Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, March 3, 2018

WAKOREA WEUSI SITA MBARONI








JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA


 
                                                                                                              Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                   Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    
Namba ya simu 2502572                                                                                                S. L. P. 260,
Fax - +255252503734                                                                                                         MBEYA.
              tanpol.mbeya@gmail.com
                                                       
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 03.03.2018.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao. Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kukamata watuhumiwa mbalimbali wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu @ wakorea.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA UHALIFU @ WAKOREA.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya Operesheni maalum pamoja na misako katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya. Operesheni hii ililenga kukamata wahalifu mbalimbali likiwemo kundi la vijana wanaojiita Wakorea ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uhalifu na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Operesheni hii imefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambayo ni Ivumwe, Mwakibete, Mwambene, Mama John, Ilomba, Mafiati, Makunguru, Iyela na Isyesye.

Katika Operesheni hii maalum, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita [06] kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-

1.     KELVIN RAPHAEL [22] Mwakibete Bomba mbili ambaye ndiye kiongozi wa kundi hili la uhalifu @ Wakorea.
2.     CLEMENCE CHRISTOPHER @ MWAKALINGA [23] Mkazi wa Mwakibete Viwandani.
3.     CHARLES MWASUMBI [21] Mkazi wa Mwakibete
4.     EDGA EDWARD [20] Makondeko Mwakibete
5.     IPYANS NDUNGURU [21] Mkazi wa Mwakibete
6.     ADEN MWALUKASA [35] Mkazi wa Mwakibete



Pia katika Operesheni hii maalum ya kuwasaka vijana wanaojihusisha na uhalifu hapa Jijini Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana watatu [03] kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji nyakati za usiku na mchana. Watuhumiwa hao wamefahamika kwa majina ya:-

1.     GODFREY JOSEPH @ MHENGA [20] Mkazi wa Ilemi Mapelele
2.     GODFREY PAUL @ MWAKASAJE [39] Mkazi wa Ilemi Mapelele
3.     MTEMI YAHAYA @ MWASANGA [42] Mkazi wa Uyole

Watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kupekuliwa walikutwa na vifaa mbalimbali walivyokuwa wakivitumia kuvunjia ambavyo ni:-
1.     Bisibisi – 03
2.     Nyundo – 01
3.     Mkasi – 01

 Aidha watuhumiwa hao walikutwa na mali mbalimbali za wizi:-
1.     Flat Screen aina ya Home base
2.     Flat Screen aina ya Samsung
3.     TV ya kawaida aina ya Home base
4.     Sub Woofer 01
5.     Deck 03 aina ya Singsung 02 na Fusion 01.

Aidha mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa nane [08] kutokana na kujihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mbeya ambao walifikishwa Mahakamani na kwa sasa wanatumikia vifungo vya nje.

Pia watuhumiwa kumi na mbili [12] ambao walikamatwa hivi karibuni katika Operesheni/Misako iliyofanyika huko katika maeneo ya Ilemi, Juhudi, Makunguru na Mwenge hapa Jijini Mbeya ambao kesi zao zinaendelea katika Mahakama ya Mwanzo Iyunga

Watuhumiwa wengine watafikishwa Mahakamani mara tu baada ya Upelelezi kukamilika.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa vijana na jamii kwa ujumla kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajishughulishe na kazi halali kwa ajili ya kujipati kipato. Aidha anatoa onyo kali wafanyabiashara ya vilezi kufuata sheria na taratibu za biashara yao ikiwa ni pamoja na kufungua na kufunga sehemu zao za biashara muda sahihi kwa mujibu wa sheria.

             Imesainiwa na:    
[MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA