Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Wednesday, February 13, 2013

MACHINGA AKAMATWA NA KIGANJA CHA BINADAMU

POLISI mkoani Mbeya wanamshikilia mfanyabiashara mkazi wa eneo la Ilolo jijini hapa Baraka Kibona(30) kwa kukutwa na kiganja cha mkono wa binadamu nyumbani kwake. Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki amesema kuwa mtuhumiwa amekamatwa nyumbani kwake Februari 12 saa 5:00 asubuhi na kutaja kiganja kilichokamatwa kuwa ni cha mkono wa kulia wa binadamu. Masaki amesema kiganja hicho ambacho hakijafahamika ni cha nani kimekutwa chumbani kwa mtuhumiwa kikiwa kimeviringishwa kamba na kisha kuhifadhiwa katika boksi. Kwa mujibu wa kaimu kamanda huyo mtuhumiwa amekiri kumiliki kiganja hicho alichosema alipewa na mganga wa jadi ili kimsaidie kujikinga ama kujilinda katika biashara zake za umachinga zisichukuliwe kwa njia za kishirikina ikiwa ni sambamba na fedha zake. Msaki amesema jeshi hilo linaendelea na taratibu za kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani na kujibu tuhuma zinazo mkabili na kuitaka jamii mkoani hapa hususani inayojishughulisha na masuala ya biashara kuachana na imani za kishirikina.

No comments:

Post a Comment