RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, LEODGAR CHILLA TENGA
MKUTANO
MKUU WA MWAKA 2012 WA TFF
Mkutano
Mkuu wa Mwaka (AGM) wa 2012 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
umefanyika kwa siku mbili (Aprili 21-22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF
Waterfront na kuhudhuriwa na wajumbe 104. Mkutano ulipokea taarifa, kufanya
uamuzi katika masuala mbalimbali na mengine yaliyojitokeza kama ifuatavyo;
EL
MAAMRY, NDOLANGA WATUNUKIWA URAIS WA HESHIMA
AGM
ilipitisha pendekezo la kuwatunuku urais wa heshima wa TFF, Alhaji Said Hamad
El Maamry na Muhidin Ahamadi Ndolanga lililowasilishwa na Mwenyekiti wa mkutano
huo ambaye pia ni Rais wa TFF, Leodegar Tenga.
Alhaji
El Maamry ambaye ni mjumbe wa heshima wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika
(CAF) alikuwa Mwenyekiti wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu
Tanzania (FAT) kuanzia mwaka 1973 hadi 1986. Alhaji Ndolanga aliongoza FAT
kuanzia mwaka 1993 hadi 2004.
BAJETI
YA MWAKA 2012
Bajeti
ya Mwaka 2012 ya sh. 7,246,628,650 kwa ajili ya matumizi ya TFF ilipitishwa.
Kwa mwaka 2012 TFF inatarajia kukusanya sh. 7,572,991,433 kupitia vyanzo
mbalimbali.
Vyanzo
hivyo ni viingilio vya uwanjani vinavyotarajiwa kuingiza asilimia 22 ya mapato
yote, udhamini (asilimia 74) na vyanzo vingine kama haki za matangazo ya
televisheni, ada za ushiriki wa timu katika mashindano mbalimbali, misaada
kutoka FIFA na CAF ambayo kwa pamoja vinatarajiwa kuingiza asilimia nne ya
mapato yote.
KAMATI
YA LIGI YA TFF
Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaendelea na mchakato
wa kupendekeza mifumo mitatu tofauti ya chombo kitakachosimamia/kuendesha Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ikieleza faida na athari za
kila mfumo uliopendekezwa na baadaye kuwafanya mawasilisho (presentation)
kwenye Kamati ya Utendaji.
Baada
ya kuwasilisha mifumo hiyo kwa Kamati ya Utendaji, Kamati ya Ligi itapendekeza
mfumo upi kati yao hiyo inaoona unafaa kabla ya kufanyika uamuzi wa mwisho.
Lengo
la kuunda chombo maalumu cha kuendesha ligi ni kuongeza ufanishi katika
uendeshaji wa VPL na FDL, na pia kuifanya Sekretarieti ya TFF kushughulikia
zaidi shughuli za maendeleo.
UUZWAJI
WA TIMU
Uuzaji
wa timu linabaki kuwa suala la kisheria. Lakini TFF imeweka utaratibu ufuatao;
lazima Mkutano Mkuu wa klabu husika uidhinishe uuzaji, na timu ikishauzwa
inabaki katika mkoa husika.
MFUMO
WA MASHINDANO
Kwa
vile kuna tatizo la ligi mbalimbali kuwa fupi, hali inayosababisha baadhi ya
wachezaji katika madaraja ya chini kucheza ligi zaidi ya moja katika msimu
mmoja, mfumo wa ligi/mashindano utaangaliwa upya.
Mfumo
uliopo sasa uliwekwa kwa ajili ya kuvutia uwekezaji katika mpira wa miguu
ambapo mwekezaji anaweza kuanzisha timu, na ndani ya miaka mitatu ikacheza Ligi
Kuu. Pili, ilikuwa ni kuondoa mlolongo mrefu wa ligi, na kuwafanya wanachama wa
TFF (mikoa) nao kuendesha ligi zao mikoani.
