Friday, June 28, 2013
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA RUNGWE WATAKA KUPEWA MKOA MPYA,MADIWANI NAO WATOA JENGO JIPYA LA HALMASHAURI LITUMIKE KAMA OFISI ZA MKOA MPYA IWAPO WATAKUBALIWA
VIONGOZI wa vyama mbalimbali vya siasa wilayani Rungwe wamezungumzia
umuhimu wa kuugawa mkoa wa Mbeya huku wote wakionekana mkoa mpya
kuitwa jina la wilaya hiyo na makao makuu kuwa mjini Tukuyu.
Katika maeneo na nyakati tofauti viongozi hao wameiambia Tripe A kuwa
kutokana na historia kuonyesha Rungwe kuwa wilaya ya muda mrefu
iliyowezesha kupatikana kwa wilaya nyingine za mkoa wa Mbeya kuna haja
ya mkoa mpya kupeleletwa wilayani hapa.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilayani hapa Ramadhan Sevungi
alisema ni muhimu mkoa mpya ukaitwa Rungwe na wilaya ya Rungwe kwa
sasa ikabadilishwa jina na kuitwa wilaya ya Tukuyu.
Sevungi alipendekeza halmashauri ya Busokelo iliyoanzishwa hivi
karibuni kupewa wilaya ili iweze kuungana na wilaya za
Kyela,Ileje,Tukuyu itakayounganisha na baadhi ya maeneo ya wilaya ya
Mbeya kuunda mkoa wa Rungwe.
Ka upande wake Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)
wilayani hapa Antony Mwasasungura alisema kutokana na historian a
umaarufu wa watu wa kabila la Wanyakyusa ambao chimuko lao ni wilaya
ya Rungwe mkoa wa Mbeya umekuwa na umaarufu mkubwa katika Nyanja za
kisiasa na uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hivyo ni vema
ukanda huo ukapewa heshima ya kuwa mkoa.
Mwasasungura alisema kwa kupewa mkoa wakazi wa ukanda huo ambao wengi
ni wakulima wataweza kuneemeka kupitia fursa za ajira zitakazopatikana
kutokana na uwepo wa viwanda hususani vya kusindika matunda kwakuwa
kutakuwa na msukumo wa karibu wa kuhamasisha uwekezaji.
Naye mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi(CUF) Antony Mwaihojo aliitaja
Rungwe kuwa moja ya wilaya zilizo na rasilimali nyingi zinazotosha
kujiendesha hata ikipewa hadhi ya kuwa mkoa.
“Wilaya yetu ina kanda tatu,Tuna uwanda wa juu wa baridi,uwanda wa
kati na ule wa joto.Hizi zote ni fursa zinazotuwezesha kulima mazao ya
aina zote na kwa misimu yote ya mwaka.Hivyo tunao uwezo wa kuzalisha
mazao ya chakula na biashara yanayoweza kutuingizia kipato na pia
akiba ya kutosha ya chakula”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment