Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, June 1, 2013

WASANII MBEYA KUANDAA FILAMU KUPINGA MAANDAMANO,MIGOMO

KATIKA kuonyesha kutoridhishwa na tabia ywanasiasa kuwatumia vijana katika migomo na maandamano,vijana kupitia wasanii mkoani hapa wapo kwenye mchakato wa maandalizi ya filamu ya kupinga masuala hayo. Ili kukamilisha lengo hilo vijana hao tayari wamekutana na viongozi wa vyama vya siasa ikiwemo Chama Cha Mapinduzi mkoani hapa na kuzungumzia nia ya suala hilo wazo lililoonekana kupokelewa kwa shwangwe kubwa na viongozi wa CCM. Kiongozi wa vijana hao George Tyson alisema lengo la filamu hiyo itakayohusisha zaidi ya wasanii 300 wa mkoani hapa ni kuwafumbua macho vijana kutambua kuwa wao kama nguvukazi ya taifa wanapaswa kutumiwa katika masuala ya msingi na yenye tija kwa taifa lao. “Tungependa vijana watambua wanatumika vibaya.Sasa wajikite kwenye kufikiri mawazo chanya.Maandamano yamekuwa mengi nchini lakini tunajiuliza anayefaidika nayo mbona siyo sisi tunaotumika.Tunataka vijana wapiganie maendeleo yao na taifa lao na si maslahi ya mtu mmoja anayenuia kulipa hasara taifa lao” alisema Tyson. Akipokea wazo la vijana hao,mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Mbeya mjini ambaye pia ni katibu wa madiwani wa halmashauri ya jiji la Mbeya Godian Mwambasi alisema maambamano yanayofanyika hivi sasa ni sawa na nyavu za kokoro zinazokusanya kila kitu tofauti nay a miaka ya zamani ambapo walioandamana walikuwa na hoja ya msingi waliyoisimamia. Alitaja baadhi ya athari zinazotokea kutokana na maandamano ya sasa kuwa ni pamoja na wizi unaofanywa na waandamanaji wasiojua hata ni kwa nini wanaandamana pamoja na uchomaji wa barabara za lami zilizojengwa kwa fedha nyingi za serikali au wahisani mbalimbali. Naye mmoja wa makada wa chama hicho Charles Mwakipesile kwa kuona umuhimu wa wazo la vijana hao licha ya kuchangia shilingi 50,000 papo hapo na kufanya harambee fupi kwa kuchangisha fedha toka kwa viongozi wa CCM pia aliahidi kushirikiana bega kwa bega hadi kufikiwa kwa lengo husika. Mwakipesile alisema azamani maandamano yalilenga kushinikiza hoja yenye manufaa kwa taifa na ndiyo sababu yalifanyika kwa hekima na busara kubwa yakitambulisha nini chanzo,nani wanaandamana na ni nani anayeshinikizwa na lakini sasa yanatumika kuvuruga amani na utulivu wa chi.

No comments:

Post a Comment