Karibu katika blogu hii,kuwa mmoja wa wale wanaochangia na kujivunia mafanikio yake. Tunakualika kwa mikono miwili wasiliana nasi kwa simu 0756409597 au nyambojoachim@gmail.com

Saturday, August 18, 2012

MBEYA WASUBIRI LIGI KUU


MENEJA wa uwanja wa Sokoine uliopo jijini Mbeya Modestus Mwaluka amesema maandalizi ya uwanja kwaajili ya ligi kuu ya Tanzania bara yamekamilika.

Akizungumza na LYAMBA LYA MFIPA,Mwaluka amesema kinachosubiriwa sasa ni kuanza kwa ligi hiyo lakini kwa upande wa maandalizi ya uwanja hakuna la ziada tena katika maandalizi.

Amesema yapo maboresho makubwa yaliyofanyika katika uwanja huo na sasa upo katika kiwango cha ubora unaofaa kwa michuano mikubwa kama ligi kuu inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.

Amesema miongoni mwa maeneo yaliyofanyiwa ukarabati ni pamoja na eneo la kuchezea(Pich) ambalo limejazwa udongo na kuoteshwa nyasi katika maeneo yaliyokuwa na mabonde hali ambayo awali ilikuwa ikisababisha usumbufu kwa wachezaji wakiwa katika mechi husika.

Meneja huyo amesema kwa maboresho yaliyofanyika kwa sasa uwanja uko katika hali nzuri na hata wachezaji wataona raha kuutumia tofauti na awali.

Kwa upande wa masuala ya usalama,Mwaluka amesema kwa sasa usalama wa wachezaji wawapo uwanjani,wale wa akiba pamoja na waamuzi na wahusika wengine ni mkubwa kutokana na wigo uliopo ambao katika siku za mechi ulinzi utaimarishwa zaidi ili mashabiki wasipate fursa ya kuingia eneo lisilowahusu.

“Mpaka sasa hatujapata ratiba lakini kwa taarifa tuilizonazo wakati wowote kuanzia leo itatoka.Kwa upande wetu kama wamiliki na wasimamiaji wa uwanja tumekamilisha mambo yote muhimu ikiwemo uboreshaji wa maeneo korofi.Tunachosubiri ni kuanza tu kwa ligi” amesema Mwaluka.

Hata hivyo baadhi ya wadau wa michezo jijini Mbeya wakiwemo wanahabari wameshauri uongozi wa uwanja kwa kushirikiana na chama cha soka mkoani Mbeya (MREFA) kuhakikisha unakuwepo utaratibu maalumu ambao hautaruhusu mamluki kuvamia eneo la wanahabari.

Katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu,mkoa wa Mbeya na mingine iliyopo jirani itawakilishwa na timu ya Tanzania Prisons ya jijini hapa iliyopata daraja baada ya kufanya vyema katika michuano ya ligi daraja la kwanza iliyopita.

Friday, August 17, 2012

WATANO WAFA MBEYA AKIWEMO MAMA NA NA WATOTO WAKE WAWILI

WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti likiwemo la familia ya mama na watoto wake wawili waliofariki kufuatia ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao wakiwa wamelala.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya  mrakibu mwandamizi Barakiel Masaki, tukio hilo lilitokea  Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 4:55 usiku.

Alisema wanafamilia hao wakiwa wamelala nyumba yao ilianza kuwaka moto na kwamba walipoteza maisha kutokana na kukosa hewa kufuatia moshi mzito ulioenea ndani ya nyumba.

Amewataja wanafamilia hao waliokufa ni mama mzazi  Upendo Paul(24) na watoto wake ambao ni Tecra Paul (4) na Aman Paul wote wakazi  wa Ilemi darajani jijini Mbeya.

Masaki alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa bado hakijajulikana na miili ya maremu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoani hapa.

Aidha  ametoa wito kwa  wananchi kuchukua tahadhari kutokana na majanga ya moto  yanayotokea  mkoani  hapa.

Wakati huo huo mkazi wa majengo Mkwajuni  wilayani  Chunya Sprian Majiyashamba(58) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuumua mke wake kwa kumchoma kisu   kutokana  ugomvi wa kifamilia.

Kaimu kamanda Masaki  amesema marehemu  alifahamika kwa  jina la Secilia Dotabarabara(64) ambaye alichomwa kisu na mume wake kwenye titi la kushoto na kusababisha kifo chake  papo hapo.

Masaki  amesema kuwatukio hilo lilitokea Agosti 16 mwaka 2012 majira ya saa 4:00 katika kijiji cha majengo  wilayani chunya na kutaja chanzo cha kifo hicho kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

Katika tukio lingine mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha  nyakazobe wilayani Mbarali amemuua mume wake kwa kumpiga  na kitu kitu kizito kichwani kutokana kutokana na na ugomvi wa kifamilia.

Akielezea tukio hili  Masaki  amesema limetokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku kijijini hapo,na kwamba Christina Msiyunga(24) alimuua mume wake Geoge Lova(26) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Amesema   mtuhumiwa  wa tukio hilio amekamtwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika,aidha aliwaomba wananchi  kutatua migogoro kwa amani ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima.

Thursday, August 9, 2012

KIFAA CHA KUZUIA AJALI ZA MELI

Kifaa hiki ndicho kilichgunduliwa bado hakijapewa jina


Mtaalamu maswala ya umeme Joseph Matwani akiwaelezea baadhi ya wananchi waliotembele banda hilo jinzi kifaa hicho kinavyofanyakazi
HABARI KAMILI

MWANAFUNZI wa Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MUST) amebuni  na kutengeneza kifaa maalum kinachodaiwa kuweza kudhibiti kupunguza na ikiwezekana kumaliza kabisa tatizo la ajali za vyombo vya usafiri wa bahari kama ilivyotokea hivi karibuni kwa Meli ya Mv.Skargit iliyogharimu maisha ya watanzania wengi.

Akizungumza na Mbeya yetu Mtaalamu wa masuala ya umeme katika chuo hicho,Joseph Matwani amemtaja mwanafunzi aliyekitengeneza kifaa hicho ambacho kinabaini meli ama boti litakalozidisha abiria ama mizigo  kuwa ni Zuberi Rutumbo.

Bw.Matwani alisema kifaa hicho ambacho bado akijapewa jina kitakuwa na uwezo wa kutoa taarifa katika mamlaka husika mathalani,Sumatra,Polisi,kwa mmiliki,nahodha na mamlaka nyinginezo zitakazoingizwa katika programu maalum kuwa meli Fulani imejaza mzigo kuliko uwezo wake na hivyo kusaidia kuizuia bandarini kabla haijaondoka.

Mtaalamu huyo amesema kuwa kifaa hicho kitafungwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri wa baharini  ambapo vitawaonesha makapteni kuona kiasi cha mzigo uliopakiwa na kuwajulisha endapo watazidisha baada ya maji kuvuka mstari wa chombo husikai kabla ya kuondoka na hivyo  kutoa mlio wa taadhari na baada ya sekunde kumia ujumbe unakwenda katika nambari za simu zilizokuwa zimefanyiwa programu katika kadi ya simu
.
Amesema kutokana na taarifa hiyo ya ujmbe mfupi wa maneno katika simu za wahusika wanatumaini kuwa watachukuwa hatua kukizuia chombo hicho kisiondoke na hivyo kufanikiwa kunusuru maisha ya  abiria na kupunguza ajali zinazodaiwa zinasababishwa na uzembe wa makapteni kuzidisha mzigo kwa makusudi.

 Mvumbuzi huyo Rutumbo amesema ameamua kutengeneza kifaa hicho alichoanza kukifikiria tangu mwaka 2011  baada ya  kuibuka kwa ajali  mbaya za meli ya Mv.Bukoba,Mv.Spice  na juzi Mv.Skargit na hivyo kuamua kuandika ‘project’ ( mradi) baada ya kushuhudia matukio hayo.

