Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 1, 2013

VIBAKA WAWA TISHIO KWA WAKAZI WA SAE MBEYA

WAKAZI wa eneo la Sae jijini Mbeya jirani na ilipo mitambo ya Shirika la Umeme(Tanesco) wamelalamikia hatari ya uwepo wa vibaka wanayokabiliana nayo kwenye eneo hilo. Hatari hiyo inatokana na mtari wa kupitisha maji ya mvua uliopo maeneo hayo kutumika na vibaka ambao hujificha kutokana na uwepo wa vichaka ambao huwawezesha kujificha na kufanya vitendo mbalimbali vya uharifu ikiwemu kuuza,kununua na kuvuta bangi. Uwemo wa mashamba ya mahindi kwenye eneo jirani na mfereji huo ni usiofuata sheria za halmashauri ya jiji inayozuia kulima mazoa marefu ndani ya eneo lake ni fursa nyingine kwa vibaka na wavutabangi kulitumia eneo hilo kama sehemu ya maskani yao. Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walisema wamekuwa wakidhurika mara kadhaa kwa kukabwa na kisha kunyang’anywa kwa nguvu mali mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na simu za viganjani. Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mama Esther alisema yeye ni miongoni mwa watu ambao mara kadhaa wameporwa mali zao na vijana ambao hulitumia eneo hilo kama njia yao ya kujipatia kipato. Mama Esther alisema nyakati za jioni na alfajiri ni mbaya zaidi kwa wapiti njia wanapofika maeneo hayo tofauti na ilivyo mchana ambapo wapitaji wanakuwa wengi. Mpita njia mwingine Titus Sichone alisema imekuwa ikiwalazimu wazazi na walezi kutowaagiza mizigo watoto hata wakati wa mchana kwakuwa wakiwa peke yao vibaka wa eneo hilo wamekuwa wakiwanyang’anya. Hata hivyo wakazi na wapiti njia walisema ni kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia hali hiyo kwa kufikisha taarifa kwenye vyombo husika lakini hakuna hatua zinazochukuliwa. “Yapo mambo ni ya wazi kabisa.Sheria ya jiji hairuhusu kulima mazao marefu ndani ya eneo lake lakini mashamba haya kila mwaka yanalimwa na kupandwa mahindi na wahusika hawachukuliwi hatua zozote stahili.Yasingelimwa haya mashamba na usafi wa mazingira ukazingatiwa vichaka kama hivi visingepatikana na wanaovitumia wasingekuwepo.Mashamba na vichaka hivi ndiyo fursa kwao kutunyanyasa sisi raia wema” alisema Sichone.

No comments:

Post a Comment