Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, January 29, 2018

TANGAZO TANGAZO TANGAZO!

MKURUGENZI wa Uchungaji wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Fr. Sirilo Mwalyoyo kupitia Kampuni ya LFCC Media anawatangazia Wakazi wa Jiji la Mbeya kujitokeza kujifunza muziki Mtakatifu.

Kwamujibu wa Mkurugenzi huyo, Masomo ya mziki Mtakatifu yatatolewa kuanzia Februari Mwaka huu katika madarasa ya Shule ya Msingi RuandaNzovwe iliyopo CCM Jijini Mbeya.

Alisema fani zitakazotolewa ni pamoja na kupiga kinanda, kusoma na kufundisha mziki (NOTA), kupiga ngoma, Kwaya masta, kutunga na kuandika nyimbo pamoja na kujifunza kuimba (Vocal).

Alisema sifaza kujiunga na Chuo hicho ni kwa mtu yeyote mwenye akili timamu anayejua kusoma na kuandika pa oja na kuwa na uaminifu na Imani.

Aliongeza kuwa muda wa masomo ni makubaliano baina ya Mwalimu na Mwanafunzi pia itategemea na wepesi wa mwanafunzi katika kushika na kuelewa vizuri masomo yake.

Alisema fomu za kujiunga zitapatiakana Shule ya Msingi RuandaNzovwe, Parokia ya Mtakatifu Yakobo Uyole, Parokia ya Roho Mtakatifu Ruanda, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima au Kanisa la Hija Mwanjelwa  na Kanisa kuu la Mtakatifu wa Antoni wa Padua mjini.

Alisema fomu za kujiunga zinapatikana kwenye vituo hivyo kwa shilingi 5000 kwa fomu moja kulingana na kozi anayotaka kusomea au kwa kuwasiliana na Mwalimu kupitia simu namba 0755 068195 au 0625760230.

Friday, January 26, 2018

Dkt Mwanjelwa kuzuru China





Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa anataraji kuzuru China mapema mwezi Mei ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya kuboresha mashirikiano kati ya Serikali hizo mbili yenye lengo la kuleta mapinduzi ya kweli kwenye Sekta ya Kilimo hususani kwenye masoko ya bidhaa za kilimo za Tanzania pamoja na eneo la kuwajengea uwezo Wakulima na Wataalamu wa Kilimo wa Tanzania.
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba ameyasema hayo mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo katika yake na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Dkt.Tizeba amesema China imeihakikishia Tanzania kuwa itaendelea kuboresha mazingira ya kilimo nchini kwa kuendelea kununua bidhaa za chakula za Tanzania ambazo ni pamoja na muhogo, nyuzi za pamba, kahawa, korosho na mbegu za mafuta.

Waziri Tizeba amesema China itaendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika eneo la utaalamu kwa kupitia programu maalumu ya kusomesha Wataalamu wa kilimo nchini lakini pia kusaidia vifaa vya kitaalamu katika eneo la utafiti na mafunzo kupitia Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na Kituo cha Cholima Dakawa vyote vya Mkoani Morogoro.

Waziri Tizeba ameongeza kuwa mara baada ya majadiliano hayo, timu ya Wataalamu imeundwa kutoka China na Tanzania ili kupitia maeneo ya kipaumbele kama walivyokubaliana na kwamba timu ya Wataalamu ya Tanzania ikiongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa itatembelea China mapema mwezi Mei kwa ajili ya kujiridhisha kuhusu mashirikiano hayo na baada ya hapo Serikali zote mbili zitasaini hati za makubaliano.

“Napenda kuwafahamisha Watanzania habari njema ya zao la muhogo kupewa kipaumbele na kuundiwa timu ya kimkakati na zaidi ya yote, Ndugu zetu Wachina wameonyesha nia ya kuisaidia Programu yetu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo ASDP II ambayo tutaizindua hivi karibuni” Amekaririwa Dkt, Tizeba.

Awali akizungumza mara baada ya mapokezi hayo katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alimuhakikishia Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli itaendeleza ushirikiano na serikali ya china ili kuongeza kasi na uwajibikaji na kuwa chachu ya maendeleo kwa watanzania.

