Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 1, 2013

MOMBA WANAVYOTAKA MKOA MPYA UWE

WADAU katika halmashauri ya wilaya ya Momba wamependekeza mkoa mpya utakaogawanywa kutoka mkoa wa Mbeya kupewa jina la wilaya hiyo huku wakishauri mkoa huo mpya uundwe na wilaya za Momba,Mbozi,Ileje na Chunya. Wadau hao wakiwemo wataalamu wa halmashauri ya wilaya ya Momba wamependekeza makao makuu ya mkoa huo mpya kuwa katika mji mdogo wa Vwawa uliopo wilayani Mbozi. Mapenekezo hayo yalitolewa kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kijijini Ukwile wilayani Mbozi kutokana na miundombinu kutokamilika katika kijiji cha Chitete yalipo makao makuu ya wilaya hiyo mpya. Wajumbe wa kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti mkuu wa wilaya hiyo Abiudi Saideya walipendekeza mara baaad ya kugawanywa mkoa wa Mbeya ubaki na wilaya ya Mbeya, Kyela, Rungwe na Mbarali. Saideya alisema wilaya ya Momba ina vivutio vya kiutalii, idadi ya watu kubwa ya wakazi, pamoja na sifa ya kuzalisha mazao ya chakula na biashara kama vile ufuta, kahawa, mahindi, mpunga pamoja na uoto mzuri wa asili. “Sote tunatambua kuwa Momba ndio kitovu cha barabara kuu iendayo nchi za kusini mwa Afrika.Iwapo utapewa hadhi ya Mkoa utaongeza kipato kupitia ushuru wa forodha kwa nchi za kusini mwa afrika,”alisema Mkuu huyo wa wilaya pia alikitumia kikao hicho kutoa onyo kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kusababisha vifo vya watu kutokana na imani za kishirikina ambavyo vimetajwa kukithiri wilayani hapa. Aliwataka waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli kuacha mara moja akisisitiza kuwa wao ni chanzo kikubwa cha matukio yanayohusisha imani za kishirikina na kusababisha migongano ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment