Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Monday, June 3, 2013

KADA WA CCM GORDON KALULUNGA AKABIDHI MPIRA AINA YA JABULAN KWA TIMU YA VIJANA YA CHATU FC YA MBALIZI.HII NI SEHEMU YA KUKUZA AJIRA KWA KUIBUA NA KUVIKUZA VIPAJI VYA VIJANA

Na Mwandishi wetu, Mbalizi TIMU ya vijana chini ya miaka 17 Chatu FC ya mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya, imekabidhiwa mpira aina ya Jabulani wenye thamani ya Tsh.120,000 kutoka kwa Mwandishi wa habari Gordon Kalulunga. Akikabidhi mpira huo mbele ya waandishi wa habari, Kalulunga aliwaambia wachezaji wa timu hiyo kuwa wakitaka mafanikio ni lazima wawe na nidhamu. ''Mkitaka mafanikio ni lazima muwe na nidhamu, pendaneni, ipendeni Mbalizi, ipendeni Mbeya pia ipendeni Tanzania'' alisema Kalulunga. alisema kuwa yeye hana fedha wala dhahabu, bali anao utajiri wa marafiki ambao ndiyo wamefanikisha kupatikana kwa mpira huo kwa ushirikiano na familia yake. Aliwataja baadhi ya marafiki zake waliofanikisha kupatikana kwa mpira huo kuwa ni pamoja na kampuni ya MMI Intergrated steel mills Ltd ya Jijijini Dar es Salaam. Baadhi ya marafiki wa Kalulunga aliokuwa ameongozana nao katika hafla hiyo Ayas Yusuph na Mwandishi wa habari Joachm Nyambo, walisema kuwa timu hiyo wataunga mkono baada ya kuona wachezaji wa timu hiyo wanajituma. Kwa upande wa uongozi wa timu hiyo Emmanuel Mwakapugi na Erasto Mwampamba, walishukuru kwa msaada huo wa mpira na kuitaja moja ya changamoto inayotakiwa kutatuliwa kuwa ni ukosefu wa jezi na viatu.

No comments:

Post a Comment