Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, April 18, 2023

SPIKA DKT. TULIA AICHANGIA MBEYA CITY MILIONI MBILI, WABUNGE NAO WAMUUNGA MKONO




Na Mwandishi wetu, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa kiasi cha Shingi Milioni mbili kwa timu ya Mbeya City ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo dhidi ya Kagera Sugar.
Fedha hiyo imetolewa Aprili 18, 2023 wakati wa Chakula cha mchana kilichoandaliwa na Spika kwa wachezaji wa Mbeya City Jijini Dodoma wakiwa safarini kuelekea Bukoba kwenye Mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa tarehe 23/04/2023
Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Mhe. Spika wa Bunge, Mbunge wa Jimbo la Lupa Chunya kwa kushirikiana na wabunge wa Mbeya nao wametoa kiasi cha Shilingi milioni moja kama sehemu ya motisha kwa wachezaji
Kiasi kilichotolewa na Spika pamoja na wabunge wa Mbeya kinafikisha jumla ya Shilingi milioni tatu.
Pamoja na mambo mengine, Wabunge hao wameahidi kununua ushindi kwa timu ya Mbeya City kwa kila mechi zilizosalia kwenye ligi Kuu ya Tanzania inayoendelea.