Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Thursday, June 13, 2013

BENKI YA POSTA MBEYA WACHANGIA DAMU SALAMA

WAFANYAKAZI wa benki ya Posta tawi la Mbeya leo wamejitolea kuchangia damu salama ikiwa ni mkakati wa watumishi hao kusaidiana na jamii inayowazunguka. Wafanyakazi waliochangia damu katika kituo cha mpango wa damu salama kanda ya nyanda za juu kusini kilichopo jijini Mbeya ni saba kati ya 12 walliopo katika tawi hilo. Wafanyakazi hao ni Felix Mapunda,Antony Ngonye,Winifrida Kalinga.Boniface Mwakajinga,Amon Mwakajungwa ,Hagai Gilbert na Noel Fredy. Akizungumzia tukio hilo,Meneja wa Posta tawi la Mbeya Hamfray Julius amesema wameamua kuchangia damu ili pia kuihamasisha jamii kujenga mazoea ya kuchangia damu kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo. Kwa upande wake Meneja wa mpango wa taifa wa Damu salama kanda ya nyanda za juu kusini Dk.Baliyima Lelo amesema kituo kimekuwa kikikusanya chupa 18,000 hadi 19,000 za damu kwa mwaka wakati mahitaji halisi ni chupa 45,000. Hii si mara ya kwanza kwa benki ya posta kusaidia kituo hicho kwani katika siku ya maadhimisho ya uchangiaji wa damu salama mwaka jana ilitoa fulana 50 zilizokuwa na ujumbe wenye kuihamasisha jamii kushiriki uchangiaji damu.

No comments:

Post a Comment