Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, January 20, 2018

THE MBONGOBONGO TOUR-MBEYA

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Sisimba jijini Mbeya wakiwa wamejipanga kupokea ugeni wa The Mbongobongo uliowafikia shuleni kwao.
Fortunatus Kasomfi muasisi wa The Mbongobongo akizungumza na wanafunzi na kuwasimulia namna alivyokuwa wakati akisoma katika shule hiyo.





 Fortunatus Kasomfi akifanya yake masuala ya michezo mbalimbali huku  wanafunzi wakishuhudia.

 Ni mchezo wa kutafuna tishu kidogo then unatoa kamba ndeefu kutoka tumboni hakika mambo yalifana.The Mbongobongo ni kiboko yao.








 Fortunatus akawatengenezea wadogo zake biskuti na pipi kwa miujiza na kuwafurahisha zaidi.
 Zawadi ya mwisho ikawa ni kuwakabidhi Jezi na Mpira kwaajili ya timu ya shule.Ikumbukwe wakati akisoma hapa Kasomfi alikuwa Golikipa namba moja wa timu ya shule.


 Baada ya hapo Team The Mbongobongo ikahamia shule ya Sekondari Mbeya Day nako mambo yakawa matamu zaidi. Kwakuwa aliwahi pia kusoma katika shule hii,Kasomfi hakusita kuzungumza na wadogo zake yaani wanafunzi.





Kasomfi akikabidhi Mpira kwa kaka mkuu wa Shule ya Mbeya Day Sec kwaajili ya timu ya shule.

 Kasomfi akikabidhi Mpira dada mkuu wa shule kwaajili ya timu ya shule.

 Kasomfi akitoka kusalimiana na wanafunzi baada ya kumaliza kuzungumza nao.

 Mara Paaaaaa!!! akakutana na Mtoto wa Golikipa mahiri nchini Tanzania,Ivo Mapunda ambae enzi hizo waliwahi kucheza timu ya Shule na Kasomfi.






 Mmoja wa walimu waliokuwa shuleni hapo wakati Fortunatus akisoma na kuwa na mchango mkubwa kwake.


WATANZANIA wametakiwa kuwa na utamaduni wa kurudisha fadhila kwa jamii na taasisi zilizowawezesha kupata mafanikio katika Nyanja mbalimbali.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya day, Magreth Haule pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sisimba, Rebeka Tindwa zote za jijini Mbeya walitoa rai hiyo katika nyakati na sehemu tofauti walipokuwa wakipokea msaada wa Mipira na Jezi za timu za shule zao kutoka kwa mmoja wa watu waliowahi kusoma kwenye shule hizo,Fortunatus Kasomfi anayeishi nchini Afrika kusini.

Mwalimu Tindwa alisema ni watu wachache sana ambao huweza kukumbuka walikotoka ikiwemo mashuleni walikoandaliwa msingi bora wa maisha lakini akasema utamaduni wa kukumbuka nyuma ni muhimu sana.

“Ni watu wachache kuwakumbuka waliowasaidia kupata mafanikio na kuwatembelea ili kuwashukuru hivyo tunamshukuru huyu kijana kwani alihitimu hapa mwaka 1991 hivyo wengine waige mfano wake.Hapa anawajengea pia msingi mzuri wadogo zake aliowakuta leo hapa shuleni” alisema Mwalimu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya day, Magreth Haule alisema kama kila aliyepita katika shule hiyo akajitokeza kutoa ushuhuda wa mafanikio yake kutasaidia kuongeza hamasa kwa wanafunzi waliopo mashuleni.

Mwalimu Haule alisema wanafunzi wa siku hizi wamekuwa na tabia mbaya ikiwemo utoro na uchelewaji wa kufika Shule hivyo wahitimu waliofanikiwa wakitoa ushuhuda mbele yao kutasaidia kuwabadilisha.

Hata hivyo kwa pamoja Walimu hao walitoa wito kwa watanzania wenye mapenzi mema hususani waliosoma katika shule hizo kujitokeza kusaidia kutata changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa na walimu hao zinazoweza kupatiwa ufumbuzi kwa wadau mbalimbali waliosoma kurudi na kuwaunga mkono kwa kila mmoja alivyojaaliwa ni pamoja na uchakavu wa majengo kutokana na shule hizo kujengwa zamani ambapo Sisimba ilijengwa mwaka 1950 na Mbeya day sekondari ikijengwa mwaka 1962.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Fortunatus Kasomfi alisema baada ya kupata mafanikio katika shughuli zake nchini Afrika kusini amekumbuka chimbuko lake kuwa ni shule alizosoma.

Kasomfi alisema aliamua kupeleka zawadi ya vifaa vya michezo kwakuwa akiwa katika shule hizo alikuwa akizitumikia timu za shule akiwa Golikipa na kuziwezesha kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Alisema kwa kuanzia ameona atoe seti moja moja kwa kila shule sambamba na mpira ili wengine waweze kuguswa kwa kuchangia kutatua changamoto ya uchakavu wa majengo.

Mtanzania huyo aliongeza kuwa katika mafankio yake ambayo yametokana na msingi mzuri kutoka kwa Walimu wa Shule ya Msingi Sisimba na Sekondari ya Mbeya hivi sasa anajishughulisha na kazi za sanaa pamoja na ujasiliamali.

No comments:

Post a Comment