Ijulikane
kuwa ligi za mikoa (regional leagues) zinachezwa. Kwa sababu TFF inaendeshwa
kwa mfumo wa shirikisho (federation), nia ni wanachama wa federation nao kuwa
na majukumu ya kusimamia na kuendesha ligi, kwa vile TFF haiwezi kusimamia ligi
zote.
MAREKEBISHO
YA KATIBA
Mkutano
Mkuu wa TFF umepitisha marekebisho ya Katiba katika maeneo mawili; moja ni
kuanzisha Baraza la Wadhamini ambalo linatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua
watatu na wasiozidi watano.
Marekebisho
mengine ni kuongeza idadi ya kanda kutoka kumi na moja za sasa hadi 13.
Marekebisho hayo yamefanyika kutokana na Serikali kuongeza mikoa mipya ya
kijiografia.
Kanda
mpya sasa zitakuwa Kagera/Geita, Arusha/Manyara, Kilimanjaro/Tanga,
Katavi/Rukwa, Njombe/Ruvuma, Dodoma/Singida, Dar es Salaam, Shinyanga/Simiyu,
Mwanza/Mara, Lindi/Mtwara, Kigoma/Tabora, Mbeya/Iringa na Pwani/Morogoro.
Ukiondoa
mamlaka ya uteuzi aliyonayo Rais kwa mujibu wa Katiba ya TFF, wajumbe wote wa
Kamati ya Utendaji huchaguliwa kwa kanda.
HESABU
ZILIZOKAGULIWA
Mkutano
Mkuu ulipitisha hesabu zilizokaguliwa za mwaka 2010 (Audited Accounts) , na pia
kuiteua kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya TAC Associates kuwa mkaguzi wa hesabu
za TFF kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
YANGA
YAOMBA RADHI MKUTANO MKUU
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Yanga ambaye pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF
akiwakilisha klabu za Mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Bhinda aliwaomba radhi
wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa kitendo cha wachezaji wake kumpiga mwamuzi Israel
Nkongo kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam iliyochezwa Machi 10
mwaka huu.
Pia
alimuomba Rais wa TFF, Leodegar Tenga kutoa msamaha wa adhabu ya kulipa faini
iliyotolewa na Kamati ya Ligi ya TFF kwa wachezaji wawili wa Yanga ambao mpaka
sasa hawajalipa faini hiyo.
Rais
Tenga alimshukuru Bhinda kwa ujasiri alioonesha wa kuomba radhi mbele ya
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF kwa kitendo kile. Aliongeza kuwa kwa vile yeye
ni muumini wa kanuni, na adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kanuni hawezi
kutoa msamaha, hivyo wachezaji hao walipe faini hizo.
Pia
Rais Tenga alisema binafsi haziingilia kamati za TFF katika uamuzi ambao
zinafanya kwa vile zina watu waadilifu, na angekuwa yeye binafsi ndiye anayetoa
adhabu, angetoa adhabu kali zaidi kwa vile vitendo vya kupiga waamuzi
havikubaliki katika mchezo wa mpira wa miguu.
KANUNI
ZA NIDHAMU, MAHAKAMA YA USULUHISHI
Akizungumza
wakati wa kufunga mkutano huo, Rais Tenga aliwaambia wajumbe kuwa Kanuni za
Nidhamu (Disciplinary Code) za TFF na uundaji wa Mahakama ya Usuluhishi
(Arbitration Tribunal) ya TFF ambacho ndicho kitakuwa chombo cha juu cha kutoa
haki kwa masuala ya mpira wa miguu nchini vitakamilika mwaka huu.
Pia
TFF itaendelea kutafuta wadhamini kwa ajili ya timu za Taifa za vijana na
wanawake, itaendelea kuendesha semina na makongamano katika nyanja mbalimbali
za mpira wa miguu, kutengeneza mtaala wa academy na kutengeneza mpango wa
maendeleo (Comprehensive Plan) baada ya ule wa awali kumalizika mwaka huu.