni John Kanyenye,wajumbe ni Paul Mwanjabike,Mwanahamis Muya na Albert Mwakasege. Kamati ya Mashindano Juma Kila ni mwenyekiti,katibu ni Dickson Sinkwembe,wajumbe ni Joel Kasebele na Omary Upuu,kamati ya Uchaguzi mwenyekiti Basilius Namkambe anaendelea na nafasi yake na wajumbe ni Shaaban Robert,Bakari Mketo na Daud Malimali. Mwanjala alisema balaza la wadhamini wajumbe wake ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapundizi(CCM) wilayani Kyela Dk.Hunter Mwakifuna,mkuu wa wilaya ya Rungwe Chrispin Meela,Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali Adam Mgori,mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya dk Ernest Kihanga na mfanyabiashara Thom Mwang’onda. “Kamati ya utendaji kwa kuzingatia majukumu iliyo nayo imeunda pia kamati ya masoko ambayo itakuwa na wajumbe Francis Mwasamwene,Gabriel Shawa na Claud Chawene kutoka kampuni ya bia ya TBL,David Bulegi na Priscar Kalinga kutoka kampuni ya Saruji ya Mbeya Cement na Uzia Mgala wa kampuni ya simu ya Vodacom”

Sunday, February 10, 2013

WAPELEKWA SEKONDARI KUJAZA VYUMBA

ASILIMIA 70 ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari mwaka huu wilayani Mbozi mkoani Mbeya hawana sifa za stahili za kujiunga na kidato cha kwanza. Asilimia hiyo ni ya wanafunzi 2,276 walioteuliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za wilayani hapa kati yao wakiwamo wasichana 1,143 na wavulana 1,133. Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk.Michael Kadege aliyasema hayo katika kikao cha balaza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo na kuwataka madiwani na wadau wengine kuangalia ni namna gani wanaweza wakainusuru elimu wilayani kwao. Dk.Kadege alisema Utafiti uliofanywa umebaini kuwa kati ya wanafunzi hao waliochaguliwa hawakupata alama za ufaulu za A,B na C badala yake ililazimu kuchukua kuanzia waliopata alama D hadi F ili kupata wanafunzi wa kujaza mvyumba katika shule za sekondari.

WATATU WATIMULIWA KAZI MBOZI

HALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya imewafukuza kazi watumishi wake watatu na kutoa onyo kwa wengine kadhaa kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za utumishi wa umma. Adhabu hiyo ilitolewa kwa watumishi hao baada ya kikao cha balaza la madiwani kulazimika kujigeuza na kuwa kamati kisha kujadili tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinawakabili baadhi ya watumishi wengi wao wakiwa ni maofisa watendaji wa vijiji na kata. Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elick Ambakisye aliwataja waliofukuzwa kazi kuwa ni pamoja na mkaguzi msaidizi Adela Shayo ambaye hajafika katika kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi sita pasipo mwajiri wake kuwa na taarifa yoyote. Ambakisye aliwataja wengine kuwa ni ofisa mtendaji wa kijiji cha Kilimapimbi kata ya Isandula Joseph Mwashilindi na Abel Kandonga wa kijiji cha Senga ambao pamoja na makosa mengine pia walikuwa hawasomi mapato na matumizi ya vijiji vyao. Mwenyekiti huyo pia alisema halmashauri imeamuru kuwaandikia barua za onyo maofisa watendaji wengine 21 pamoja na barua za pongezi kwa maofisa watendaji wawili walioonekana kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.

Thursday, February 7, 2013

TALAKA (4)- JINSI YA KUPELEKA SHAURI LA KUVUNJA NDOA AU KUTENGANA MAHAKAMANI

Kabla shauri hilo halijapelekwa mahakamani,ni lazima lipitie kwenye balaza la usuluhishi la ndoa linalotambuliwa kisheria.Mwanandoa anayetaka kufanya hivyo anaweza kupeleka shauri hilo katika balaza la usuluhishi la ndoa ambalo linaweza kuwa la kidini au balaza la usuluhishi la ndoa la kata.Balaza linatakiwa kuwasikiliza au kuwasuluhisha wanandoa.Endapo balaza litashindwa kuwasuluhisha,litatoa taarifa/hati itakayowasilishwa mahakamani juu ya kushindwa huko ili mahakama iendelee kuamua itakavyoona inafaa.Hata hivyo sharti la kupeleka shauri la ndoa kwenye balaza la usuluhishi linaweza kuepukwa endapo tu itathibitika kuwa zipo sababu za msingi za kufanya hivyo.ITAENDELEA KESHO..........

AUAWA AKITOKA KWENYE MKUTANO WA KIJIJI

MNAMO TAREHE 06.01.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SENGA – KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA . HAMISI S/O LINGSON MATOKA,MIAKA 40,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA KITONGOJI CHA MING’ONGO KIJIJI CHA SENGA ALIKUTWA PORINI AKIWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA . MAREHEMU AMBAYE ALIKUTWA NA JERAHA KUBWA KICHWANI ALIKUWA ANARUDI NYUMBANI KWAKE AKITOKEA MAKAO MAKUU YA KIJIJI CHA SENGA KWENYE MKUTANO WA KAWAIDA WA MAENDELEO YA KIJIJI . MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA NJIANI NA KUMPIGA HADI KUFA . CHANZO KINACHUNGUZWA .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE WATATUE MATATIZO YAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

Wednesday, February 6, 2013

KESI YA MWANAMKE ALIYEMLISHA MTOTO KINYESI JIJINI MBEYA NI KESHO.BAADHI YA WADAU WANATARAJI KESHO IWAPO HAKIMU HATOTOA HUKUMU BASI ANAWEZA KUTAJA TAREHE YA HUKUMU

POLISI,JAMBAZI WAUANA KWA RISASI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 06. 02.2013. WILAYA YA CHUNYA – ASKARI POLISI MMOJA AUAWA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI NA MAJAMBAZI MNAMO TAREHE 06.02.2013 MAJIRA SAA 00:30HRS HUKO KATIKA HOSPITALI YA MWAMBANI – MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED MIAKA 30,MUHA WA KITUO CHA POLISI MKWAJUNI ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO . CHANZO CHA TUKIO NI MAJAMBAZI WANNE WAKIWA NA SILAHA IDHANIWAYO KUWA AINA YA SMG WALIVAMIA KITUO CHA MAFUTA KILICHOPO KIJIJI CHA MATUNDASI MALI YA SAMORA S/O MUYOMBE NA KUPORA PESA TSHS 2,200,000/= WAKITUMIA GARI T.227 BST AINA YA TOYOTA COROLA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA SHABAN S/O MSULE,MIAKA 33,MBENA MKAZI WA MAKAMBAKO .MAREHEMU AKIWA DORIA NA ASKARI WENZAKE WALIFUATILIA TUKIO HILO NA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI ASKARI HUYO ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI UBAVU WA KULIA NA KUKIMBIZWA HOSPITALINI KWA MATIBABU ZAIDI . KATIKA TUKIO HILO JAMBAZI SHABAN S/O MSULE ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI .GARI LILILOTUMIKA KATIKA TUKIO HILO LIMEKAMATWA NA MAGANDA 9 YA RISASI AINA YA SMG/SAR NA RISASI 6 ZIMEOKOTWA ENEO LA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU ASKARI G.68 PC JAFARI KARUME MOHAMED UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO .MSAKO MKALI UNAENDELEA CHINI YA UONGOZI WA RCO MBEYA ROBERT MAYALA – SSP, ASKARI POLISI NA WANANCHI ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA MTU/WATU WENYE TAARIFA JUU YA MAHALI WALIPO WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE , VINGINEVYO WAJISALIMISHE MARA MOJA. [ BARAKAEL MASAKI – SSP ] KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Tuesday, February 5, 2013

TALAKA (3)

MAMBO YA MUHIMU KUZINGATIWA KABLA YA KUTOA TALAKA...... Kwa kawaida mahakama hutoa talaka inapothibitika kwamba ndoa hiyo imevunjika kiasi cha kutokurekebishika tena kwa kuangalia mambo au vigezo vifuatavyo (a)Ikiwa mmoja wa wanandoa hao atathibitika kufanya uzinzi(Ugoni) (b)Ikiwa mmoja wa wanandoa hao alithibitika kumfanyia ukatili wa kimwili au kiakili mwanandoa mwenzake au watoto wao (c)Iwapo itathibitika kuwa mmoja wa wanandoa hao amemtelekeza mwenzake na kwenda kuishi mbali au kumtelekeza akiwa ndani ya nyumba(Kwa kuhama chumba,kitanda au kuishi nyumba ya pili kati ya wanazomiliki bila ridhaa/idhini ya mwenza wake) (d)Uasi au utoro (e)Kutelekeza kwa makusudi (f) kutengana kwa hiari au kwa amri ya mahakama kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu (g)Kifungo kisichopungua miaka mitano au cha maisha (h)Kichaa kisichotibika kilichothibitishwa na madaktari bingwa wa akili wasiopungua wawili (i)Tofauti ya itikadi za kidini au siasa ITAENDELEA KESHO.................

BREAKING NEWZZZZZZZZZZ

HABARI TULIZOPATA HIVI PUNDE NI KUWA ASKARI WA JESHI LA POLISI ANADAIWA KUUAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI KATI YA ASKARI WA JESHI HILO NA MAJAMBAZI WALIOTAKA KUVAMIA DUKA MOJA MKWAJUNI WILAYANI CHUNYA MKOANI MBEYA.KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUWA NASI.......................

WATANO WAUAWA KWA RADI

WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa kupigwa radi katika matukio matatu tofauti likiwemo lililoua ndugu watatu wa familia moja. Wanandugu hao watatu wakazi wa kata ya Nyimbili wilayani Mbozi wamefikwa na mauti Februari 5 mwaka huu majira ya saa saba mchana wakati mvua kubwa iliyoambatana na radi za mara kwa mara ikiendelea kunyesha wakiwa nyumbani. Afisa mtendaji wa kata ya Nyimbili Lingtone Nzowa amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Jerumana Halinga(35),David Halinga(5) na Kumi Halinga(3) ambapo pia radi hiyo imemjeruhi mtoto wa miezi tisa ambaye jina lake halikufahamika mara moja. Tukio la pili limetokea katika kijiji cha Magurula kata ya Utengule Usangu Wilayani Mbarali ambapo radi iliyotokana na mvua kubwa imempiga Kasim Sagutangu na kusababisha kifo chake ambapo diwani wa kata hiyo Juntwa Mwalyaje amesema mvua hiyo imenyesha Februari 3 majira ya saa nane za mchana. Tukio la tatu limetokea februari 3 katika kijiji cha Mbagala Kata ya Ilembo wilayani Mbeya ambapo mwanamke Kotanida Petro amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akiwa shambani kwake. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio hayo ya vifo vya watu watano vilivyotokana na radi.