Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, January 22, 2018

ZIARA YA MAAFISA UBALOZI WA MAREKANI MAKAO MAKUU YA TAJATI









UBALOZI wa Marekani nchini umeahidi kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) katika masuala mbalimbali ya kihabari ili kupanua wigo wa utendaji kazi baina ya pande hizo mbili.

Afisa habari kutoka ofisi ya Ubalozi huo,Bwana Benjamin Ellis amesema kati ya mambo yatakayoimarishwa ni pamoja na kusimamia na kutangaza miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani Kanda ya Nyanda za juu kusini.

Bw.Ellis ametoa ahadi hiyo jana alipofanya ziara ya kutembelea Ofisi za TAJATI zilizopo jijini Mbeya kwa lengo la kujua shughuli zinazofanywa na Chama hicho na kujenga mahusiano kati ya kitengo cha Habari chini ya Ubalozi na Wanahabari wa Tajati.



Amesema amefarijika kufika katika ofisi za Tajati na kujionea shughuli mbalimbali ambazo Chama hicho kimezifanya ambazo zimechangia kuchochea ukuaji wa uchumi katika sekta za Utalii na Uwekezaji nchini.



Amesema atazungumza na uongozi wa Ubalozi ili kuhakikisha Miradi ambayo imefadhiriwa na Serikali ya Marekani na inayotekelezwa katika Mikoa ya ukanda wa Nyanda za juu kusini.



Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na iliyopo katika Sekta za afya, Elimu, Kilimo na kupambana na Uwindaji haramu dhidi ya wanyapori hivyo kutokana na shughuli za TAJATI ni vema ikashiriki moja kwa moja katika kufuatilia utekelezaji wake.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tajati,Venancy Matinya katika taarifa kwa ugeni huo amesema changamoto inayokikabili Chama hicho ni ukosefu wa vitendea kazi vitakavyowezesha kurahisisha kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutembelea maeneo yenye fursa za Utalii na Uwekezaji.



Naye Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili amesema Mfumo wa utekelezaji wa majukumu ya chama hicho unatokana na kufanya kazi kwa ushirikiano wa pamoja kwa kwenda kwenye eneo la tukio kama timu hivyo kinachohitajika ni uwezeshaji wa vitendea kazi.



Mwakilili amesema katika kazi zilizofanyika kwa miaka miwili tangu kuanzishwa kwa chama hicho zilikuwa za kujitolea kwa wanahabari wenyewe hata hivyo zimekuwa zikileta mafanikio   kwa jamii na Taifa kwa ujumla.



Awali Mkurugenzi wa Habari na mahusiano wa TAJATI, Felix Mwakyembe amezitaja baadhi ya kazi zilizofanywa na Chama hicho na kuleta mafanikio kuwa ni pamoja na kuandika habari kuhusu kuvamiwa kwa uwanja wa ndege wa zamani uliopo jijini Mbeya na kuandika kuhusu fursa za Uwekezaji na Utalii katika hifadhi ya wanyama Kitulo.

No comments:

Post a Comment