Thursday, January 25, 2018

HARAKATI KUSAKA MAJI MBEYA

Wakazi wa Ituha jijini Mbeya wakihaha kusaka maji kutokana na changamoto ya maji inayolikabili eneo hilo.(Picha na Erasto Kikwala)

Monday, January 22, 2018

ZIARA YA MAAFISA UBALOZI WA MAREKANI MAKAO MAKUU YA TAJATI









UBALOZI wa Marekani nchini umeahidi kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) katika masuala mbalimbali ya kihabari ili kupanua wigo wa utendaji kazi baina ya pande hizo mbili.

Afisa habari kutoka ofisi ya Ubalozi huo,Bwana Benjamin Ellis amesema kati ya mambo yatakayoimarishwa ni pamoja na kusimamia na kutangaza miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani Kanda ya Nyanda za juu kusini.

Bw.Ellis ametoa ahadi hiyo jana alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi za TAJATI zilizopo jijini Mbeya kwa lengo la kujua shughuli zinazofanywa na Chama hicho na kujenga mahusiano kati ya kitengo cha Habari chini ya Ubalozi na Wanahabari wa Tajati.



Amesema amefarijika kufika katika ofisi za Tajati na kujionea shughuli mbalimbali ambazo Chama hicho kimezifanya ambazo zimechangia kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta za Utalii na Uwekezaji nchini.



Amesema atazungumza na uongozi wa Ubalozi ili kuhakikisha Miradi ambayo imefadhiriwa na Serikali ya Marekani na inayotekelezwa katika Mikoa ya ukanda wa Nyanda za juu kusini.



Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na iliyopo katika Sekta za afya, Elimu, Kilimo na kupambana na Uwindaji haramu dhidi ya wanyapori hivyo kutokana na shughuli za TAJATI ni vema ikashiriki moja kwa moja katika kufuatilia utekelezaji wake.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tajati,Venancy Matinya katika taarifa kwa ugeni huo amesema changamoto inayokikabili Chama hicho ni ukosefu wa vitendea kazi vitakavyowezesha kurahisisha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutembelea maeneo yenye fursa za Utalii na Uwekezaji.



Naye Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili amesema Mfumo wa utekelezaji wa majukumu ya chama hicho unatokana na kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja kwa kwenda kwenye eneo la tukio kama timu hivyo kinachohitajika ni uwezeshaji wa vitendea kazi.



Mwakilili amesema katika kazi zilizofanyika kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chama hicho zilikuwa za kujitolea kwa wanahabari wenyewe hata hivyo zimekuwa zikileta mafanikio   kwa jamii na Taifa kwa ujumla.



Awali Mkurugenzi wa Habari na mahusiano wa TAJATI, Felix Mwakyembe amezitaja baadhi ya kazi zilizofanywa na Chama hicho na kuleta mafanikio kuwa ni pamoja na kuandika habari kuhusu kuvamiwa kwa uwanja wa ndege wa zamani uliopo jijini Mbeya na kuandika kuhusu fursa za Uwekezaji na Utalii katika hifadhi ya wanyama Kitulo.

Saturday, January 20, 2018

THE MBONGOBONGO TOUR-MBEYA

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sisimba jijini Mbeya wakiwa wamejipanga kupokea ugeni wa The Mbongobongo uliowafikia shuleni kwao.
Fortunatus Kasomfi muasisi wa The Mbongobongo akizungumza na wanafunzi na kuwasimulia namna alivyokuwa wakati akisoma katika shule hiyo.





 Fortunatus Kasomfi akifanya yake masuala ya michezo mbalimbali huku  wanafunzi wakishuhudia.

 Ni mchezo wa kutafuna tishu kidogo then unatoa kamba ndeefu kutoka tumboni hakika mambo yalifana.The Mbongobongo ni kiboko yao.








 Fortunatus akawatengenezea wadogo zake biskuti na pipi kwa miujiza na kuwafurahisha zaidi.
 Zawadi ya mwisho ikawa ni kuwakabidhi Jezi na Mpira kwaajili ya timu ya shule.Ikumbukwe wakati akisoma hapa Kasomfi alikuwa Golikipa namba moja wa timu ya shule.


