Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 30, 2013

MKUTANO WA WADAU WA BONDE LA MAJI LA ZIWA NYASA ULIOFANYIKA MKOANI NJOMBE

UELEWA mdogo wa masuala ya utunzaji mazingira umetajwa kuwa mongoni mwa changamoto kubwa zinazoikabili ofisi ya maji ya Bonde la ziwa Nyasa. Afisa wa maji wa bonde la ziwa Nyasa Witgal Nkondola aliyasema hayo kwenye warsha ya kupitia na kujadili maoni ya wadau mbalimbali wa bonde hilo iliyofanyika mjini Njombe. Nkondola alisema pamoja na jitihada ambazo zmekuwa zikifanywa na ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali bado kuna wimbi kubwa la wananchi wasio na uelewa katika suala la utunzaji wa mazingira ikiwamo vyanzo vya maji. “Elimu ya utunzaji mazingira kwa wakazi wa maeneo ya bonde letu bado inahitajika.Wengi wao hawatambui umuhimu wa kutunza mazingira hivyo wameendelea na vitendo vinavyohatarisha uwepo wa vyanzo vya maji.Hii kwetu ni changamoto kubwa” alisema Nkondola. Afisa huyo pia alieleza uhaba wa rasilimali fedha kuwa kikwazo kingine katika utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya bonde hilo na kuomba serikali na wadau kuangalia uwezekano wa kuongeza bajeti kuisaidia ofisi iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Changamoto nyingine alisema ni upungufu wa watumishi wa kda ya maafisa maendeleo ya jamii aliosema ni nyenzo muhimu ambayo wamekuwa wakiitumia kuielimisha jamii juu ya masuala ya utunzaji mazingira. Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi idara ya rasilimali maji nchini Naomi Lupimo alisema rasilimali ya maji nchini inazidi kupungua kila siku huku mahitaji nayo yakiongezeka hivyo kuibua changamoto ya uwepo wa mkakati madhubuti wa kukabiliana na hali hiyo. Lupimo alitaja sababu za kupungua kwa rasilimali maji kuwa ni pamoja na ongezeko la watu pamoja na shughuli za kijamii ambazo baadhi zimekuwa zikifanyika pasipo kujali athari za kimazingira. Aliwataka wananchi kutambua kuwa rasilimali maji itazidi kuwepo iwapo tu kutakuwa na uangalifu mkubwa katika kuhakikisha vyanzo vya maji vilivyopo vinalindwa na kutunzwa ipasavyo. Akifungua warsha hiyo ya siku mbili yenye washiriki 70,kaimu katibu tawala wa mkoa wa Njombe Mathias Damish aliwataka wadau kutoa maoni yatakayowezesha uwepo wa msukumo chana wa kuliendeleza bonde la maji la Ziwa Nyasa kwa maslahi ya taifa na dunia kwa ujumla. Miongoni mwa wadau waliohudhuria warsha hiyo ni pamoja na wanahabari,wakurugenzi wa halmashauri,maafisa kilimo,maafisa umwagiliaji na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utunzaji wa mazingira.

MATUKIO MBALIMBALI SHINDANO LA REDDS MISS KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI

Saturday, June 29, 2013

MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI ILIVYONOGA

MSHINDI WA MISS REDD'S TANZANIA KANDA ZA NYANDA ZA JUU KUSINI LINA ALLAN AKIWA NA WASHINDI WENGINE AMBAO WALISHINDA TANO BORA

Friday, June 28, 2013

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA RUNGWE WATAKA KUPEWA MKOA MPYA,MADIWANI NAO WATOA JENGO JIPYA LA HALMASHAURI LITUMIKE KAMA OFISI ZA MKOA MPYA IWAPO WATAKUBALIWA