Amesema ajali nyingi zinaonekana zinasababishwa na uzembe wa watu wachache waio na huruma na watanzania lakini anaamini kupitia kifaa hicho uwajibikaji utaongezeka na kila mmoja atawajibika kupitia nafasi yake na kuwabaini wazembe ambapo pia kifaa hicho kinaweza kufungwa  katika mlango ama dirisha katika nyumba na kuprogramu katika simu na hivyo kukupa taarifa ya uhalifu endapo unatokea.

Tuesday, August 7, 2012

TUKO NANE NANE

Mwanamke ambaye hakufahamika jina lake akiwa amenasa katika seng'enge alipojaribu kutumia njia isiyo halali kufika lilipo bwawa dogo la maji aliyokuwa akiyahitaji kwaajili ya matumizi katika Uwanja wa maonesho ya wakulima(Nane nane )kanda ya nyanda za juu kusini wa John Mwakangale jijini Mbeya
 Watoa huduma za vyakula katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya yanakofanyika maonesho ya wakulima nanenane kanda ya nyanda za juu kusini wakiendelea kuwatayarishia wateja wetu kama walivyokutwa na kamera yetu muda mfupi uliopita

BONANZA LA KUFUFUA TUKUYU STARS

 Mkuu wa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya Crispin Meela (Mwenye kofia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wachezaji wa timu ya Tukuyu stars mwaka 1986 ilipovuma na kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzaniua bara.Meela na wachezaji hao walipiga picha hii katika bonanza la kuhamasisha kufufuliwa kwa timu hiyo lililofanyika katika mji mdogo wa Tukuyu
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Crispin Meela akijiandaa kupiga mpira wa penati kama ishara ya kuzindua bonanza la kuhamasisha kufuful;iwa kwa timu ya Tukuyu Stars lililofanyika jana katika mji mdogo wa Tukuyu wilayani hapo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo kikundi cha Tukuyu Stars Family(Banyambala) cha jijini Dar es salaam.

Sunday, August 5, 2012

MWEKA HAZINA MBARONI KWA UBADHIRIFU


MWEKA hazina katika halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Ferdnand Manyere(52) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za serikali kiasi cha shilingi 87,245,420.43.

Taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi mkoani Mbeya Athuman Diwani kwa vyombo vya habari leo(Agosti 5) inaeleza kuwa afisa huyo anashikiliwa kwaajili ya kuhojiwa juu ya ubadhirifu huo.

Kamanda Diwani alisema mnamo Agosti 2 mwaka huu jeshi hilo lilipokea taarifa juu ya ubadhirifu wa kiasi hicho cha fedha kutoka halmashauri ya wilaya ya Mbarali na ndipo walianza kulifanyia kazi na hatimaye kumkamata mtuhumiwa mmoja.

Alisema ubadhilifu huo unadaiwa kufanyika kati ya Aprili na Juni mwaka huu na kubainisha kuwa fedha hizo zilikuwa za miradi mbalimbali na malipo ya wazabuni.

“Mtuhumiwa mmoja Ferdnand Manyere ambaye ni mweka hazina wa halmashauri ya wilaya hiyo amekamatwa na aanaendelea kuhojiwa na polisi.”imeeleza taarifa hiyo

Kamanda huyo amesema baada ya upelelezi kukamilika jeshi hilo litatoa taarifa kwa umma juu ya matokeo na hatua zilizochukuliwa.

Hivi karibuni katika kikao maalumu cha kupitia taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(CAG) mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliitaja halmashauri ya wilayaa ya Mbarali kuwa miongoni mwa halmashauri zisizo na nidhamu katika matumizi ya fedhaa za miradi mbalimbali.

Friday, August 3, 2012

NANE NANE MBEYA

MKULIMA MTAALAMU KUTOKA HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA MKOANI KATAVI AKITOA MAELEZO YA NAMNA YA KULIMA BUSTANI MFUKO KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI YANAYOENDELEA KATIKA UWANJA WA JOHN MWAKANGALE JIJINI MBEYA.

Thursday, August 2, 2012

WASIKILIZE SHAROMILIONEA,SHILOLE NA BARNABA

Shilole na Sharomilionea
"Nikiamka na hela kwenye wallet siku yangu huianza na tabasamu tele.Nisipoamshwa na simu ya habari mbaya na kubwa zaidi nipatapo maoni mazuri na ya kutia moyo kutoka kwa fans wangu"...Sharo milionea.
 ''Nikiamka salama,nikiwa sina binadamu yoyote anayenisumbua na kuniskosesha amani,gari yangu ikiwa full tank na nikiwa na pesa kwenye waleti"...Shilole
"Kwanza nina meno mazuri masafi na meupe yamejipanga vizuri,pia napenda kucheka sijui kukasirika hata nikikerwa"...Barnaba

MWAKALEBELA NA MUNGAI WASAKWA NA TAKUKURU IRINGA

Siku Mwakalebela na mkewe walipopandishwa kizimbani na TAKUKURU Iringa
Siku Mungai alipopandishwa kizimbani na TAKUKURU Iringa

TAASISI ya kuzuaia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa yazidi kumng’ang’ania aliyekuwa waziri wa wizara mbali mbali katika awamu mbali mblia katika serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mufindi Kaskazin Joseph Mungai kwa lengo la kumfikisha mahakamani ili kujibu mashitaka ya kujihusisha na rushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2010.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Iringa kaimu mkuu wa Takukuru mkoani hapa Stephen Mafipa amesema taasisi hiyo inamtafuta mheshimiwa mungai ili kumfikisha mahakamani kujibu mashitaka hayo baada ya mahakama kuu kanda ya Iringa kupitia kwa jaji kiongozi wa mahakama hiyo sekieti kihio kutupilia mbali rufaa yake.

katika rufaa yake aliyokata kupitia kwa mawakili wake wawili basiri mkwata na Alex Mgongolwa Mungai aliiomba mahama hiyo kutupilia mbali uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa kupitia kwa mheshimiwa marry senapee tarehe 31 january 2011 ambapo alitupilia mbali hati yamashitaka ya rushwa yaliyokuwayakimkabli mheshimiwa mungai na kuamuru upande wa mashitaka kufanyia marekebisho hati hiyo na kumfikisha mahakamani mtuhumiwa.

katika rufaa yake mh.mungai aliiomba mahakama hiyo kutupilia mbali uamuzi wa mahakama ya hakimu mkazi na kisha kutolea maamuzi hoja nyingine ambazo hazikutolewa maamuzi na mahakama hiyo ya hakimu mkazi ambapo katika makosa yote 15 ya kutoa rushwa ambayo mungai alikuwa akishitakiwa nayo yalikuwa siyo makosa ya jinai kwa kukosa maneno muhimu kisheria kama inavyotakiwa katika kifungu cha 15 (1)(b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

katika hoja ya pili bwana mafipa amefafanua kuwa kifungu cha 21(1) (a) na kifungu cha 24 (8) cha sheria ya gharama za uchaguzi,sheria namba 6 ya mwaka 2010.ambacho mheshimiwa mungai na wenzake walishitakiwa nacho kilikuwa hakitengenezi kosa la jinai kisheria .

Aidha taasisi hiyo inakusudia kumkamata na kumfikisha mahakamani aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha soka nchiniTFF Fredrick Mwakalebela ili kujibu kesi kama hiyo ya rushwa ya uchaguzi mwaka 2010 baada ya rufaa yake inayofanana na ya mheshimiwa mungai kutupiliwambali na mahakama kuu kanda ya Iringa siku chache zilizopita.

Mungai na mwakalebela walikuwa wagombea ubunge katika majimbo ya mufindi kaskazini na Iringa mjini ambapo wote wanatuhumiwa kuwa walitumia ushawishi wa rushwa kwa wapiga kura katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi ccm.

MAHAKAMA KUU YAWATAKA WALIMU KUSITISHA MGOMO


MAHAKAMA KUU KITENGO CHA KAZI IMEPIGA STOP MGOMO WA WALIMU KWA MAELEZO KWAMBA HATUA ZILIZOPITIWA KUUFANYA NI BATILI. tAARIFA AMBAZO MTANDAO HUU UMEPATA ZINASEMA, MAHAKAMA HIYO IMEMTAKA KIONGOZI ALIYETANGAZA MGOMO HUO, KUTANGAZA MARA MOJA KUUSITISHA.