Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Tuesday, June 11, 2013

WANAHABARI WADAU MUHIMU WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO

WAANDISHI wa habari mkoani Mbeya wametajwa kuwa miongoni mwa wadaui muhimu wanaoweza kusaidia kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vinavyofanywa na jamii mkoani hapa. Hayo yalibainishwa na mmoja wa wawezeshaji wa semina ya siku moja ya kuutambulisha mradi wa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wanawake na watoto yanayotokana na unyanyasaji(GBV) Hijja Wazee kwa waandishi wa habari. Mradi huo wa majaribio utakaoendeshwa kwa muda wa miezi 18 chini ya shirika la Water Reed itashirikisha mikoa ya Mbeya,Dar es salaam,Mara na Iringa ikiwa ni mikoa inayoongoza kwa kuwa na matukio ya unyanyasaji kwa wanawake na watoto. Kwa mkoani Mbeya mradi huo utaendeshwa katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya,Ibaba wilayani Ileje,bijiji vya kata za Chokaa na Itewe wilani Chunya,na Ilembo na Masoko wilayani Mbeya. Maeneo Mengine ni Tukuyu Rungwe,Mwakaleri Busokelo na baadhi ya maeneo ya wilaya ya Kyela amapo maeneo yote hayo mradi utajikita kwenye ukatili unaofanyika kwenye maeneo ya huduma za afya na pia maeneo ya kijamii ikiwa ni kwa hisani ya mfuko wa rais wa Marekani. Akiwasilisha mada ya Jukumu ya vyombo vya habari kwenye utekelezaji wa mradi huo,Wazee alikiri kundi hilo kuwa muhimu na litakalowezesha jamii kujua nini kinaendelea kwenye maeneo yao. Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya jamii ya wanawake na watoto imekuwa ikitendewa ukatili pasipokujua kama haikupaswa kufanyiwa hivyo kubaki ikiona matukio hayo kama ya kawaida. Alisema ni kalamu ya mwandishi wa habari pekee itakayowezesha kuibadilisha jamii iliyo na mawazo duni kama hiyo pamoja na wanaume ambao pia wamekuwa wakiwafanyia ukatili wanawake kwa misingi ya mfumo dume. Mwezeshaji mwingine Mergitu Ebba aliwataka waandishi wa habari walioteuliwa kushiriki utekelezaji wa mradi huo kujiona sehemu ya mradi na kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao ipasavyo wakilenga kuisaidia jamii inayowazungunga. Hata hivyo baadhi ya wanahabari wakiwasilisha kazi za makundi walizitaja changamoto zitakazokabili utendaji kazi wao kuwa ni pamoja na ugumu wa kuyafikia baadhi ya maeneo,jamii kutotoa ushirikiano kwa kuogopa aibu au kuvunja miiko ya makabila ama koo zao.

No comments:

Post a Comment