Sunday, February 10, 2013
WATATU WATIMULIWA KAZI MBOZI
HALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya imewafukuza kazi watumishi
wake watatu na kutoa onyo kwa wengine kadhaa kutokana na makosa
mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za utumishi wa umma.
Adhabu hiyo ilitolewa kwa watumishi hao baada ya kikao cha balaza la
madiwani kulazimika kujigeuza na kuwa kamati kisha kujadili tuhuma
mbalimbali zilizokuwa zinawakabili baadhi ya watumishi wengi wao
wakiwa ni maofisa watendaji wa vijiji na kata.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elick Ambakisye aliwataja waliofukuzwa
kazi kuwa ni pamoja na mkaguzi msaidizi Adela Shayo ambaye hajafika
katika kituo chake cha kazi kwa zaidi ya miezi sita pasipo mwajiri
wake kuwa na taarifa yoyote.
Ambakisye aliwataja wengine kuwa ni ofisa mtendaji wa kijiji cha
Kilimapimbi kata ya Isandula Joseph Mwashilindi na Abel Kandonga wa
kijiji cha Senga ambao pamoja na makosa mengine pia walikuwa hawasomi
mapato na matumizi ya vijiji vyao.
Mwenyekiti huyo pia alisema halmashauri imeamuru kuwaandikia barua za
onyo maofisa watendaji wengine 21 pamoja na barua za pongezi kwa
maofisa watendaji wawili walioonekana kufanya shughuli zao kwa ufanisi
mkubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment