Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, February 26, 2013

WIZI KWA ATM WAIBUKIA MBEYA

WATU wane wanashikiliwa na polisi wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya kukutwa wakiiba fedha benki kupitia kadi za mashine za ATM. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa mkuu wa wilaya Chrispin Meela amesema wanaoshikiliwa ni pamoja na mhitimu wa kidato cha nne mwaka jana katika moja ya shule za sekondari za wilayani Bunda mkoani Mara Joseph Peter(20) anaeishi kwa sasa Msasani Tukuyu wilayani Rungwe. Amewataja wengine kuwa ni mfanyabiashara Juma Kabelo(28) mkazi wa Tukuyu,Jumanne Magele(29) mkazi katika mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi na Miraji Ketahe(34) mkazi wa Msasani wilayani Rungwe. Mkuu huyo wa wilaya amesema mnamo majira ya saa 2:00 usiku Februari 25 alipigiwa simu na raia mwema na kuambiwa juu ya uwepo wa watu waliokuwa wakitoa fedha mfululizo katika ATM ya benki ya NMB tawi la Tukuyu na ndipo akamuagiza mkuu wa polisi wilayani hapa kutuma makachero eneo hilo. Baada ya makachero hao kufika waliwakuta watuhumiwa wakiendelea kutoa fedha na baada ya kuwakamata wakakuta tayari wamekwishatoa shilingi milioni 20.5 huku wakiwa pia na kadi bandia 150 za ATM zilizoonekana kuwa za wateja tofauti. TAFADHALI ONA AIBU KUCOPY STORY HII.

No comments:

Post a Comment