Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, February 21, 2013

MBEYA MARUFUKU KUUZA KANDA,CD,DVD ZINAZOCHOCHEA MGOGORO WA KIDINI

Na Joachim Nyambo,Mbeya. SERIKALI mkoani Mbeya imeonya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakaehusika kwa aina yoyote kueneza kaulizi zenye uchochezi wa migogoro ya kidini. Hayo yamebainishwa na kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya Dk.Norman Sigalla katika kikao chake na waandishi wa habari yakiwa ni matokea ya majadiliano ya kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kilichoketi leo(Feb 21). Sigalla amesema kuanzia sasa serikali mkoani hapa haitaruhusu mahubiri yanayolenga uchochezi katika makanisa wala misikiti na kuonya viongozi wa dini na wanasiasa wanaoitumia migogoro kama njia ya kupata umaarufu. Amesema amri hiyo inakwenda sambamba na kuzuia kudurufu ama kusambaza mikanda na CD zenye jumbe zinazochochea migogoro ya kidini na kusema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwakamata wamiliki wa maduka yaliyo na bidhaa hizo. Amewataka watu wote walio na bidhaa hizo kuzisalimisha mikononi mwa vyombo vya sheria na kwa raia wema kutoa taarifa juu ya uwepo wa bidhaa hizo katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment