Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, October 27, 2014

KIJANA AKUTWA NA SHORTGUN NA RISASI 7 CHUMBANI KWAKE



POLISI mkoani Mbeya inamshikilia mkazi wa mtaa wa Pambogo maeneo ya Airport Jijini Mbeya kwa tuhuma za kukutwa na bunduki aina ya Short Gun na risasi saba alizokuwa akizimiliki kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi,amemtaja anayeshikiliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Emmanuel Mwakeja(27).

Kwa mujibu wa kamanda Msangi kijana Emmanuel amekamatwa Oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 12:40 jioni akiwa nyumbani kwake Pambogo.

Kamanda Msangi alisema awali siku hiyo mnamo majira ya saa 11 jioni maeneo ya uwanja wa Sokoine katika kata ya Sisimba mkazi wa vMakunguru jijini hapa Alfonce Mwakasege(38) aligundua kuibiwa pikipiki yake aina ya Kinglion yenye namba za usajiri T 683 BDM.

Amesema baada ya kufanyika kwa msako wa haraka juu ya wizi wa pikipiki hiyo ndipo walikamatwa watuhumiwa wawili Joseph Kigulu(24) mkazi wa Airport na Juma Nelson(31) mkazi wa Iyela wote jijini Mbeya na walipohojiwa wakasema pikipiki hiyo ipo nyumbani kwa Emmanuel.

Kamanda Msangi amesema mara baada ya kwenda nyumbani kwa kijana huyo na kufanya upekuzi ndipo alipokutwa na bunduki aina ya Shortgun na risasi saba alizokuwa amezificha chini ya Godoro.

Amesema watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi hilo na watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Saturday, October 25, 2014

CHADEMA MBEYA YAPATA PIGO

Mwanzonje akipokea kadi ya CCM kutoka kwa Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga.
 Hapa akielezea kinachompeleka CCM akitokea Chadema
 Mstahiki Meya akizungumza jambo baada ya kumpokea

 









CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) Mbeya mjini kimepata pigo kubwa baada ya mmoja wa makada wake nguli kukihama chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Kada Machachari aliyekihama Chadema ni Joseph Mwanzonje aliyekuwa Mwekahazina wa chama hicho katika kata ya Iziwa iliyopo jijini Mbeya na alikuwa pia mjumbe wa serikali ya mtaa wa Ilungu uliopo katika kata ya Iziwa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi kadi ya Chadema na kukabidhiwa ya CCM,Mwanzonje alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona chama chake hakina mwenendo mzuri.

“Nimefikiri kwa kina nikaona Chadema kila wanachokifanya wanafanya kwa kukurupuka.Hakuna mwelekeo wenye kuonesha dira ya maendeleo ya kichama”

“Maamuzi haya sijakurupuka.Nimefikiri na nikajiridhisha kuwa nahitaji kujiunga na chama chenye mtazamo mzuri.Sijaondoka kwa kificho kwa baadhi ya wanachadema nimewaambia juu ya uamuzi wangu.Naamini pia kati yao wengi watakuja CCM.” Alisema

Akimkaribisha ndani ya CCM mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa,na mlezi wa Chama hicho tawi la kata ya Iziwa,Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga amepongeza uamuzi huo na kumtaka kuwa muadirifu ndani ya chama hicho.

Kapunga alisema kujiunga na CCM ni hatua ya kwanza lakini jambo la pili na lililomuhimu ni kutoa mawazo ya kimaendeleo kupitia vikao mbalimbali vilivyowekwa kwa mujibu wa katiba ya chama.

Alisema yale yote aliyokuwa akiyaona hayatekelezwi na serikali ya CCM katika kuwaletea maendeleo wananchi anapata kuitumia fursa aliyoipata kuwashauri viongozi ili yatekelezwe kwa manufaa ya taifa.

Akiwa ndani ya Chadema Mwanzonje alikuwa tishio kubwa kwa CCM kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa akionesha nyakati za kampeni za chaguzi mbalimbali hivyo kujiunga na chama hicho ni faraja kubwa kwa wanaccm katika kukijenga Chama chao.

Thursday, October 23, 2014

Walio na kazi wana ichezea wakati wasionayo wanaililia.






Na Joachim Nyambo,Mbeya.

UPO usemi usemao “Nilitafuta kazi nikapata kazi,Sintoona kazi kufanya kazi”.Ni nyingi kati ya ofisi za umma utakapoingia utakutana na mabango yaliyoandikwa sentesi hii kwenye kuta kabla haujaingia kukutana na mtu uliye na shida naye.

Maneno haya mazuri na yenye kuonesha watu wa oifisi husika wamekikaa kimkakati wa kiutendaji zaidi umekuwa ukionekana zaidi katika ofisi za umma.Ni faraja kubwa kuingia katika ofisi yoyote na kukutana na maneno kama haya.

Lakini kwa baadhi ya watumishi wa umma kauli hii haina uzito wowote.Wao Badala ya Bilitaka kazi nikapata kazi,sintoona kazi kufanya kazi wao ni Nilipewa kazi bila kazi sintoona kazi kutofanya kazi.Ni kutokana na mtazamo huu wao hufanya kile wanachokiona badala ya kile walichoagizwa.

Mantiki hii ya kutoona umuhimu wa kufanya kazi imejidhihirisha hivi karibuni huko mkoani Kagera ndani ya jeshi la polisi.Kupitia Vyombo mbalimbali vya habari juma lililopita tulimsikia na kumsoma kamanda wa Polisi mkoani Kagera,Hennry Mwaibambe akitangaza hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na jeshi hilo kwa askari walionekana kupigwa picha ya mahaba na kuiweka mitandaoni.

Siku chache kabla ya maamuzi hayo ya jeshi askari wawili walioonekana kuvalia sare za kikosi cha usalama barabarani mmoja akiwa wa kiume na mwingine wa kike walionekana katika picha ya pamoja wakiwa wamekumbatiana na kupigana busu.

Picha hii iliyosambaa katika mitandamo mingi ya kijamii ndani na nje ya nchi ilionesha dhahiri wawili hawa walifanya tukio hili wakati wakiwa katika majukumu yao ya kikazi waliyopangiwa na mkubwa wao.Kwakuwa na askari wa kikosi cha usalama barabara,licha ya kuwa picha haikuonesha barabara lakini ni imani ya walio wengi kuwa walikuwa kando kando ya barabara waliyopangiwa kufanyia kazi siku hiyo.

Picha hiyo ilionesha askari wa kiume akiwa amempakata wa kike wakiendelea kupigana busu.Picha hiyo ilipigwa mwaka 2012 wakati askari hao wakiwa kazini.


Katika kikao chake na waandishi wa habari,kamanda Mwaibambe alisema jeshi hilo limechukua maamuzi ya kuwafukuza kazi askari hao walioonekana katika mkao wa uhusiano wa kimapenzi.

Lakini rungu la jeshi halikuiishia kwa wawili hawa walioonekana kwenye picha.Askari mwenzao pia anaedaiwa kupiga picha hiyo mwaka 2012 na kuisambaza kwenye mitandao ya kijamii.Kamanda Mwaibambe anasema polisi hao watatu wamefukuzwa kwa kukosa maadili mema ya jeshi hilo.

Mwaibambe anawataja polisi walio kwenye picha ya mahaba kuwa ni mwenye namba F.7788 PC Mpaji Mwamsumbi na WP 8898 PC Veronica Mdeme wote wa wilaya ya Missenyi.Aliyewapiga picha ni askari mwenye namba G.2122 PC Fadhil Linga.

Kamanda alisema picha hiyo inakwenda kinyume na maadili mema ya jeshi kwakuwa walipiga picha wakiwa kazini na wamevaa sare za kazi.Kwa upande wa Fadhili kamanda alisema anakabiliwa na kosa la kuwapiga picha wenzake hao kwa kutumia simu yake ya kiganjani na kutuma kwenye mitandao mbalimbali wakati akijua ni kinyume cha maadili ya jeshi la Polisi.Kosa la pili ni kutuma picha hiyo kwenye mtandao.

Kamanda anasema picha iliyoonekana kwenye mtandao ni picha halisi ambayo haijachakachuliwa ama kufanyiwa uhariri wa aina yoyote mpaka iweze kupoteza uhalisia wake.

Kamanda huyo pia anasisitiza kuwa maadili ya jeshi yapo kisheria na askario wao wote wanatambua.Wanapokwenda vyuoni wanafundishwa namna ya kuishi katika maisha ya utumishi wa jeshi la polisi.