VIONGOZI wa vyama mbalimbali vya siasa wilayani Rungwe wamezungumzia umuhimu wa kuugawa mkoa wa Mbeya huku wote wakionekana mkoa mpya kuitwa jina la wilaya hiyo na makao makuu kuwa mjini Tukuyu. Katika maeneo na nyakati tofauti viongozi hao wameiambia Tripe A kuwa kutokana na historia kuonyesha Rungwe kuwa wilaya ya muda mrefu iliyowezesha kupatikana kwa wilaya nyingine za mkoa wa Mbeya kuna haja ya mkoa mpya kupeleletwa wilayani hapa. Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani hapa Ramadhan Sevungi alisema ni muhimu mkoa mpya ukaitwa Rungwe na wilaya ya Rungwe kwa sasa ikabadilishwa jina na kuitwa wilaya ya Tukuyu. Sevungi alipendekeza halmashauri ya Busokelo iliyoanzishwa hivi karibuni kupewa wilaya ili iweze kuungana na wilaya za Kyela,Ileje,Tukuyu itakayounganisha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Mbeya kuunda mkoa wa Rungwe. Ka upande wake Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) wilayani hapa Antony Mwasasungura alisema kutokana na historian a umaarufu wa watu wa kabila la Wanyakyusa ambao chimuko lao ni wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya umekuwa na umaarufu mkubwa katika Nyanja za kisiasa na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hivyo ni vema ukanda huo ukapewa heshima ya kuwa mkoa. Mwasasungura alisema kwa kupewa mkoa wakazi wa ukanda huo ambao wengi ni wakulima wataweza kuneemeka kupitia fursa za ajira zitakazopatikana kutokana na uwepo wa viwanda hususani vya kusindika matunda kwakuwa kutakuwa na msukumo wa karibu wa kuhamasisha uwekezaji. Naye mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi(CUF) Antony Mwaihojo aliitaja Rungwe kuwa moja ya wilaya zilizo na rasilimali nyingi zinazotosha kujiendesha hata ikipewa hadhi ya kuwa mkoa. “Wilaya yetu ina kanda tatu,Tuna uwanda wa juu wa baridi,uwanda wa kati na ule wa joto.Hizi zote ni fursa zinazotuwezesha kulima mazao ya aina zote na kwa misimu yote ya mwaka.Hivyo tunao uwezo wa kuzalisha mazao ya chakula na biashara yanayoweza kutuingizia kipato na pia akiba ya kutosha ya chakula”

MTOTO APOTEA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI,HISIA ZA KUUAWA ZATANDA KWA JAMII

JINAMIZI la kuibwa kwa watoto limezidi kuukabili mkoa wa Mbeya baada ya mtoto Victor Ngisa(4) wa kitongoji cha Barabarani kata ya Lugelele wilayani Mbarali kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Grace Muhuzi hadi leo ni siku saba zimepita tangu kupotea kwa mwanaye na juhudi za kumtafuta zinaonekana kutokuwa na mafaninikio. Akizungumza na Lyamba Lya Mfipa kwa njia ya simu Grace alisema mwanaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu juni 22 majira ya saa tatu asubuhi alipokuwa akicheza na watoto wenzake. Mama huyo alisema alimwacha mwanaye nyumbani kwa mama yake mdogo kwakuwa yeye alikwenda msitu uliopo jirani kwaajili ya kufuata kuni kwa matumizi ya nyumbani lakini aliporudi hakuweza kukutana tena na mwanaye huyo hadi leo hii. Alisema baada ya kurudi alikutana na mtoto mkubwa kati ya watatu waliokuwa wakicheza na mwanaye na alipomuuliza akasema wenzake walikwenda kuchuma ubuyu katika vichaka vilivyopo jirani na nyumbani kwao lakini alipojaribu kuwafuata huko akakutana na mtoto mwingine na kuambiwa mtoto Victor alilala kabla hajatokea mtu mmoja aliyevaa koti refu jeusi kuwatisha na wao kukimbia. Alisema baada ya watoto hao kukimbia kwa kutishwa na baadaye kubaini walimuacha mwenzao walirejea kwaajili ya kumfuata lakini hawakumkuta tena hivyo wakawa na imani alichukuliwa na mtu huyo wa jinsia ya kiume aliyewatisha. Grace alisema alilazimika kuwafahamisha majirani na jitihada za kumtafuta mtoto huyo zikaanza mara moja na ndipo walipoanza kukutana na taarifa tofauti tofauti kwa kuambiwa na baadhi ya watu kuwa walimuona mtu mmoja akiwa na mtoto mdogo katika maeneo na nyakati tofauti “Kwa siku ya kwanza tulitafuta mpaka usiku bila mafanikio wala taarifa yoyote.Siku ya pili tukiendelea kutafuta tukakutana na watu wakasema walimuona wakiwa wanaelekea machimboni.Siku ya tatu tukakutana na watu wengine wakasema walimuona msukuma mmoja akiwa na mtoto akimnunulia chakula maeneo ya Madibira.Naumia sana kutomuona mwanangu hadi leo” alisema Grace. Mama huyo alisema si tukio la kwanza kutokea wilayani hapo kwani watoto na hata watu wazima wamekuwa wakipotea katika mazingira ya kutatanisha na miili yao kuokotwa baada ya siku kadhaa ikiwa imeharibika vichakani. Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Barabarani Ramadhan Mkatilwa alisema alipokea taarifa ya kupotea kwa mtoto Victor Juni 22 mwaka huu majira ya saa 12 jioni na kulazimika kupiga mbiu kukusanya wakazi wa eneo hilo na jitihada za kumtafuta zikaanza. Alisema katika siku zote za kumtafuta mtoto huyo wametumia njia mbalimbali ikiwemo wamiliki wqa pikipiki kusafiri umbali mrefu kutoa taarifa kwa vijiji jirani lakini hakuna mafanikio yoyote. Mwenyekiti huyo alikiri kuwa si mara ya pili kwa tukio la kuibwa kwa mtoto kutokea eneo hilo kwani Mei 2012 mtoto mmoja aliibwa lakini kwakuwa mama yake alibaini mapema akapiga yowe na watu walipokusanyika mtu aliyemuiba akamtelekeza porini na kukimbilia kusikojulikana. Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwani Athuman awali alisema hana taarifa za kupotea kwa mtoto huyo na kuomba mawasiliano ya wazazi wa mtoto na ndipo alipoamuru mkuu wa kituo cha polisi wilayani Mbarali kufika eneo husika na kupewa taarifa halisi.

WAREMBO 12 KUWANIA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2013 HII LEO

HINDANO LA REDDS MISS KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI 2013 LINAFANYIKA USIKU WA LEO JIJINI MBEYA LIKISHIRIKISHA JUMLA YA WAREMBE 12 KUTOKA MIKOA YA RUKWA,KATAVI,MBEYA,IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA KATIKA UKUMBI WA MTENDA ULIOPO SOWETO.KWA MUJIBU WA MRATIBU WA MASHINDANO HAYO FREDDY HELBERT,KIINGILIO KITAKUWA SH.10,000 KWA VITI VYA KAWAIDA NA SH.25,000 KWA VIP AMBAO WATAPATA NA CHAKULA CHA USIKU UKUMBINI HAPO. SHUGHULI NZIMA ITASINDIKIZWA NA BURUDANI KUTOKA BENDI YA FM ACADEMIA MAARUFU KAMA WAZEE WA NGWASUMA

Thursday, June 27, 2013

AUAWA KWA KUCHOMWA KISU

MNAMO TAREHE 26.06.2013 MAJIRA YA SAA 12:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAMANG’OMBE WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. PATRICK S/O YOHANA,MIAKA 30,MNYAMWANGA, MKULIMA MKAZI WA KIJIJI CHA SAMANG’OMBE ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU UBAVU WA KULIA NA LIVINGSTONE S/O MULYATETE @ MBASA,MIAKA 42,MKULIMA,MNDALI MKAZI WA KIJIJI CHA SAMANG’OMBE. CHANZO NI UGOMVI ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA BAADA YA MAREHEMU KUMTANIA/KUMKEJELI MTUHUMIWA KUWA AMENUNUA PIKIPIKI MBOVU. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUDHIBITI HASIRA ZAO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

NANI ZAIDI KATI YA HAWA?