Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 1, 2013

MBUNGE ZAMBI AIHAKIKISHIA VWAWA MAJI YA UHAKIKA

ASILIMIA 70 ya wakazi wa mji mdogo wa Vwawa wilayani Mbozi watakuwa wanapata maji safi na salama ifikapo mwaka 2015. Hayo yalisemwa na mbunge wa Mbozi Mashariki Gofray Zambi alipozungumza na wakazi hao ikiwa ni ziara ya kumkutanisha na wananchi ili kbaini kero zinazowakabili na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kuzitatua kwa kushirikiana na wadau. Zambi alisema ili kufikia malengo hayo serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 570 ili kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwenye mji huo kupitiatia vyanzo vya maji vilivyopo ambavyo ni vya uhakika. Kadhalika mbunge huyo alisema kama inavyoendelea kwa upande wa barabara za mji huo,serikali pia ina mpango wa kuboresha huduma za upatikanaji wa nishati ya umeme kwenye mji wa Vwawa na vijiji vingine 15 vilivyopo jimboni hapa. Alivitaja baadhi ya vijiji ambavyo vitanufaika na mpango huo kuwa ni pamoja na Hasamba,Itaka,Hezya,Senjele,Itapula,Itewe,Haterere na Hasanga. Aliwataka wananchi kutambua kuwa serrikali ina malengo mazuri ya kutatua kero zinazowakabili wananchi lakini inabidi ifanye hivyo kwa hatua huku akisisitiza kuwa kero zote haziwezi kutekelezwa kwa wakati mmoja. Zambi alionya wananchi kutowasikiliza wanasiasa wanaopanda majukwaani na kuwapotosha kwa kuwaambia uongo kuwa serikali haifanyi lolote na kuwataka pia wanasiasa hao kubadilika kwa kuwaambia ukweli wananchi. “Tusipande majukwaani kutukana,tuwaeleze wananchi nini serikali yao inafanya.Ndiyo sababu tunawasihi pia wananchi kuwa makini na wanasiasa wa aina hii.Hawa ndiyo wale wanaoeneza pia chuki na kuigombanisha serikali ya CCM na wananchi lakini wao tukiwa kwenye maeneo tunayokutana wanaongea na sisi,kula pamoja na kunywa pia tofauti na walivyo waelezeni ninyi”. Aliwataka pia wananchi kujituma katika kufanya kazi za uzalishaji mali kwa bidii pamoja na kuwapeleka watoto shule akisema hiyo ndiyo njia ya kupata maisha bora na si kusubiri misaada kutoka kwa mtu mwingine.

No comments:

Post a Comment