Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Sunday, June 23, 2013

UZINDUZI WA MRADI WA GBV ULIVYOFANA WILAYANI KYELA

MMOJA WSA WARATIBU WA MRADI WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VVU KWA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA NA WATOTO(GBV) HIJJA WAZEE AKISOMA TAARIFA YA MRADI HUO HUKU AKISIKILIZWA KWA MAKINI NA MKUU WA WILAYA YA KYELA MAGRETH MALENGA AKIMSIKILIZA KWA MAKINI SIKU YA UZINDUZI WA MRADI SHUGHULI ILIYOFANYIKA KWENYE UWANJA WA MWAKANGALE KYELA MJINIMKUU WA WILAYA YA KWELA AKIKABIDHI CHETI KWA MMOJA WA WATU WATAKAOJITOLEA KUSHIRIKI KATIKA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO UNAOFADHILIWA NA MFUKO WA RAIS WA MAREKANI.WASHIRIKI WA KUJITOLEA KATIKA GBV WAKIFURAHIA VYETI BAADA YA KUKABIDHIWA NA MKUU WA WILAYABURUDANI NAZO ZILICHUKUA NAFASI YAKE NA KUMFURAHISHA KILA ALIYEHUDHURIA UZINDUZI HUO. WANAWAKE wametakiwa kudai haki zao kwa kufuata misingi yenye kulenga kuleta usawa wa kijinsia na si kwa kutumia lugha za kuwanyanyasa wanaume. Mkuu wa wilaya ya Kyela Magreth Malenga aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi(VVU) kwa kukomesha ukatili wa kijinsia na watoto(GBV) utakaoendeshwa na shirika la Watereed iliyofanyika kwenye uwanja wa Mwakangale uliopo wilayani hapa. Malenga alisema wapo baadhi ya wanawake wanaotumia kigezo cha kudai haki zao kwa kutumia mbinu ambazo kimsingi na wao wanawakosesha haki waume zao. “Baadhi ya wanawake wanavyojitetea sasa imegeuka unyanyasaji kwa waume zao.Kila siku huko ndani ni kupiga kelele na sisi wanawake tunajijua tuilivyo hodari wa kupiga kelele.Mwan aume hawezi kupiga kelele lakini tutambue kuwa tunakuwa hatumtenei nay eye haki hivyo tunageuza ukatili toka kwetu tunapeleka kwake” alisema Malenga. Mkuu huyo wa wilaya aliwasihi wanawake kuhakikisha wanadai haki kwa kufuata misingi yenye kuwa na manufaa kwa familia yote na si upande mmoja kama inavyoonekana kufanyika. Aliitaka jamii pia kuwa na mtazamo chanya wa kutoa usawa katika kuwapa elimu watoto akisema hakuna mizani inayowezesha kutambua ni nani mwenye faida kwa familia kati ya mtoto wa kike na wa kiume baada ya kupewa elimu. Alisema bado jamii inawapa kipaumbele watoto wa kiume kwa kuwapa elimu kwa kisingizio kuwa ndiyo wanaoweza kuisaidia familia husika baada ya kupata ajira jambo alilosema ni dhana potofu na iliyopitwa na wakati. Malenga pia alilalamikia hatua ya unyanyasaji wa kijinsia kuonekana kupungua kwa kasi ndogo jambo alilosema inaonesha jamii kutolitilia mkazo na kuona unyanyasaji wa aina hiyo ni sehemu ya maisha ya kawaida. Awali mmoja wa waratibu wa mradi wa GBV Hijja Wazee alisema mradi huo wa miezi 18 unaofadhiliwa na mfuko wa rais wa marekani utaendeshwa wilayani hapa kwa kushirikiana na shirika la Mango Tree.

No comments:

Post a Comment