Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, October 4, 2014

WANAJESHI 9 WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Mali unasema kuwa
watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa wakitumia pikipiki wamewaua walinda amani tisa wa Umoja wa Mataifa kaskazini mashariki mwa taifa hilo.

Uvamizi huo ndio mbaya zaidi kuwai kuwakumba wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi hao kutoka nchini Niger walikuwa wakisafiri kati ya miji ya Menaka na Ansongo wakati walipovamiwa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa amesikitishwa na kile alichokitaja kuwa vitendo vya kigaidi.

Mwandishi wa BBC nchini Mali amesema kuwa kikosi hicho cha umoja wa mataifa kimelalamika kuhusu vifaa duni inavyomiliki.

Walindamani hao walitumwa miaka miwili iliyopita baada ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua udhibiti wa maeneo ya kaskazini mwa Mali.

KUTOKA BBC.

No comments:

Post a Comment