Msisitizo huu wa kamanda Mwaibambe ndio unaodhihirisha kuwa askari hawa watatu hawakuona umuhimu wa kufanya kazi,kwasababu hawakufanya kazi kuipata kazi.Wangekuwa wanathamini kazi waliyopewa ni lazima wangesimamia maadili waliyofundishwa chuoni na kuheshimu pia maagizo ya bosi aliyewapangia kazi siku hiyo.

Ni jambo la kusikitisha sana katika dunia ya sasa ambayo kilio kikubwa ni ukosefu wa ajira.Tanzania kama nchi inayoendelea ni miongoni mwa mataifa yanayokabiliwa na wimbi kubwa na ukosefu wa ajira wa wananchi wake.

Vijana ni ndiyo jamii kubwa nchini ambayo kila kukicha kilio chake kikubwa na uhaba wa ajira.Vijana walio na elimu na wasio na elimu wote maisha kwa kiasi kikubwa yamekuwa sawa kwakuwa wote wanaangukia katika kilio kile kile cha kukosa ajira.

Ni hivi karibuni tu hapa nchini ilionekana kituko cha mwaka baada ya wizara ya Mambo ya ndani kupitia idara ya Uhamiaji kuita watu kwenye usahili.Idara hiyo ilikuwa ikihitaji kutoa nafasi za ajira kwa watu wapatao 70 pekee,Ajabu ni kuwa waliitwa kwenye usaili kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaama walikuwa zaidi ya 10,000.Tunaambiwa hao 10,000 walioitwa Dar es salaam ni wale waliochujwa katika mchujo wa awali.

Kwa uwiano huu wa mahitaji ya Idara ya uhamiaji katika usaili huu na watu waliopeleka maombo ni jibu tosha la kuwezesha kujua mahitaji ya ajira yalivyo makubwa nchini.Wapo waliosafiri umbali mrefu kutoka mikoa ya Katavi,Rukwa,Kagera na Kigoma kwenda kwenye usaili na walikosa nafasi licha ya kutumia gharama kubwa.Hii leo watu walioko kwenye ajira kama askari hawa watatu wanachezea ajira yao.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa askari wa jeshi la polisi kuchezea ajira zao.Wapo wengine pia ambao katika kipindi cha hivi karibuni tumekuwa tukisikiwa wamewajibishwa kwa kukiuka matakwa ya ajira yao.Wapo wanaojihusisha na rushwa,Ujambazi na hata wizi wa watoto.

Aprili mwaka huu askari wawili mmoja wa jeshi la polisi mkoani Mbeya na mwingine wa magereza walikuwa miongoni mwa washitakiwa watano waliohukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Askari hawa ni EX-F 8302 PC James(32) wa polisi na B 500 Sajent Juma Musa(37) wa Magereza.Askari hawa walihukumiwa na washitakiwa wenzao watatu na mahakama ya mkoa wa Mbeya kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mawakili wa serikali Basilius
Namkambe na Achileus Mulisa mbele ya hakimu mkaazi mfawidhi wa
mahakama hiyo Michael Mteite kuwa washitakiwa wote kwa pamoja
walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria
kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mawakili hao waliieleza mahakama kuwa washitakiwa hao walitenda kosa
hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima
Kawetere barabara ya Mbeya/Chunya.

Walisema washitakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia
gari lenye namba T 756 ABL aina ya Toyota Pick Up lililokuwa
likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya
ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar
Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili
ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari lingine ambalo
lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 aina ya  Grand Mark II.

Walisema ghafla washitakiwa hao waliokuwa na pingu na panga moja
waliwateka wafanyabiashara na kuwapora fedha taslimu kiasi cha
shilingi milioni tatu,mabegi matatu yaliyokuwa na nguo,Kompyuta
mpakato moja aina ya Sumsang,simu ya kiganjani aina ya Sumsang pia na
mablanketi mawili.

Akisoma hukumu hiyo mahakamani hapo ja, Hakimu mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Michael Mteite alisema watuhumiwa wote kwa pamoja wanatiwa
hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi wawili.

Alisema ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye alikuwa dereva
Ezekia Matatira (34) na shahidi wa pili  Sreedhar Pasupelet(38) mwenye
asili ya Kiasia kwamba haukuacha shaka yoyote na ulishabihiana.