 Baada ya hapo Team The Mbongobongo ikahamia shule ya Sekondari Mbeya Day nako mambo yakawa matamu zaidi. Kwakuwa aliwahi pia kusoma katika shule hii,Kasomfi hakusita kuzungumza na wadogo zake yaani wanafunzi.





Kasomfi akikabidhi Mpira kwa kaka mkuu wa Shule ya Mbeya Day Sec kwaajili ya timu ya shule.

 Kasomfi akikabidhi Mpira dada mkuu wa shule kwaajili ya timu ya shule.

 Kasomfi akitoka kusalimiana na wanafunzi baada ya kumaliza kuzungumza nao.

 Mara Paaaaaa!!! akakutana na Mtoto wa Golikipa mahiri nchini Tanzania,Ivo Mapunda ambae enzi hizo waliwahi kucheza timu ya Shule na Kasomfi.






 Mmoja wa walimu waliokuwa shuleni hapo wakati Fortunatus akisoma na kuwa na mchango mkubwa kwake.


WATANZANIA wametakiwa kuwa na utamaduni wa kurudisha fadhila kwa jamii na taasisi zilizowawezesha kupata mafanikio katika Nyanja mbalimbali.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya day, Magreth Haule pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa zote za jijini Mbeya walitoa rai hiyo katika nyakati na sehemu tofauti walipokuwa wakipokea msaada wa Mipira na Jezi za timu za shule zao kutoka kwa mmoja wa watu waliowahi kusoma kwenye shule hizo,Fortunatus Kasomfi anayeishi nchini Afrika kusini.

Mwalimu Tindwa alisema ni watu wachache sana ambao huweza kukumbuka walikotoka ikiwemo mashuleni walikoandaliwa msingi bora wa maisha lakini akasema utamaduni wa kukumbuka nyuma ni muhimu sana.

“Ni watu wachache kuwakumbuka waliowasaidia kupata mafanikio na kuwatembelea ili kuwashukuru hivyo tunamshukuru huyu kijana kwani alihitimu hapa mwaka 1991 hivyo wengine waige mfano wake.Hapa anawajengea pia msingi mzuri wadogo zake aliowakuta leo hapa shuleni” alisema Mwalimu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya day, Magreth Haule alisema kama kila aliyepita katika shule hiyo akajitokeza kutoa ushuhuda wa mafanikio yake kutasaidia kuongeza hamasa kwa wanafunzi waliopo mashuleni.

Mwalimu Haule alisema wanafunzi wa siku hizi wamekuwa na tabia mbaya ikiwemo utoro na uchelewaji wa kufika Shule hivyo wahitimu waliofanikiwa wakitoa ushuhuda mbele yao kutasaidia kuwabadilisha.

Hata hivyo kwa pamoja Walimu hao walitoa wito kwa watanzania wenye mapenzi mema hususani waliosoma katika shule hizo kujitokeza kusaidia kutata changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa na walimu hao zinazoweza kupatiwa ufumbuzi kwa wadau mbalimbali waliosoma kurudi na kuwaunga mkono kwa kila mmoja alivyojaaliwa ni pamoja na uchakavu wa majengo kutokana na shule hizo kujengwa zamani ambapo Sisimba ilijengwa mwaka 1950 na Mbeya day sekondari ikijengwa mwaka 1962.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Fortunatus Kasomfi alisema baada ya kupata mafanikio katika shughuli zake nchini Afrika kusini amekumbuka chimbuko lake kuwa ni shule alizosoma.

Kasomfi alisema aliamua kupeleka zawadi ya vifaa vya michezo kwakuwa akiwa katika shule hizo alikuwa akizitumikia timu za shule akiwa Golikipa na kuziwezesha kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Alisema kwa kuanzia ameona atoe seti moja moja kwa kila shule sambamba na mpira ili wengine waweze kuguswa kwa kuchangia kutatua changamoto ya uchakavu wa majengo.

Mtanzania huyo aliongeza kuwa katika mafankio yake ambayo yametokana na msingi mzuri kutoka kwa Walimu wa Shule ya Msingi Sisimba na Sekondari ya Mbeya hivi sasa anajishughulisha na kazi za sanaa pamoja na ujasiliamali.