Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 2, 2013

MWIGULU NCHEMBA ALIPO UNGURUMA MBEYA

NAIBU katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) bara Mwigulu Nchemba amewataka wakazi wa kata ya Iyela jijini hapa kukipa kura chama hicho katika uchaguzi mdogo wa kumchagua diwani wa kata hiyo akisema itakuwa ni shukrani yao kwa rais Jakaya Kikwete kwa kuwaletea wakazi mradi mkubwa wa maji. Nchemba aliyasema hayo jana alipokuwa akimnadi mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM Richard Shangwi kwenye moja ya mikutano ya kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu. “Yapo mengi aliyokwisha yafanya rais lakini hili la kuwaletea mradi mkubwa wa maji na kuwapa heshima ya kuja mwenyewe kuufunguaa yatosha mkamshukuru kwa kumpa udiwani mgombea wake huyu Richard” Aliwataka wakazi hao kutambua kuwa siku uchaguzi kwenye kata hiyo unapaswa kufanyika kwa wakazi kuirejesha nafasi ya diwani kwa mgombea wa CCM kwakuwa aliyekuwepo pia kabla ya kufikwa na mauti alikuwa wa chama hicho. Naibu katibu mikuu huyo alisema wakazi hao kumchagua mgombea kutoka chama kingine ni sawa na anapofariki padre shekhe akakabidhiwa kuliongozaa kanisa lake au anapofariki shekhe padre akakabidhiwa msikiti kuongoza waumini jambo alilosema haliwezekani. Aliwashauri wakazi wa kata hiyo kutambua kuwa kwa kumchagua Shwangwi watakuwa wameiunganisha kata yao na mtandao wa mipango na mikakati ya kimaendeleo unaoendelea kufanyiwa kazi na serikali ya CCM. Alikilinganisha chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ambacho pia kimesimamisha mgombea kwenye kata hiyo sawa na genge la watu waliojipanga kuvuruga amani ya nchi ni kusababisha watanzania kuishi bila amani na utulivu kama walivyozoea. Hata hivyo Nchemba alionya wafuasi wa vyama vya siasa vinavyosjhiriki uchaguzi huo mdogo kutofanya vurugu zaaina yoyote katika mchakato wote wa uchaguzi akisema uchaguzi unaofanyika si vita ya kuwa kila mmoja anang’ang’ania ushindi. Alisema busara ya wananchi wenye kutambua nani anayeweza kuwasaidia kutatua kero zinazowakabili na kusababisha wakapiga hatua kuyafikia maendeleo ndizo zinazopaswa kutumika kuchagua kiongozi wao. Kwa upande wake mgombea Shangwi aliwataka wakazi wa kata hiyo kumpa nafasi hiyo ili aendeleze mipango ya kimaendeleo iliyoachwa na marehemu Mkwenzulu chini ya mwamvuli wa CCM. Aliwataka kuwapuuza wapinzani wanaomchafua kuwa si raia wa Tanzania huku akisisitiza kuwa ni raia mwenye sifa zote na jijini Mbeya ndipo yalipo makazi yake ya kudumu na familia yake kama ambavyo watu wote wanafahamu. Katika mkutano huo Nchemba pia alipokea kadi ya aliyekuwa kada wa Chadema mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya kitivo cha Sheria Ally Katiba aliyeamua kuhamia CCM.

No comments:

Post a Comment