Kama vile haitoshi mwezi huo huo afisa mmoja wa jeshi la polisi akakamatwa na jeshi hilo na kufukuzwa kazi kwa tuhuma za kuiba mmtoto mchanga wa siku saba

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi alimtaja jaskari
anayeshikiliwa kuwa ni Detactive Constable Priscar Kilwai mwenye namba
WP 5367 ambae eneo lake la kazi ni mkoa maalumu wa kipolisi wa Ilala
katika kanda maalumu ya Dar es salaam.

Kamanda Msangi alisema WP Priscar alikamatwa April 17 majira ya
kati ya saa nne na saa tano asubuhi akiwa katika eneo la Meta jijini
Mbeya alikokutwa akiwa na kichanga alichoiba.

Akizungumzia kisa cha wizi huo,kamanda msangi alisema mtoto mchanga
aliyeibwa alifahamika kwa jina la Goodlack Salehe ambaye alizaliwa
April 6 mwaka huu huko mjini Kyela.

Aliwataja wazazi wa mtoto aliyeibwa kuwa ni Mboka Mwakibabile makazi
wa eneo la Njiapanda mjini Kyela ambaye ni mama wa mtoto na Salehe Isa
Mwangosi mkazi wa Kasumulu ambaye ni baba wa mtoto huyo na ambaye pia
anashikiliwa.

Alisema siku moja kabla ya siku ya tukio baba wa mtoto huyo
alimjulisha mzazi mwenzie kuwa kuna shangazi yake ambaye kesho yake
angefika nyumbani kwa mama wa mtoto kwa lengo la kumwona mtoto na pia
aweze kumsindikiza kumpeleka mtoto huyo kliniki.

Alisema siku iliyofuaata yaani April 6 mwaka huu majira ya kati ya saa
sita na saa saba mchana shangazi huyo ambaye ni WP Priscar alifika
nyumbani kwa mkwewe na baada ya kumsalimia mtoto huyo waliongozana
wote wawili kukipeleka kichanga kliniki kama mzazi mwenza alivyokuwa
amependekeza.

Alisema baada ya kufika kliniki walitakiwa kuwa na daftari na kwakuwa
hawakwenda nalo ikalazimu jitihada za kwenda dukani kununua daftari
hilo zifanyike.

Kamanda huyo alisema shangazi huyo bandia alitoa kiasi cha shilingi
2000 na kumpa mama wa mtoto aliyekwenda moja kwa moja dukani huku
akimwacha mwanaye kwa WP Priscar akijua kamwacha sehemu salama kwani
alijua ni bibi yake yaani shangazi wa mzazi mwenzie.

Ajabu ni kuwa mama huyo aliporudi na daftari lake hakumwona mkwewe
wala mtoto hali iliyolazimu aanze kuuliza watu waliokuwepo jirani
ambao baadaye walimwambia kuwa walimwona mtu aliyemwachia mtoto
akipanda pikipiki na kutokomea kusikojulikana.

“Baada ya hapo mama huyu akalazimika kutoa taarifa kituo kidogo cha
polisi kilichopo pale Kyela na jitighada za kutafuta zilianza mara
moja.Hatua ya kwanza ilikuwa ni kumkamata baba wa mtoto kwakuwa moja
kwa moja alionekana kuhusika katika njama za wizi huo” alisema.

Alisema baada ya kumkamata baba wa mtoto jitihada ziliendelea hadi
April 17 alipokamatwa maeneo ya Meta jijini Mbeya akiwa na
kichanga hicho.

“Baada ya kumkamata na kupata tetesi kuwa ni afisa wa jeshi tulianza
kupeleleza na ndipo tukabaini ukweli na kuwa anatokea mkoa maalumu wa
kipolisi wa Ilala Dar es salaam”

Alisema uchunguzi wa awali unaonesha hakuna mahusiano yoyote ya
undugu kati ya askari huyo na baba wa mtoto isipokuwa mahusiano
yaliyopo ni ya kibiashara ambapo ilionekana kuna biashara ambazo
wamekuwa wakifanya kwa kushirikiana.

Matukio haya na mengine mengi yanaonyesha wazi ni kwa namna gani baadhi ya askari hawaoni uchungu wa ajira zao.Wanaziona ajira zao kama kido kisicho cha msingi wakati wasio na ajira wanalia usiku na mchana kusaka.Wapo wanaolazimika hata kwenda hata kwa waganga wa jadi wakiamini huenda wanaweza kusaidiwa kupata ajira.

Ni vema askari wetu wakajitathmini iwapo wanmaitaka kazi au la.Kama wameichoka wanaweza kuweka wazi wakawaachia wanaoihitaji wakalitumikia jeshi kwa uadirifu badala ya kuendelea kulipaka matope jeshi letu.

Mwisho.

Wednesday, October 22, 2014

KAMPENI YA CHANJO YA SURUA-RUBBELA ILIVYOZINDULIWA KIMKOA MBEYA

Mkuu wa wilaya ya Ileje Rosemary Senyamle akimnywesha dawa mmoja wa watoto kama ishara ya kuzindua rasmi kampeni ya chanjo hiyo.

 Mama wanachelewa sana hawa,watatuweka hapa mi nawaita
 Oyaaaa Doktaaaaa fanya fasta njoo nipe chanjo nisepe,sikula kitu cha uji asubuhi ujue,halafu dingi anatungoja home.
 Haya mpigia simu baba mwambie hata wakubwa wanapata chanjo,mwambie aje sawa eeh
 Mama eti ile sindano inauma kama ile ya Ndui?Mi naogopa ujue mamaaa
 Unanidanganya mamaa inaumaaa mbona wale wanalia,mi naogopaaaaa!!!!!!

 Mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Brand Nelson akiangalia kama kamera yake imepata kwa uzuri picha ya mwanafunzi huyu anaeruka sarakasi



Mganga mkuu wa mkoa wa Mbeya Seif Mhina akisakata ngoma ya asili ya kabila la wandali la wilayani Ileje maarufu kwa jina la Babaton

Tuesday, October 21, 2014

WABUNGE WA BUNGE LA CONGRESS LA MAREKANI WATEMBELEA MIRADI INAYOENDESHWA NA ANGLIKANA MBEYA


 
 Mkurugenzi wa Maendeleo wa kanisa la Anglikana dayosisi ya kanda ya Nyanda za juu kusini Padre Jonathan Mwashilindi(kushoto) akitoa maelezo ya namna miradi inayofadhiriwa na Wamarekani


 Wabunge wakikagua bidhaa za mikono zilizotengenezwa na wanavikundi








                                                       HABARI KAMILI

WAJUMBE tisa wa kamati ya bunge la Congres la Marekani wamefanya ziara ya siku moja kutembelea miradi inayoendeshwa na kanisa la Anglikana Dayosisi ya Nyanda za juu kusini inayofadhiriwa na serikali ya Marekani kupitia shirika la Watereed.

Miradi inayoendeshwa na kanisa hilo kwa ufadhili wa wamarekani ni ule wa Kupinga ukatili wa kijinsia(GBV) na ukatili dhidi ya watoto(VAC),Ushauri na upimaji virusi vya ukimwi kwa hiari,Vikundi vya uzalishajimali na mradi wa Elimu ya kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Wakiwa jijini Mbeya wabunge hao wamekagua shughuli mbalimbali zinazofanywa kupitia miradi hiyo kupitia hafla fupi ya maonesho iliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Mbata kabla ya kurejea jijini Dar es salaam.

Katika hafla hiyo fupi,wabunge hao ambao wameongozana na maafisa wachache kutoka ofisi ya Wizara ya Afya walitaka kujua idadi ya watu ambao wamekuwa wakihudumiwa kupitia miradi inayofadhiriwa na wamarekani na pia namna vikundi vinavyonufaika na miradi hiyo.

Akizungumzia,ujio wa wabunge hao Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya nyanda za juu kusini John Mwela aliiwashukuru watu wa Marekani kwa upndo wao wa kuendelea kufadhiri miradi yenye lengo la kuistawisha jamii ya watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo wa kanisa la Anglikana dayosisi ya kanda ya Nyanda za juu kusini Padre Jonathan Mwashilindi amesema kanisa limejipanga kuwahudumia watu walio katika hali hatarishi zaidi kwa kuwafikia na kuwapa elimu.

Amesema pia kanisa limejipanga kuimarisha klabu za watu waliopima ambazo uanachama wake haujalishi kuwa mtu aliyekutwa na maambukizi ya VVU au hana ili kuziwezesha kuwa na miradi ya kujiongezea kipato.

Amesema kwa kuziimarisha klabu hizo kutatoa fursa kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kuwa na njia za kuimarisha kipato chao na kuondokana na utegemezi.